Mheshimiwa Rais utatumbua jipu la katiba mpya (Sauti yetu) lini?

Kule Kwetu

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,157
1,893
Habarini Wadau,

Hili ni swali la msingi sana tulilo nalo sisi wananchi wa Tanzania. Tunashukuru kwa ujasiri na uthubutu uliothihirisha kwa kutumbua majipu katika baadhi ya vitengo na taasisi nyeti nchini.

ILA kumbuka tu kuwa Katiba iliyorasimiwa na Jaji Joseph Warioba ndio Sauti ya watanzania wanyonge walioona haja ya mabadiliko kadhaa katika katiba iliyopita.

Hayo ni MAONI NA MAHITAJI YETU WATANZANIA,endapo hutaipitisha katiba hiyo basi yoote uyafanyao ni sawa na kujilisha upepo kwakuwa sio hasa maoni ya watanzania na ni kinyume na demokrasia.

Mh. Rais John Pombe Magufuli Tunakuomba utupe katiba yetu watanzania.
 
Alisema wanainchi hawaitaji katiba mpya bali mabadiliko ya kweli yenye kuleta maendeleo kwa kasi, na nchi ipande iwe yenye kipato cha kati, na wala hakikua kipaumbele chake
 
Hivi kuna watu wanategemea mabadiliko kutoka kwa huyu Jamaaa .huyu ni mtu mnafiki ever bora jk alijitaidi hâta kuanzisha mchakato pamoja na kupingwa na chama chake huyu Jamaa ni muoga akiitwa pale Lumumba huwa anatia huruma .hana uwezo huo yupo kuwafurahisha walimuweka mtasibiri sana pale sio
 
Alisema wanainchi hawaitaji katiba mpya bali mabadiliko ya kweli yenye kuleta maendeleo kwa kasi, na nchi ipande iwe yenye kipato cha kati, na wala hakikua kipaumbele chake
Hayo mabadiliko yanayotakiwa na wananchi yaliainishwa wapi? Natumai unajua kuwa Katiba ninayomaanisha ni maoni ya wananchi.
 
upinzani waweke mkakati. kabla ya 2020 wahakikishe kwa njia yoyote katiba ya warioba inapita, hiyo ndio hatua ya kwanza kama kweli wana ndoto za kuja kitoa CCM madarakani. sio siri 2015 walichanga karata zao hovyo, badala ya kutumia nguvu nyingi kumnadi mgombea uraisi, walipaswa ku kita mizizi majimboni ili waweze kudhibiti bunge kwanza, na kama wangelikua ni watu serious 2015 ilikua ni golden chance. kushinda ubunge kwa katiba iliyopo ni rahisi kuliko uraisi. kwahiyo unaanza na kudhibiti bunge kisha mnabadilisha katiba, hapo sasa unaweza ukaanza kuota kuhusu kuchukua dola.
 
Sidhani kama Wapinzani wanaweza kuweka mkakati wa kuipata katiba kwa kutumia rasimu ya Warioba. Mwaka jana walishindwa kupeleka muswada bungeni wa kubadilisha baadhi ya vipengere vya Katiba ya sasa ili angalau kuwepo na Tume Huru!
 
Hivi kuna watu wanategemea mabadiliko kutoka kwa huyu Jamaaa .huyu ni mtu mnafiki ever bora jk alijitaidi hâta kuanzisha mchakato pamoja na kupingwa na chama chake huyu Jamaa ni muoga akiitwa pale Lumumba huwa anatia huruma .hana uwezo huo yupo kuwafurahisha walimuweka mtasibiri sana pale sio

Binafsi nadhani kunamabadiliko makubwa tumeyapata kutoka kwa Dr Joh Pombe Magufuli. Na ninamatumain mengi yatakuja, ila ninapopishana na Rais wetu ni kuwa hawezi kuyalinda mabadiliko haya bila madiliko ya Katiba. Na katiba pekee itakaypolinda haya mabadiliko, hata kama ni kiduchu kama ufuatiliaji na uwajibishaji wa watumishi wa umma, ni ile ya Mzee Warioba. Kama kweli ile katiba pendekeza ndiyo furaha ya chama cha mheshimiwa Rais basi afungue mazungumzo ili wananchi tuiboreshe kufikia katiba endelevu na yenye tija katika kulinda mabadiliko makubwa, madogo, kiduchu na kadhalika.

Nasikitika kama hakuna Katiba mpya yenye tija, mabadiliko haya yote yateleta mtafuruku na vurugu zaidi katika nchi yetu. Wabunge wote walioumizwa kwa kutolewa kwenye bodi za mashirika ya umma kwasababu ya mgongano wa maslahi na uvunjaji wa dhana ya utawala bora na uwajibikaji hususan mgawanyo wa madaraka/mamlaka na kazi kati ya mihimili mitatu ya dola itarudishwa kwa kasi endapo Dr John Pombe hatachaguliwa tena mwaka 2020. Vile vile, wale watumishi wa umma waliopteza ajira, mali na heshima kwa tuhumu ama ubadhirifu watarudi na kulipa visasi visivyotarajiwa. Tulinde chema/vyema kwa kuvikazia kwenye Katiba.
 
katiba mpya sidhani kama ni kipaumbele cha serikali hii iliyopo madarakani!
But ni kitu cha msingi kama watanzania wanaona umuhimu wa katiba mpya basi wangepewa.
 
Back
Top Bottom