Mheshimiwa rais Magufuli, leo nakukosoa

Mheshimiwa rais Magufuli, leo nakukosoa

Hapana mkuu Hatutakiwi kutukana watu wala kulaumu vyama .. wote ni pamoja TUTAFUTE MAKOSA PAMOJA . kusaidiane mawazo, pamoja , tumsupport raisi wetu na VISIONS zake pamoja . TWENDE MBELE KAMA ELIMU INAVYOTUELEKEZA... tukifuata principles za elimu na kuomba MUNGU pamoja NA kusaidiana pamoja kuwa na moyo mmoja TUTAKUWA ZAIDI YA USA NA CHINA
sasa kama unaambiwa adui wa taili ni ccm utaki,tutasaidiana vipi?au anataka nikuambie adui wa taifa ili ni Ardhi?
 
  1. Anasema kuwa Watanzania wengi wasomi wanashidwa kutumia elimu yao kwa manufaa ya nchi.
  2. Anasema Watanzania wengi wana "PhDs" wanashindwa kutengeneza au kutoa mazawo ktk suara la kuwa na viwanda
  3. Anasema wasomi wengi Wamebobea katika elimu wanashindwa kuisaidi nchi.
Makosa
Mheshimiwa Raisi huna wasomi unaowafikiria wewe. Kuwa mbunifu sio lazima uwe na PhDs au umebobea katika elimu. Kwani watu wengi waliosoma sana elimu ya darasani (theory) wanakuwa sio wabunifu na wengi wao wanaishia kufa masikini, wanapenda kukimbilia siasa kwani ndio njia nyepesi ya kupata pesa za wizi. nk. Angalia watu kama Zuckerberg, Billgate, Steven Job (RIP), Brendon na wengine. Hawana PhDs leo hii ndio wanabadilisha maisha ya watu duniani

Tanzania kuna watu kama Ally Mufuruki, Bakhressa, Mengi, na wengine wadogo wadogo sana kama Erick Shigongo, Kusaga, Zadoki hawana hata diploma wametengeneza kazi zaidi ya watu 70 kila mmoja, wamebadilisha maisha ya watu na familia zao. Na wanalipa kodi kuendeleza nchi hii masikini.

Asilimia 78 ya kazi Marekani zinatengenezwa na makampuni binafsi madogo madogo na yanachangia karibu asilimia 46 ya kodi. Ndio maana kila siku wanafundisha watoto wao elimu bora (theory +vitendo +life skills) hili wajasiriamali wazidi kuwa wengi hili wa isaidie Marekani kwenda mbele. Angalia China, Japani, Ujerumani wana system hii pia ya kuongeza na kuboresha viwanda vidogo


SOLUTION
  1. Tuache siasa za kizamani (wapinzani si maadui).
  2. Wapinzani wasipinge kushinda hoja tusaidiane nchi ni yetu wote
  3. Elimu yetu mbovu, imepitwa na wakati (acha kuamini PhDs kama unavyofikilia) amini vitendo kuliko midomo.
  4. Katiba Mbovu (unafanya kazi vizuri(nakupongeza) una ujasiri zaidi ya Nyerere. Lakini ukiondoka watarudia ya nyuma kwani katiba itawaruhusu kufanya maovu. Tubadilishie
  5. Viwanda vinaitaji elimu ya kitendo (hatuna), umeme (hatuna). Miundo mbinu (hatuna) mitaji (hatuna) Ali Mufuruki na wafanya biashara ambao wanajua wanafanya nini sio wanasiasa na wapiga domo wameshauri hili.
  6. Tunahitaji life skills (tuingize kwenye elimu yetu kuanzia vidudu mpaka vyuo vikuu na lazima kila mtu kusoma) ndio maana hatujui tunatoka wapi , tupo wapi tunakwenda wapi.. Mikelele tu

Ana PhD ameisaidiaje Tanzania miaka yote 20 aliyokuwa Mbunge na Waziri?
 
