Mhudumu wa Songea

BigBro

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
3,210
9,861
Nilifika Songea nikaaa bar moja inaitwa Serengeti, mhudumu aliyekuwa ananuhudumia nikamuona anazungumza na dada moja mzuri sana. Yaani mzuri elewa hivyo.

Nikamuita nikamwambia yule dada uliyekuwa unazungumza nae nimemuelewa niitie, akasema yule ni mdogo wake mtoto wa baba yake mdogo ni mwalimu. Ila sahizi anarudi kwake alipita tu kunisalimia. Nikamwambia namtaka na wakati huo alishaondoka, akasema ngoja nimpigie, lakini simu yangu haina vocha.

Nikampunguzia 5000, akajiunga akampigia wakaongea sana, baadae akaja kuniambia kaelewa lakini hadi amalize kupika ndo atakuja.

Nikamwambia asipike aje ale hapa. Akaelewa.

Kosa nililofanya ni kumuambia chukua bia unywe, mimi huwa naagiza bia mbilimbili ndo utaratibu wangu, kumbe na yeye akawa anafanya hivyo hivyo akiwa na wahudumu wenzake watatu.

Basi yule mwalimu akaja tukanywa tukala, sasa wakati naletewa bili ili niondoke na bibiye nashangaa inasoma bia 36. Nikauliza vipi mimi nimekunywa nane na konyagi ndogo moja na mwalimu kanywa maji tu.

Akasema si nilimwambia anywe hivyo na yeye akawa anaagiza mbilimbili na wenzie watatu. Nikacheka tu, nikalipa nikaondoka na mwalimu tukafanya yetu, asubuhi nikaenda Mbinga kufanya lililonipeleka.

Wakati narudi nikapita tena Songea na nikaonana tena na teacher.
Nimerudi naendelea kuwasiliana na teacher, kasema mwezi wa tatu atakuja Dar kumsalimia mama yake mdogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom