Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,889
- 8,487
Umeongea ukweliWizara ile inahitaji mtu aliyetokea humo ndani mfano Tanroads au ambae ameitumikia kwa kipindi kirefu na kuielewa nje ndani network zote za barabara azitambue fika kiasi kwamba miradi inayoendelea/inayotazamiwa kuanza iwe kipaumbele na sio kupiga siasa huku akiwaachia katibu mkuu na watendaji wengine yeye akisubiri kusoma majibu tu bungeni. Bila kubanana na meneja wa mikoa (RMs) mambo hayaendi ipasavyo maana watawaacha wakandarasi watekeleze miradi wanavyotaka kwa visingizio visivyo na mashiko, kingine ni bajeti na vipaumbele kutiliwa mkazo, utiliwaji mkazo wa matumizi sahihi ya barabara ikiwemo adhabu kwa magari yote ( hasa malori) yanayoharibikia njiani na kuzuia watumiaji wengine na wale wanaomwaga mafuta au vilainishi barabarani