Mheshimiwa Rais Magufuli tusaidie Wakulima wa Madibila

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,067
2,222
Mheshimiwa Rais tunakuja kwako kuomba Msaada wa kununuliwa Mpunga, huku Mbarali kata ya Madibila hali ni mbaya sana, Mpunga umeshuka bei kutoka 65000, hadi 40000.

Na hiyo bei ya 40000 bado wanunuzi hawaonekani kabisa. NFRA walikuja wiki mbili zilizopita wakanunua Mpunga, kwa Sh 700 kwa kilo ya mpunga. Angalau ilitupa unafuu wa bei, tukashawishika kuuza kwao, lakini hawakukaa muda wakasema Mpunga walionunua umetosha, na kuacha kilio upya kwetu sisi tukiwa hatuna pa kupeleka zao letu.

Tunakuomba mheshimiwa Rais wetu, mtetezi wetu sisi wanyonge waruhusu hawa NFRA waendelee kununua Mpunga wetu, kabla walanguzi hawajaja kutumaliza. Tunajua wakigundua kwamba huku Madibila Mpunga umedoda, watataka kununua kwa bei ya Sh. 30000 kwa gunia. Na Sisi kwa hali ilivyo mbaya, tuna mikopo, lakini pia tunakaribia kuanza maandalizi ya msimu wa Kilimo, tutalazimika kuwauzia.

Ndiyo maana tunakuomba Raisi wetu warudishe hawa NFRA, angalau watuokoe.
 
Poleni, mwaka huu kwa zao la mpunga sio mzuri. Mchele hapa Mbeya jiji umeshuka kutoka elfu 40 kwa kilo 20 hadi elfu 25.

Poleni sana aisee, wakulima tunapata shida sana. Hivi huko msimu mpya wa kilimo unaanza lini na mashamba kwa eka moja kukodi ni bei gani?
 
Si huko tu, mpunga umeporomoka maeneo mengi ikiwemo ukanda wa tabora
 
Bei ya Chato mpunga in l 42,000 kwa gunia.

Naomba bei ishuke zaidi, ili tusiolima tule jasho lenu.

Walanguzi walishaweka shehena ya kutosha kwenye magodauni yao na wamebakiza mpunga wa kutosha kwa mkulima.

Hadi Leo, tar 06-08-20 SAA 5 asubuhi alhamisi, bei ya mchele hapa ushirombo ilikuwa sh 1,000 kwa kilo.
 
kweli hali iko tofauti kwa mimi mkazi wa mafinga mchele kilo 1 ni 1400 bei ya mashineni kwa wewe mkazi wa madibila kama unajiweza njoo uukoboe uuze mchele town hapa
 
Poleni, mwaka huu kwa zao la mpunga sio mzuri. Mchele hapa Mbeya jiji umeshuka kutoka elfu 40 kwa kilo 20 hadi elfu 25.

Poleni sana aisee, wakulima tunapata shida sana. Hivi huko msimu mpya wa kilimo unaanza lini na mashamba kwa eka moja kukodi ni bei gani?
Msimu unaanza kuanzia mwezi wa kumi na moja.Mashamba ya kumwagiia hukodishwa kwa milion 1.2 hadi 3 kwa hekta.,yale ya mvua bei maelewano kuanzia laki nne kwa heka
 
Bei ya Chato mpunga in l 42,000 kwa gunia.

Naomba bei ishuke zaidi, ili tusiolima tule jasho lenu.

Walanguzi walishaweka shehena ya kutosha kwenye magodauni yao na wamebakiza mpunga wa kutosha kwa mkulima.

Hadi Leo, tar 06-08-20 SAA 5 asubuhi alhamisi, bei ya mchele hapa ushirombo ilikuwa sh 1,000 kwa kilo.
Wewe ni zaidi ya wapuuzi
 
Back
Top Bottom