HAWANA MPHDS.... bro.... nimefanya kazi na ali miaka 6 kama mwenye kampuni na boss wangu. U miss a point think deeply on this. Tumefika hapa kwa ajili ya watu wenye mawazo kama yako... I KNOW CHANGE IS HARD.. but YES WE CAN CHANGE
Umeandika hata degree hawana una uhakika Mengi,Mafuruki na Zadoki hawana hiyo Elimu?
 
Cha kuongezea tu.
Kama kila mtu angefanya kazi yake kwa usahihi, tusingekuwepo hapa.

Yaan hapo bas!

Maana kuna kila aina ya chombo cha usimamizi katika kila nyanja, ila eti mpaka Rais aje kuchimba mabiti ndo mtu anawajibika.

Tunafanya kazi kwa kuvizia tu.

Tusiporekebisha hapo katika uwajibikaji, hakuna mabadiliko yoyote yatatokea. Kwa mfano sasa hivi jamaa amekaza vyuma, lakini bado kuna watu wameshapata upenyo wao, na wanaendelea tu kufanya nchi ni shamba lao. Wengine wameshakuwa miungu baada tu ya kupata madaraka. Inakuwa sio uajibikaji tena, bali inabaki kusubiri maamuzi ya mtu mmoja akijisikia tu mwenyewe.

Mwisho wa siku nakuunga mkono mtoa mada, kwamba ni suala la elimu. Watu wanafundishwa uzalendo ni kuchagua upande wa mtu fulani mwenye mamlaka.

Mtu anajiita mzalendo wakati hapendi maendeleo ya jirani yake, anataka ya kwake binafsi, anataka aibe, kila siku analopoka "mjini ujanja".

Utakuwaje mzalendo ukishachukia kundi fulani la watu? Ukiwachukia hao sasa unabaki na uzalendo kwenye taifa lipi? Wakati taifa ni watu. Au uzalendo ni kupenda nini hasa?

Elimu ianze kwenye uzalendo kwanza. Maana hatujui uzalendo ni kupenda nini. Na ukisema nchi, unamaanisha ni nani/nini hasa.

Otherwise, tutaendelea na kurushiana vijembe tu, hata aingie nani madarakani
 
Tumumekuwa hatuwatumii maprofesa wetu vizuritumewaingiza kwenye siasa na mambo ambayo hawakusomea na hivyo tumewaweka katika mazingira magumu ya kuonyesha uwezo wao wa kielimu huku tukiamini watafanya wonders. Pili bado wasomi wetu hawalipwi wanavyostahili na hivyo kuwapa wasisi juu ya maisha yao ya baadae (baada ya kustaafu) ukikumbuka hawa watu wametumia muda mwingi wa maisha yao katika kujielimisha zaidi na hivyo muda wao wakutumika kazini unakuwa umepungua. Kwa nchi nyingi zilizoendelea nimeona maprofesa wamekuwa washauri wakubwa wa serikali katika fani walizobobea na hivyo kuleta mapinduzi makubwa kwenye nyanja mbalimbali.
 
Hapana mkuu Hatutakiwi kutukana watu wala kulaumu vyama .. wote ni pamoja TUTAFUTE MAKOSA PAMOJA . kusaidiane mawazo, pamoja , tumsupport raisi wetu na VISIONS zake pamoja . TWENDE MBELE KAMA ELIMU INAVYOTUELEKEZA... tukifuata principles za elimu na kuomba MUNGU pamoja NA kusaidiana pamoja kuwa na moyo mmoja TUTAKUWA ZAIDI YA USA NA CHINA
Kuilaumu Chama kilichotufelisha siyo kutukana mtu!! Bila kukilaumu hicho chama wala hawatajua wapi tunaangukia

Kuhusu wasomi na elimu yetu ni kuwa watu wamejifunza theory zaidi, ubunifu na mitaji ni matatizo makubwa ukilinganisha na sera za mabenki ya nchi yetu.
 
Tatizo ni kwamba mh anaamini kuwa msomi anayeisaidia nchi na mzalendo ni yule ambaye ambaye anasema ndiyo kwa kila kitu,msomi anayepinga na kukosoa huyo haisaidii nchi na siyo mzalendo.

