Miaka 10 ya Mtandao Vilivyotamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 10 ya Mtandao Vilivyotamba

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Dec 19, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Dec 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  MUONGO MMOJA WA MTANDAO

  Jinsi Rais wa marekani alivyotumia mtandao wa kimataifa kwa ajili ya kufanya kampeni zake za kuwania uraisi nchini marekani imebadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi watu wanavyoweza kutumia mitandao hii kwa ajili ya kufanya kampeni zao na jinsi ya kuwasiliana na watu wao .

  Upande mwingine ni jinsi waandamanaji wa nchini Irani walivyofanikiwa kutumia Mitandao jamii kama Twitter katika kuwasiliana na kubadilishana habari hii ilisaidia sana katika kufanya mabadiliko kidogo nchini wao , ingawa kwa sasa vyombo vya usalama vya nchi mbalimbali vinaanza kuingiza watu wao kwenye mitandao hii ili iwe sehemu ya wanachama ili kuweza kudhibiti hali hii .

  Pamoja na Facebook kutoka kuwa mtandao wa kijamii shuleni kufungiliwa milango kwa watu wengine zaidi kuweza kushiriki kwenye mtandao huo na kuwa mtandao bora zaidi wa jamii ulimwenguni watu wengi wameweka taarifa zao kwenye mtandao huo .

  Kwa wale wanaopenda kuandika na kuchangia mambo mbalimbali kwenye mitandao walifaidi sana ulipozinduliwa mtandao wa blogger , wordpress na mitandao mengine ambayo mtu anaweza kujisajili na kuanzisha blogu yake ambayo anaweza kuandika mambo mbalimbali jinsi anavyotaka lakini nzuri kuliko yote imekuwa ni Wikipedia ambao ni mtandao wenye makala nyingi kuliko yote duniani na ni mtandao unaotumia lugha nyingi kuliko mitandao yote duniani wikipedia ilianzishwa mwaka 2001 kama una mradi wako ungependa wengine washiriki katika mradi huo ni rahisi kuliko ilivyokuwa

  Kwenye upande wa matangazo mmoja ya vitu vilivyotia for a zaidi ni google adwords ambao ulianzishwa mwaka 2000 mtandao huu unaruhusu watangazaji kutangaza biashara zao kwenye huduma zote za google na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulipa matangazo yaliyoko kwenye baadhi ya blogu na tovuti kwahiyo kublogu imekuwa ajira kama zingine kuna watu sasa wanafanya kazi ya kublogu na wanalipwa kutokana na watu wanaotembelea blogu hizo ambazo zina bidhaa Fulani au habari fuleni .

  Mwaka 2001 kampuni ya napster ilifungiwa kutokana na kuruhusu watu kuchukuwa , kuruhusu watu kushirikiana miziki na kazi zingine za sanaa bure kupitia mtandao wao , kufungwa huku ndio ukawa mwanzo mpya wa watu kushirikiana zaidi kwenye kutoa , kugawa na kushiriki kazi za sanaa na programu za komputa ndio kampuni kama kazaa na ares zilipopata umaarufu kwa sasa kuna torrents na aina nyingine nyingi ya kuweza kupata kazi hizi .

  Hakuna mtu aliyefikiri kwamba ataweza tena kutafuta video za mwaka 1980 kwa mfano na kuzipata hata kuzihifahdi kwenye kompyuta yake lakini mwaka 2006 Mtandao wa YOUTUBE ulipoanzishwa yote haya yaliwezekana , unaweza kupata video za wanamuziki na wanasiasa za habari na vipindi vya televisheni , makala na mengine mengi sana ni wewe tu .

  Kuanzia mwaka 2010 binafsi nafikiri kampuni zitakazokuwa na ushindani zaidi kwenye masuala ya mitandao ni Msn Na Google haswa kwenye Search engine zao ingawa Google inaongoza kwa mbali dhidi ya Bing ya Msn pamoja na yahoo , google itaweza kusaidiwa sana na Browser yake ambayo ni Crome pamoja na programu zingine za kurahisisha kazi mbalimbali za kutafuta vitu kwenye mtandao na kwenye kompyuta .

  Kwenye upande wa programu Kampuni ya Microsoft inaweza kufanikiwa haswa baadhi ya kuamua kuwa na Antivirus yake inayoitwa Microsoft Essentials mpaka sasa imepata Hongera nyingi toka kwa watumiaji Mbalimbali walioijaribu mimi ni mmoja wao .

  Pamoja na yote hayo kitu ambacho nimeanza kuwa na hofu nacho ni jinsi Watu wanavyounganishwa kwenye mitandao hii kupitia vifaa vingine kama simu za mkononi ambapo mtu anaweza kuitumia kuhamisha pesa , kusurf na kufanya mambo mengine mengi , kama wahalifu wakifanikiwa kuvamia mitandao hii inaweza kuleta balaa kwa kundi kubwa sana la watu kuliko hata aina nyingine ya uhalifu unavyofanyika .

  Kwahiyo muongo ujao tujiandae kwa aina mpya za uhalifu ambazo zinatumia zaidi taarifa za watu ambao ziko kwenye mitandao au vitu vilivyopotea au hata wafanyakazi wanaohifadhi taarifa hizo kuamua kushirikisha wahalifu .

  Na mwisho ni suala la jinsi watu na vikundi vya watu wanavyoshiriki kwenye mtandao hii huko mbeleni kampuni zitalazimika kufuatilia wafanyakazi wao kwenye mitandao hii kujua wanafanya nini na kujua baadhi ya vitu wanavyoshiriki kuona kama zina maslahi kwenye kampuni wanazofanya au kwenye nchi wanazotoka wao .

  Hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo vilisaidia sana kupeleka maendeleo ya mtandao mbele kwa miaka 10 iliyopita ingawa kuna mengi zaidi ya haya hivi ni vile vinavyotumika katika maisha ya kila siku hata ukieleza mtu anaweza kukuelewa .
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2

Loading...