mhhh! BAADA YA CUF ,SASA CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mhhh! BAADA YA CUF ,SASA CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zamwamwa, Mar 3, 2012.

 1. z

  zamwamwa Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Ndo tabu ya kujenga demokrasia kwenye nchi masikini kama Tanzania, sio kazi rahisi hasa mafanikio yakishaanza kuonekana au kupata mafanikio kidogo sana, taasisi zinazoijenga demokrasia hasa vyama vya siasa husambaratika. Vikipona kusambaratika huushia kwenye migogoro isiyokuwa na kichwa wala miguu na hivyo vyama husika hudumaa>

  Nchini tumeshuhudia kudumaa kwa NCCR-Mageuzi, TLP na sasa CUF inakoelekea SIO KUFA kama wengi wanavyotabiri isipokuwa KUDUMAA baada ya wanachama wengi wenye tija kwa chama kukihama na kuanzisha vyama vingine au kujiunga na vyama vingine.

  Tafiti ndani na nje ya nchi zinaonyesha kuwa mara nyingi vyama hivi hudumazwa na migogoro ya ndani ya Chama ambayo huibuka mara tu baada ya kuanza kupata mafanikio kidogo katika harakati zao (mifano mizuri kwa hapa nchini ni NCCR-Mageuzi na TLP na sasa CUF).

  Sioni namna ambayo Chadema wanakwepa shimo hili, either sioni juhudi zozote za kumulika na kuliona shimo hili zinazofanywa na Chadema,chama ambacho kiukweli kingeweza kutegemewa kuwa Chama mbadala au mshindani wa dhati wa CCM.

  Najua kwa asili ya JF iliyojinyonyoa manyoya nitatukanwa na kubezwa lakini, hoja yangu hii nitaitunza na nitaileta hapa siku mambo yakiana kwenda kama nnavyo au tunavyoyaona wachambuzi wa mambo ya sayansi ya siasa.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Aisee hiyo ni cra p takatifu
   
 3. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  kuna wimbo unasema mwombee adui yako aishi miaka mingi aweze kuona mafanikio yako.mahubiri ya kushidwa tushayazoea nakumbuka nilpokuwa najoin mech engneer watu walinivunja moyo nitadisko wapi wewe nimemaliza chuo bila hata supu
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  Unachosema ni sawa kabisa.Wewe kweli ni mpenzi wa demokrasia. Huo ni wosia mzito ulioutoa. Chadema waufanyie kazi. Sijui kama wanasoma posting za JF. CCM inasimama kwa vile kuna mkono kwenda kinywani, na sio mapenzi ya dhati. Chadema mnaweza kujenga msingi wa mapenzi ya kweli kwa sababu hamna dola sasa. Watu wnaipenda chadema kwa siasa safi na uongozi bora. Umenena jambo kubwa sana. Bravo!!!!!
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mimi pamoja na kuipenda Chadema lakini naamini mtoa mada yupo correct kabisa kabisa. Mara nyingi ubadhirifu, ubaguzi kwa misingi yote ya ubaguzi, ubabe na kukosekana uwazi vinapotokea na kushamiri kwenye chama kuna kundi linalojitokeza linaloachwa 'yatima' sasa kwakuwa CCM wana vyombo vya kumonitor external and internal progress ya vyama hivi kwao ni rahisi kuwa notified na kuweka mkakati wa kipropaganda na mamluki kukiua chama husika. So ni kweli inawezekana baada ya cuf ikafata chdm
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Umejitahidi sana kueleza lakini napata taabu kidogo kwani hujaeleza nini unanakiona kwa mbali kama kingesababisha CHADEMA kudumaa japo kwa mifano tu

  Kwa hapa unacho sema ni utabiri utokanao na unajimu au ramri aidha unapenda kuwa siku moja itokee hivyo na unaombea itokee hivyo ndiyo kisa cha kutunza kumbukumbu hii
  Ungelikuwa msaada mzuri sana kwa CHADEMA kama ungelikuwa unaeleza wazi matatizo yaliyopo ndani ya chama ili kijirekebishe

  tatizo matatizo au migogoro mnayo unda ni ya kufikirika tu mfano UKABIRA, UKANDA na sasa UDINI vyote hivi mna prove failure

  Labda niseme wazi kuwa CHADEMA ni chama mbadala wa CCM ushahidi hata wewe unao practically na theoretically hata kama majina yanabadilika from CUF to ADC lakini bado CHADEMA inakubalika tu na ndiyo mkombozi wa kweli
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Unaandika utumbo lakini unajua bila heading kuweka neno CDM hakuna atakayeifungua thread yako
   
 8. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  CDM iko chini ya uongozi imara sana kwa sasa, we bakia na ndoto yako lakini CDM kumeguka sio leo.