Wakati maendeleo ya nchi yanaletwa kwa kuwasikiliza wasomi wote,wanaosema ndiyo na wanaosema hapana.

Kwenye mikataba mibovu ya madini wangesikilizwa wasomi waliosema hapana nchi isingefika mahali ilipofika,kwenye uuza wa nyumba za serekali wasomi waliokosoa mpango huo wangesikilizwa kusingekuwa na ulazima wa serekali kuingia gharama za ujenzi wa nyumba serekali.

Kwenye uuzaji wa viwanda wasomi waliopinga mpango huo wangesikilizwa serekali isingekuwa inahangaika na ujenzi wa viwanda vipya.
 
Angiza bia nakuja kulipia hiyo ndio tunaita open-minded sio kusifia ujinga ujinga
 
Ukijaribu kutoka kwenye dream world na ukaingia kwenye real world mleta uzi umeona panapo takiwa kuonwa
 
Mtoa mada m
  1. Anasema kuwa Watanzania wengi wasomi wanashidwa kutumia elimu yao kwa manufaa ya nchi.
  2. Anasema Watanzania wengi wana "PhDs" wanashindwa kutengeneza au kutoa mazawo ktk suara la kuwa na viwanda
  3. Anasema wasomi wengi Wamebobea katika elimu wanashindwa kuisaidi nchi.
Makosa
Mheshimiwa Raisi huna wasomi unaowafikiria wewe. Kuwa mbunifu sio lazima uwe na PhDs au umebobea katika elimu. Kwani watu wengi waliosoma sana elimu ya darasani (theory) wanakuwa sio wabunifu na wengi wao wanaishia kufa masikini, wanapenda kukimbilia siasa kwani ndio njia nyepesi ya kupata pesa za wizi. nk. Angalia watu kama Zuckerberg, Billgate, Steven Job (RIP), Brendon na wengine. Hawana PhDs leo hii ndio wanabadilisha maisha ya watu duniani

Tanzania kuna watu kama Ally Mufuruki, Bakhressa, Mengi, na wengine wadogo wadogo sana kama Erick Shigongo, Kusaga, Zadoki hawana hata diploma wametengeneza kazi zaidi ya watu 70 kila mmoja, wamebadilisha maisha ya watu na familia zao. Na wanalipa kodi kuendeleza nchi hii masikini.

Asilimia 78 ya kazi Marekani zinatengenezwa na makampuni binafsi madogo madogo na yanachangia karibu asilimia 46 ya kodi. Ndio maana kila siku wanafundisha watoto wao elimu bora (theory +vitendo +life skills) hili wajasiriamali wazidi kuwa wengi hili wa isaidie Marekani kwenda mbele. Angalia China, Japani, Ujerumani wana system hii pia ya kuongeza na kuboresha viwanda vidogo


SOLUTION
  1. Tuache siasa za kizamani (wapinzani si maadui).
  2. Wapinzani wasipinge kushinda hoja tusaidiane nchi ni yetu wote
  3. Elimu yetu mbovu, imepitwa na wakati (acha kuamini PhDs kama unavyofikilia) amini vitendo kuliko midomo.
  4. Katiba Mbovu (unafanya kazi vizuri(nakupongeza) una ujasiri zaidi ya Nyerere. Lakini ukiondoka watarudia ya nyuma kwani katiba itawaruhusu kufanya maovu. Tubadilishie
  5. Viwanda vinaitaji elimu ya kitendo (hatuna), umeme (hatuna). Miundo mbinu (hatuna) mitaji (hatuna) Ali Mufuruki na wafanya biashara ambao wanajua wanafanya nini sio wanasiasa na wapiga domo wameshauri hili.
  6. Tunahitaji life skills (tuingize kwenye elimu yetu kuanzia vidudu mpaka vyuo vikuu na lazima kila mtu kusoma) ndio maana hatujui tunatoka wapi , tupo wapi tunakwenda wapi.. Mikelele tu
Point zako nyingi nakubaliana nazo.
 
