Mhubiri wa Jamaica awasili nyumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhubiri wa Jamaica awasili nyumbani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Jan 24, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mhubiri wa Jamaica awasili nyumbani

  Mhubiri wa kiislam aliyefukuzwa kutoka Kenya kutokana na sababu za kuwa tishio kwa usalama, amewasili nchini kwao, Jamaica, ambako amehojiwa na polisi.

  Maafisa walisema mhubiri huyo, Abdullah al-Faisal, hakuvunja sheria yeyoye nchini Jamaica, lakini polisi walitaka kujua ni wapi wanaweza kumpata.

  Bw al-Faisal, ambaye alitumikia kifungo che jela nchini Uingereza kwa kuchochea mauaji, amaearifiwa kuwafahamisha polisi nchini Jamaica kuwa safari yake ya ndege ya siku mbili kutoka Kenya, iligharimu dola nusu milioni.

  Kwa uchache watu watano waliuwawa mjini Nairobi, baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe, ambao walikuwa wanadai kuachiliwa huru kwa Bw al-Faisal.

  Serikali ya Kenya ilimkamata Bw al-Faisal mwishoni mwa mwezi uliopita mjini Mombasa kwa madai ya kukiuka kanuni na uhamiaji.

  Source:BBC
   
Loading...