Mhubiri wa kimataifa, Nabii Shepherd Bushiri atabiri Tanzania kuongoza nchi za Afrika kwa ugunduzi wa teknolojia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mhubiri wa kimataifa, Nabii Mkuu Prophet Shepherd Bushiri anayeongoza Kanisa la Enlighted Christian Gathering (ECG) la Afrika Kusini, ametabiri maajabu yatakayoishangaza dunia katika miaka saba ijayo kuanzia sasa, kwa Tanzania kuongoza nchi za Afrika kwa ugunduzi wa teknolojia.

Nabii Bushiri maarufu zaidi kama Major 1, pia amesema katika kipindi hicho, kutatokea ugunduzi katika nchi ya Tanzania kwa vijana wadogo kugundua vitu vingi vya kisayansi, kwa vile mkono wa Mungu uko juu ya nchi yao na nchi yao itaendelea kuimarika zaidi na Zaidi.

Nabii Bushiri yupo mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa Kimataifa wa siku tatu unaofanyika katika viwanja vya Ushirika.

Nipashe
 
Tapeli tu kama wengine.
Angehimiza watu wafanye kazi kwa ufanisi ,biashara ziimarike mingemuelewa.
 
Alishasema Mzee wetu mmoja atakufa na bado anadunda tu, na kwa nguvu ya mwenyezi MUNGU ataendelea kudunda, sina hamu naye huyu. Pia angalia hii FAKE MIRACLE ==> . Jamaa wanatupiga sanaaa hasa wadada.

Hata hivyo UTABIRI WAKE UNAKARIBISHWA SANA
 
Mhubiri wa kimataifa, Nabii Mkuu Prophet Shepherd Bushiri anayeongoza Kanisa la Enlighted Christian Gathering (ECG) la Afrika Kusini, ametabiri maajabu yatakayoishangaza dunia katika miaka saba ijayo kuanzia sasa, kwa Tanzania kuongoza nchi za Afrika kwa ugunduzi wa teknolojia.

Nabii Bushiri maarufu zaidi kama Major 1, pia amesema katika kipindi hicho, kutatokea ugunduzi katika nchi ya Tanzania kwa vijana wadogo kugundua vitu vingi vya kisayansi, kwa vile mkono wa Mungu uko juu ya nchi yao na nchi yao itaendelea kuimarika zaidi na Zaidi.

Nabii Bushiri yupo mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa Kimataifa wa siku tatu unaofanyika katika viwanja vya Ushirika.

Nipashe
Matapeli wakubwa
 
Huyu ni tapeli aliyekubuhu, I know him deep, mimi nilikuwa namkubali sana enzi za ujinga. Nilikuwa ukimsema huyu naumia mno, kumbe ni jizi kubwa. Kuna watu ukimsema watakutisha kwa vitisho vingi kiasi kwamba kama humjui Mungu wako unaweza kuogopa.
Hii dunia ni heri Yesu aje achukue kanisa lake linaloyumbishwa na hawa fake prophets.
Ushirikina unaofanywa na wafanyabiashara, uzinzi na uesharati unaopambwa kweupe nchi petu na duniani Mungu asimwonyeshe hivyo ili avikemee anamwonyesha mambo ya maendeleo.
Tanzania must back to God urgently.
 
Back
Top Bottom