Mheshimiwa Rais tunakuja kwako kuomba Msaada wa kununuliwa Mpunga, huku Mbarali kata ya Madibila hali ni mbaya sana, Mpunga umeshuka bei kutoka 65000, hadi 40000.
Na hiyo bei ya 40000 bado wanunuzi hawaonekani kabisa. NFRA walikuja wiki mbili zilizopita wakanunua Mpunga, kwa Sh 700 kwa kilo ya mpunga. Angalau ilitupa unafuu wa bei, tukashawishika kuuza kwao, lakini hawakukaa muda wakasema Mpunga walionunua umetosha, na kuacha kilio upya kwetu sisi tukiwa hatuna pa kupeleka zao letu.
Tunakuomba mheshimiwa Rais wetu, mtetezi wetu sisi wanyonge waruhusu hawa NFRA waendelee kununua Mpunga wetu, kabla walanguzi hawajaja kutumaliza. Tunajua wakigundua kwamba huku Madibila Mpunga umedoda, watataka kununua kwa bei ya Sh. 30000 kwa gunia. Na Sisi kwa hali ilivyo mbaya, tuna mikopo, lakini pia tunakaribia kuanza maandalizi ya msimu wa Kilimo, tutalazimika kuwauzia.
Ndiyo maana tunakuomba Raisi wetu warudishe hawa NFRA, angalau watuokoe.