ndisinzowa
Member
- Aug 18, 2010
- 86
- 14
Nakumbuka..cuf ya haki ,haki sawa kwa wote asiyependa haki ....rip cuf
Cdm ingefikisha vibuda viwili!Nimetafakari kwa kina na nikagundua kumbe kweli yawezekana yakatukumba kama yaliyo wakumba CUF! Kwani inabidi CDM wawe makini katika kupokea mamluki na kuwapa nyazifa na dhamana kubwa ndani ya chama kabla ya kuwachunguza kiundani! Mfano mzuri ni yule jamaa aliyejitoa CCM baada ya kukosa kura kwenye kinyang'anyilo cha kura za maoni kule Arumeru Mashariki na hatimae akakimbilia CHADEMA na papo kwa papo akavuta fomu ya kuombe kuteuliwa kugombea ubunge! Mungu saidia kapata kura 8 je angepata kushinda kwenye kura za maoni si angetuuza?
CHADEMA TAFAKALI CHUKUA HATUA!.........
Wewe una mapenzi yasiyoona ukweli. Kinachonyemelea /kinachotokea kwa vyama vingine CDM is not an exception, ila wanaweza wakazuia kwa vile wameona mifano kwa wengine. Siyo kuwa anaombea itokee, anaipenda chadema ndio maana anaonyesha shimo isitumbukie!
Wakuu,
Ndo tabu ya kujenga demokrasia kwenye nchi masikini kama Tanzania, sio kazi rahisi hasa mafanikio yakishaanza kuonekana au kupata mafanikio kidogo sana, taasisi zinazoijenga demokrasia hasa vyama vya siasa husambaratika. Vikipona kusambaratika huushia kwenye migogoro isiyokuwa na kichwa wala miguu na hivyo vyama husika hudumaa>
Nchini tumeshuhudia kudumaa kwa NCCR-Mageuzi, TLP na sasa CUF inakoelekea SIO KUFA kama wengi wanavyotabiri isipokuwa KUDUMAA baada ya wanachama wengi wenye tija kwa chama kukihama na kuanzisha vyama vingine au kujiunga na vyama vingine.
Tafiti ndani na nje ya nchi zinaonyesha kuwa mara nyingi vyama hivi hudumazwa na migogoro ya ndani ya Chama ambayo huibuka mara tu baada ya kuanza kupata mafanikio kidogo katika harakati zao (mifano mizuri kwa hapa nchini ni NCCR-Mageuzi na TLP na sasa CUF).
Sioni namna ambayo Chadema wanakwepa shimo hili, either sioni juhudi zozote za kumulika na kuliona shimo hili zinazofanywa na Chadema,chama ambacho kiukweli kingeweza kutegemewa kuwa Chama mbadala au mshindani wa dhati wa CCM.
Najua kwa asili ya JF iliyojinyonyoa manyoya nitatukanwa na kubezwa lakini, hoja yangu hii nitaitunza na nitaileta hapa siku mambo yakiana kwenda kama nnavyo au tunavyoyaona wachambuzi wa mambo ya sayansi ya siasa.
Unaandika utumbo lakini unajua bila heading kuweka neno CDM hakuna atakayeifungua thread yako
katika post yako sijaona shimo lolote ulilolionyesha ili tusitumbukie zaidi ya utabiri,sadia na ueleze ni lipi hilo unaloliona linainyemelea gdm mbali na huo utabiri kuwa baada ya cuf ni cdm wakati kuna vyama vingine zaidi ya cdm lakini hujataka kuvitabiria.
alichosema mtoa maaada unapaswa kukitafakari sisi sote ni wana cdm lakini sio kwa maana ya kusifia kila kitu ambacho kimo ndani ya chama hata kama ni kibaya ikumbukwe kuwa bado kuna watu wanapenda ndani ya cdm kuona mgawanyiko kati ya mwkt na naibu katibu mkuu unakuwepo na kudumu kwa mda mrefu ili wao wapate nafasi ya kupika majungu kati ya mwkt (mbowe) na naibu katibu mkuu(zitto) hili pia ni tatizo tena wengi ni watumishi wa makao makuu ambao wana nafasi nzuri ya kushauri lakini hawafanyi hivyoCDM iko chini ya uongozi imara sana kwa sasa, we bakia na ndoto yako lakini CDM kumeguka sio leo.
After all CDM kwa sasa inaMEGA wengine. Tumeona aliyejiengua ubunge wa CCM Meru alimegukia CDM na hata makundi ya CCM yanayogombea madaraka yatamegukia CDM. Kumbuka hata akina Sitta walikuwa na option ya kuhamia CDM au kuunda CCJ but roho za usaliti na unafiki zikawazidi
Unayetamani CDM kumeguka utasubiri sana, sawa na Fisi kumfuata nyuma nyuma mlevi akidhania mikono ya mlevi itadondoka. CDM ina MEGA CCM
usitukane, jenga hoja. Utumbo ni nini. hapa ni majadiriano, sio kutukanana. Jenga hoja umbadilishe mwenzako. Sijapenda your way of putting arguments
kiukweli hapa tanzania demokrasia itakuwa ya kweli kama tukibakiwa na vyama viwili imara.utitiri wa vyama nalo ni tatizo lingine
Aisee hiyo ni cra p takatifu
nakuunga mkono bratha akitaka kujua cdm ni imara yeye aangalie hotuba za mwenyekiti wa ccm anavyo lala mika mfano ipo mingi akiwa mwanza jk anasema kwa sasa pesa hazitoshi inabidi muanze kutafuta vyanzo vingine vya mapato ruzuku imepungua(cdm imeongeza wabunge)...tumewanulia land cruise lakini hamfiki kunakotakiwa(hawana pesa za diesel)mabano ni maneno yanguBaada ya CUF inafuata CCM,dalili zimeanza onekana
Mkuu nilidhani umekula Ban teh teh, JF raha sanaUlitakiwa uziainishe hizo changamoto na utoe solution/suggestion