TATIZO sio raisi wetu.. kumbuka elimu yetu mbovu tangu kipindi cha NYERERE. WASOMI wetu ni product ya elimu mbovu.. nikiwa namaana hakuna vitendo ktk elimu yetu ndio maana tunashindwa kubadilish theory kuwa PRACTICAL..kukbuka hata masomo ya Art , biashara, jamii YANA PRACTICALS PIA Mfano mtu mwizi, mwongo, siomwaminifu, HATA AWE ANAVYETI GUNIA ZIMA HAJASOMA. tunafikilia elimu ni vyeti.. NDIO MAANA WALIOSOMA SANA HAWANA VITENDO... wamebaki midomo tu
Sidhani kama hiyo ndio sababu (kwamba shida ni elimu yetu). Wapo watu wamesoma nje ya nchi, kuanzia degree zao za kwanza hadi za 3 huko yaani PhD but nao ni wale wale tu.
 
  1. Anasema kuwa Watanzania wengi wasomi wanashidwa kutumia elimu yao kwa manufaa ya nchi.
  2. Anasema Watanzania wengi wana "PhDs" wanashindwa kutengeneza au kutoa mazawo ktk suara la kuwa na viwanda
  3. Anasema wasomi wengi Wamebobea katika elimu wanashindwa kuisaidi nchi.

Makosa
Mheshimiwa Raisi huna wasomi unaowafikiria wewe. Kuwa mbunifu sio lazima uwe na PhDs au umebobea katika elimu. Kwani watu wengi waliosoma sana elimu ya darasani (theory) wanakuwa sio wabunifu na wengi wao wanaishia kufa masikini, wanapenda kukimbilia siasa kwani ndio njia nyepesi ya kupata pesa za wizi. nk. Angalia watu kama Zuckerberg, Billgate, Steven Job (RIP), Brendon na wengine. Hawana PhDs leo hii ndio wanabadilisha maisha ya watu duniani

Tanzania kuna watu kama Ally Mufuruki, Bakhressa, Mengi, na wengine wadogo wadogo sana kama Erick Shigongo, Kusaga, Zadoki hawana hata diploma wametengeneza kazi zaidi ya watu 70 kila mmoja, wamebadilisha maisha ya watu na familia zao. Na wanalipa kodi kuendeleza nchi hii masikini.

Asilimia 78 ya kazi Marekani zinatengenezwa na makampuni binafsi madogo madogo na yanachangia karibu asilimia 46 ya kodi. Ndio maana kila siku wanafundisha watoto wao elimu bora (theory +vitendo +life skills) hili wajasiriamali wazidi kuwa wengi hili wa isaidie Marekani kwenda mbele. Angalia China, Japani, Ujerumani wana system hii pia ya kuongeza na kuboresha viwanda vidogo


SOLUTION
  1. Tuache siasa za kizamani (wapinzani si maadui).
  2. Wapinzani wasipinge kushinda hoja tusaidiane nchi ni yetu wote
  3. Elimu yetu mbovu, imepitwa na wakati (acha kuamini PhDs kama unavyofikilia) amini vitendo kuliko midomo.
  4. Katiba Mbovu (unafanya kazi vizuri(nakupongeza) una ujasiri zaidi ya Nyerere. Lakini ukiondoka watarudia ya nyuma kwani katiba itawaruhusu kufanya maovu. Tubadilishie
  5. Viwanda vinaitaji elimu ya kitendo (hatuna), umeme (hatuna). Miundo mbinu (hatuna) mitaji (hatuna) Ali Mufuruki na wafanya biashara ambao wanajua wanafanya nini sio wanasiasa na wapiga domo wameshauri hili.
  6. Tunahitaji life skills (tuingize kwenye elimu yetu kuanzia vidudu mpaka vyuo vikuu na lazima kila mtu kusoma) ndio maana hatujui tunatoka wapi , tupo wapi tunakwenda wapi.. Mikelele tu
Point of Correction Mengi ni Dr. Mengi pia ni CPA(T) holder rudi kwenye mafaili yako mzee
 
Back
Top Bottom