  After all CDM kwa sasa inaMEGA wengine. Tumeona aliyejiengua ubunge wa CCM Meru alimegukia CDM na hata makundi ya CCM yanayogombea madaraka yatamegukia CDM. Kumbuka hata akina Sitta walikuwa na option ya kuhamia CDM au kuunda CCJ but roho za usaliti na unafiki zikawazidi

  Unayetamani CDM kumeguka utasubiri sana, sawa na Fisi kumfuata nyuma nyuma mlevi akidhania mikono ya mlevi itadondoka. CDM ina MEGA CCM
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu usijisumbue huyu ni kibaraka namba moja wa Magamba
   
 10. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Baada ya CUF inafuata CCM,dalili zimeanza onekana
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Safi sana mkuu wangu.Umempa live huyu magamba asiye na haya
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu.Angalia Arumeru wanavyotoana roho
   
 13. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Nimetafakari kwa kina na nikagundua kumbe kweli yawezekana yakatukumba kama yaliyo wakumba CUF! Kwani inabidi CDM wawe makini katika kupokea mamluki na kuwapa nyazifa na dhamana kubwa ndani ya chama kabla ya kuwachunguza kiundani! Mfano mzuri ni yule jamaa aliyejitoa CCM baada ya kukosa kura kwenye kinyang'anyilo cha kura za maoni kule Arumeru Mashariki na hatimae akakimbilia CHADEMA na papo kwa papo akavuta fomu ya kuombe kuteuliwa kugombea ubunge! Mungu saidia kapata kura 8 je angepata kushinda kwenye kura za maoni si angetuuza?
  CHADEMA TAFAKALI CHUKUA HATUA!.........
   
 14. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sina nyongeza ktk hili ila sioni kitufe cha ''THANKS''
   
 15. R

  RUTARE Senior Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi siyo mpenzi wala mwanachama wa chama cha siasa lakini kwa namna ninavyofuatilia siasa ya multiparty CDM hakitakufa jaribu kuangalia trend yake na utamaduni wa chama ni tofauti na vyama hivyo vingine kwa mfano NCCRM Mrema kakipotezea mwelekeo na waliobakia wakazidi kukosa mwelekeo hivo zile weakness za Mrema zikahamishiwa TLP ukizingatia TLP hakikuwa chama chenye nguvu kama NCCRM.after all mimi naamini CHADEMA kina potential people na viongozi wako makini ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi maoni haya tunayowapa
   
 16. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  ukweli hata uufiche kwenye mazingira magumu vipi! still ukitoka utakuwa ukweli tu. ni kweli tunapata mafanikio. Na kupata baadhi ya majimbo kwenye miji mikubwa kama Arusha ,Mbeya Dar,K'njaro na Mwanza ni hatua nzuri na ya kujivunia. watu wa mazingira haya wana access huduma nyingi za msingi kama Hospital,Umeme,shule kwa kujipimia uwezo wenyewe. Mtoa mada ni mtu anayeitakia CDM mafanikio. Wenzetu CCM wana Dola na wana fedha za kurubuni wapinzani wao. nadhani usingeita thread hii ****. huenda ikawa we ni miongoni mwa wale kuzoea vya kunyonga. Mafanikio haya ya CDM yamejengwa na watu waliopitia tabu nyingi sana mpaka kukifikisha chama hapa. Hivyo ipo haja liibuke kundi lingine la Viongozi na wanachama wa CDM tunaotakiwa kulinda mafanikio haya na kuhakikisha chama kinatoka kwenye intercities na kushuka kwenye Rural areas ili pasiwepo na matatizo ya wizi wa kura zetu wakati huu tunapoelekea kuchukua Tanzania yetu baada ya kumtoa mkoloni CCM
   
 17. M

  MYISANZU Senior Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulitakiwa uziainishe hizo changamoto na utoe solution/suggestion
   
 18. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Fungua macho nyanyua kichwa angalia mbali tatizo watu mnaitizama cdm kwa kumwangalia Mbowe na Slaa behind kuna vichwa vingi na makini sana tunamimini kuliko hata hao wawili nlowataja hapo na si watu wa kujionyesha bali wanakaa na kufikiria ni jinsi gani ya kuwasaidia watanzania niwataje kwa uchache
  Prof Baregu
  Prof Safari
  Dr Kitila
  Mzee wetu Mtei
  Unaweza ukaongeza list.....
   
 19. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mbona hamtaki kuona migogoro CCM,halafu haya mafundisho ya kushindwa ,woga,kufa ,kupotea ,kukata tamaa...yanatolewa wapi??wacha kuleta hisia zako binafsi za kushindwashindwa!
   
 20. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  Wewe una mapenzi yasiyoona ukweli. Kinachonyemelea /kinachotokea kwa vyama vingine CDM is not an exception, ila wanaweza wakazuia kwa vile wameona mifano kwa wengine. Siyo kuwa anaombea itokee, anaipenda chadema ndio maana anaonyesha shimo isitumbukie!
   
Loading...