Miaka 18 ilitosha kudai mazungumzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 18 ilitosha kudai mazungumzo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Nov 22, 2010.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  jamani mimi nashangaa hawa watu wanaotaka mazungumzo
  kama njia ya kudai katiba walikuwa wapi miaka yote 18. Mfumo
  wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1992 kitu cha kwanza wapinzani
  kudai ilikuwa katiba mpya kwa njia ya mazungumzo lakini ccm walikataa miaka yote kwa sababu ktb iliyopo inawanufaisha. Kwahiyo nyie mnaodai (mkiwemo viongozi wa kidini na bahadhi ya wasomi )chadema watumie mazungumzo mlikuwa wapi siku zote hizi msiishinikize ccm ikubali mazungumzo hadi leo hii mnaishinikiza chadema itumie njia ya mazungumzo?? Mnaodai kuwa chadema ishinikize mazungumzo na ccm nendeni mkawaulize wakina mapalala, marando na wengineo kama njia hiyo itafanya kazi, wamejalibisha kwa miaka mingi jawabu msomaji unalijua. Njia hii ya chadema ni sahihi kwani kuanzia sasa jk kila atakaposafiri nchi yoyote duniani swali la kwanza kuulizwa kuhusiana na siasa za tanzania litakuwa swala hili la madai ya chadema kwani kumbuka kuwa siku ile kulikuwa na balozi nyingi za mataifa mbalimbali kwahiyo ujumbe huu umeshafika kwenye nchi zao. Miaka 18 inatosha kudai mazungumzo sasa imebaki vitendo tu hadi kieleweke.
   
Loading...