Mheshimiwa Rais Magufuli, kwa heshima kubwa ya Kiurafiki katuwakilishe mazishini Havana

Kwanza ujumbe wa maombolezo umeshatumwa? Watu kibao wame-tweet kuomboleza sijaona wa kutoka hapa kwetu bado.
 
Magufuli aende kufanya nini. Huyo Castrol mwenyewe HATAZIKWA ila ATACHOMWA moto Jumamosi ijayo mpaka awe JIVU (Cremated) kulingana na alivyotoa usia wake.

Sasa kum subject rais wetu Magufuli kushuhudia UCHOMAJI wa MWILI ni KUMUUMIZA kisaikolojia. Hata mimi mwenyewe siwezi kudhuhudia kichwa kikipasuka aisee!!

Hiyo haiingii akilini na si desturi zetu za kiafrika kuhudhuria tukio kama hilo!
Rambirambi zinatosha
Hii ikiwa ni pamoja na kuweka sahihi katika kitabu cha rambirambi ubalozini.
Huo ni mtazamo wangu binafsi!
 
kwa sisi wengine tuliokulia miaka ya 80 tunajua na tunakumbuka jinsi gani Cuba walivyo tusaidia kwa hali na mali ( Nasubiri kusoma makala za Ma professa Nizar Visram, Rweikiza Mkandala,mke wa marehem Haroub Othman, Issa Shivji, na bila kumsahau jenerali ulimwengu)

Je Mtukufu Rais wetu John Magufuli atakwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye huu msiba ambao marais wengi toka Africa ambao wanakumbuka mchango wa Cuba kwenye liberation movements.

Natumai Magufuli atakwenda kwenye Mzishi na sio kutuma watu waende kuiwakilisha nchi
Nauli utalipia ww!??
 
Makamu wa Rais na Waziri mkuu wapo, ataenda mmoja wapo
 
Fidel Castro atachomwa moto leo jumamosi. So zile mbwembwe za misafara na kuaga aga maiti KINAFIKI huku ukiangalia ilipo CAMERA hakuna. Enzi zile za Giza Vasco Da Gama angetimba Havana na msururu wa watu 76. Ati kutoa salamu za Pole.
 
Mchango mkubwa aliyoufanya katika bara hili hatuwezi kumlipa yeye au watu wa Cuba.

Kama sio Fidel Castro leo kuna uwezekano nchi za Kusini mwa Afrika zingekuwa bado kwenye mikono ya Makabaila.

Wanajeshi wa Cuba, katika vita huko Angola, Walionyesha Uzalendo mkubwa sana na waliamini wanapigana na Mabeberu kulinda ardhi ya mama yao "Mother Land".

Nchi nyingi hupigana vita kwa ajili ya manufaa fulani kama tulivyoona uvamizi wa nchi fulani na fulani kwa ajili ya Mafuta.
Lakini Cuba ilituma majeshi yake huko Angola kulinda hadhi ya Mwafrika. Hadhi ya Binaadamu. Na hawakutaka malipo yeyote.

Rais Mandela alimpa heshima na kumuita Fedel Castro "Wewe ndio Rais Wangu".
Wanamapinduzi, poleni kwa msiba.
Huu ni Msiba mzito sana na msiba wa wote sisi.

Kama akituma hizo salamu, ningependa ASITUMIE Twita....Na kama akituia TWITA, basi isiwe kama ile ya Pongezi za TRAMPU.
 
Rest in peace Fidel Castro! Mengine yoooooote yatabaki story
But in few days to come! NOTHING IS THE NUMBER WHEN YOU DIE
 
Back
Top Bottom