Miaka 10 ndani ya ndoa: Ahsante sana mke wangu!

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
68,012
95,358
Tarehe kama ya leo miaka kumi iliyopita ndipo nilipoanza maisha na huyu mke wangu.

Siwezi kutamba mi mwaminifu kivile, ila nashukuru sijawahi kufumaniwa wala kuhisiwa.

Sijawahi kumhisi wala kumfumania, kama ananicheat then she must be very smart (mwanachama hai wa ISC? katibu jina lake limokwenye list?)

Sijawahi kumchapa vibao wala kumtukana, pia sijawahi kutukanwa wala kunaswa vibao.

Tumewahi kukosana na kupishana kauli lakini hakuna jirani wala ndugu aliyejua.

Mi si mhudhuriaji mzuri kanisani, lakini watoto kanisani ni kama nyumbani kwao...matunda ya mama yao.

Naweza nisiwaone watoto kwa siku tano (mambo ya ulabu, na kuwahi kudamka asubuhi) lakini watoto wana afya njema na maendeleo yao shuleni ni mazuri sana....ahsante mke wangu!

Na mambo mengi sana anayafanya huyu mama, asingekuwepo sijui kama ningempata kama yeye!

Ahsante sana mke wangu...nakupenda sana....hakuna kama wewe! (Hizi infii ni tamaa za mwili, kudumisha mila na kuitikia wito wa necha, nisamehe bure mama watoto, sina jinsi kuzikwepa):loco::loco::loco:

Vijana nawasihi: Wapendeni wake zenu! Fuateni nyayo zangu Big Brother ODM!

:tea::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S-heart-2::A S-heart-2:
 
Hongera SANA mkuu!
This is great...unafanana na mimi kila kitu, kasoro kwenye ULABU na infidelity!
 
Hongera kamanda....inabidi tuwe na rule moja inayotaka infii kudumisha ndoa zako kama wewe...

BTW: Namtumia hii link mama matesha ili aone unavyompenda na kumjali...

FL1/Mom/Nyamayao etc hii inaitwa anniversary gani tena? Sio platinum ofkoz..
 
Ahsante kamanda....wanasemaga watu kuwa wanaume wasiopiga ulabu wana hobby zao nyingine...sijui ni kweli?
 
Lovely....
Sasa ukijitahidi kidogo tuu na kuachana na hizo infii ndio utakuwa unaudumisha vizuri upendo wenu....
Au we unaonaje...?!!
 
Hongera kamanda....inabidi tuwe na rule moja inayotaka infii kudumisha ndoa zako kama wewe...

BTW: Namtumia hii link mama matesha ili aone unavyompenda na kumjali...

FL1/Mom/Nyamayao etc hii inaitwa anniversary gani tena? Sio platinum ofkoz..

Sure katibu, lakini angalia usilikoroge ukachanganya na ile ya teamo....utaharibu mazima!
 
Lovely....
Sasa ukijitahidi kidogo tuu na kuachana na hizo infii ndio utakuwa unaudumisha vizuri upendo wenu....
Au we unaonaje...?!!

Hujui kuwa infii ndio zilinipa mauzoefu ya kuitunza ndoa yangu? 10 solid years siyo joke! I deserve standing ovation....karibu zero pub leo jioni...kuna ka geti tugeza ka kumpongeza biggie!
 
Tarehe kama ya leo miaka kumi iliyopita ndipo nilipoanza maisha na huyu mke wangu.

Siwezi kutamba mi mwaminifu kivile, ila nashukuru sijawahi kufumaniwa wala kuhisiwa.

Sijawahi kumhisi wala kumfumania, kama ananicheat then she must be very smart (mwanachama hai wa ISC? katibu jina lake limokwenye list?)

Sijawahi kumchapa vibao wala kumtukana, pia sijawahi kutukanwa wala kunaswa vibao.

Tumewahi kukosana na kupishana kauli lakini hakuna jirani wala ndugu aliyejua.

Mi si mhudhuriaji mzuri kanisani, lakini watoto kanisani ni kama nyumbani kwao...matunda ya mama yao.

Naweza nisiwaone watoto kwa siku tano (mambo ya ulabu, na kuwahi kudamka asubuhi) lakini watoto wana afya njema na maendeleo yao shuleni ni mazuri sana....ahsante mke wangu!

Na mambo mengi sana anayafanya huyu mama, asingekuwepo sijui kama ningempata kama yeye!

Ahsante sana mke wangu...nakupenda sana....hakuna kama wewe! (Hizi infii ni tamaa za mwili, kudumisha mila na kuitikia wito wa necha, nisamehe bure mama watoto, sina jinsi kuzikwepa):loco::loco::loco:

Vijana nawasihi: Wapendeni wake zenu! Fuateni nyayo zangu Big Brother ODM!

:tea::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S-heart-2::A S-heart-2:

Hongera kamati inafanya logistics ya kuandaa sherehe kidogo nawasiliana na viongozi wengine ila hapo kwenye red naangalia orodha ya majina kama nikikutana na jina lake nitakufahamisha ili tuone kama kuna agreement yoyote inaweza kufanyika pande zote mbili bila kuwa na matatizo yoyte yale
 
Sure katibu, lakini angalia usilikoroge ukachanganya na ile ya teamo....utaharibu mazima!

Niko makini sana...
Worry yangu ni asije akawa curious na kucheki ya Teamo...
 
hongera sana,mpe hongera na mkeo pia,she is a good wife and a good mother for ur children,kila la heri katika ndoa yenu,ndoa na iheshimiwe na watu wote
 
Babu na Bibi Yangu HONGERENI SANA KWA KUVUMILIANA.
MUNGU awajalie miaka 10 * 10 zaidi

Wenu Mjukuu
 
Hongera sana miaka 10 si mchezo mmevuka milima na mabonde hapo.

Mi lazima niige nyayo zako
 
Sijawahi kumhisi wala kumfumania, kama ananicheat then she must be very smart (mwanachama hai wa ISC? katibu jina lake limokwenye list?)
Nimedabo cheki jina lake halimo...
 
Hongera sana mkuu!
Leo ukamtayarishie (sio kupika, wanaume hawapiki wanatayarisha - prepare) mama matesha machalari ya kiti moto, lakini make sure umekitoa bandani mwenyewe---mdudu wa mbeya anapewa ARVs
 
Lovely....
Sasa ukijitahidi kidogo tuu na kuachana na hizo infii ndio utakuwa unaudumisha vizuri upendo wenu....
Au we unaonaje...?!!
kwa maelezo yake, upendo wake anaudumisha vizuri sana tu...nampa hongera kwa hilo
 
Hongera kamati inafanya logistics ya kuandaa sherehe kidogo nawasiliana na viongozi wengine ila hapo kwenye red naangalia orodha ya majina kama nikikutana na jina lake nitakufahamisha ili tuone kama kuna agreement yoyote inaweza kufanyika pande zote mbili bila kuwa na matatizo yoyte yale

Mkuu tunasubili hiyo sherehe kiongozi Kaizer umesha wasiliana nae?

Na mzigo wa Valuu weka wa kutosha sana mm nitakuja na mchumba.
 
Back
Top Bottom