Mi nililia kwa hasira,wewe je??

Mi nililia kwa hasira,wewe je??

trachomatis

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Posts
3,758
Reaction score
746
Takribani miaka kadhaa iliyopita,nilikuwa na galfriend ambaye alikuwa akitoka na mzee mmoja mwenye fedha zake. Ilichukua akili,muda na gharama kidogo kumuachanisha na huyo baba,kwa taaluma ni Eng.

Nilipiga sana simu,nilienda baa alizokuwa anakunywa,na kumsihi asimfuate tena yule dada.Alikubali.Akanishauri nimuoe kabisa,nami nikamwambia,ndiyo lengo langu.

Ndipo nilipotangaza nia ya kufunga pingu za maisha na yule dada,vikao vikaanza pale Riverside.
Jumamosi moja kabla ya Jumamosi ya harusi,mi na mchumba wangu tulienda duka moja maarufu kwa mapambo ya maharusi na sherehe kama hizo,ni K'koo jirani na mlango wa magari yanayoingia shimoni..


Nikiwa busy naangalia mapambo,mchumba wangu akiwa na furaha na bashasha tele, akanistua nigeuke,na nilipogeuka,hamadi uso kwa uso na Eng na midevu yake,akiwa na mkewe!
Nilimsalimia ye na mkewe na nikatokomea baa iitwayo Palace nikaanza kunywa kwa hasira.
Nilikumbuka taabu niliyopata kuwaachanisha,nililia na nikamwadithia mbaba wa kaunta..
 
Wadada wanaochukua waume za watu wana vituko vingi.. Wanaweza kukaa na wake za mabwana zao,mmama wala hujui!
Nikaona hapa,choo cha kike nimeingia..
 
Ulijuaje wakati yeye alimuona tu pale!Na kama ni furaha na bashasha tele alikuwa nazo kwa ajili yako,mbona ulimuhisi vibaya?

Hapana si kwa ajili yangu. Mi niko busy na mhindi,alipowaona akawachangamkia sana, kisha akanistua.
Nilitamani nimuulize yule mama katambulishwaje na mumewe,kuwa yule dada ni nani.Nilitamani.
 
Hapana si kwa ajili yangu. Mi niko busy na mhindi,alipowaona akawachangamkia sana, kisha akanistua.
Nilitamani nimuulize yule mama katambulishwaje na mumewe,kuwa yule dada ni nani.Nilitamani.
Kumbuka kuwa walikwishaachana na ndio maana hakuona taabu kukujulisha kuwa wapo mahali pale,hata hivyo mzee aliyekuwa anakula mali zako alikuwa na mkewe,tatizo lilikuwa wapi?

Ilifaa umuamini mwenza wako kwa wakati ule maana kilichokuwa akilini kwake si ngono zembe bali ndoa na alitaka uamini kuwa hakuwa na mahusiano tena na yule mzee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom