Mheshimiwa Rais Magufuli, kwa heshima kubwa ya Kiurafiki katuwakilishe mazishini Havana

Ung'eng'e tatizo ase, hawezi kwenda labda amtume PM au Vice President.
 
Kwanza nianze kwa kuwapeni wale ' Wanamapinduzi ' wenzangu wote kwa ' Msiba ' mkubwa sana uliotokea muda si mrefu wa ' kuondokewa ' na Rafiki yetu mkubwa sana Tanzania aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro.

Hakuna asiyejua kuwa urafiki wetu Tanzania na Cuba ni wa ' Kihistoria ' kabisa hasa ukizingatia kuwa ' uliratibiwa ' vizuri mno na Kiongozi huyo wa Kihistoria wa Cuba na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hizi nchi mbili zimefaidika mno kwa ushirikiano wa Kisiasa, Kilimo, Biashara bila kusahau Kiulinzi na Kiusalama.

Ndipo kwa Heshima na taadhima kabisa huku nikijua kuwa Mheshimiwa Rais wetu ana ratiba ngumu kabisa na majukumu mengi ya kututumikia sisi Watanzania na mara nyingi amekuwa akituma wawakilishi wako katika mambo kadhaa huko nje ya nchi hasa Makamu wake Mama yetu Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim ila kwa huu ' msiba ' mzito na mkubwa wa Kidunia tunamwomba sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ' akatuwakilishe ' moja kwa moja Watanzania na ' tutafarijika ' sana.

Naomba ' uzi ' huu usieleweke vibaya labda kama nataka kumpangia Rais nini cha kufanya kwani kiukweli hata uwezo huo sina ila ' nimeguswa ' na huu ' msiba ' mzito kabisa kutokana na Historia zetu hizi nchi mbili na Urafiki wetu wa shida na raha na Watu wa Cuba.

Poleni sana Watanzania mlioguswa kama Mimi na huu ' msiba ' na pia pole zao kubwa Wananchi wa Cuba kwa kuondokewa na Revolutionary Icon na True Hero Mzee Fidel Castro na ama hakika ametuachia kumbukumbu na legacies nyingi mno sisi Wanamapinduzi ambayo bila shaka inabidi sasa tupite mule mule ambapo ' Marehemu ' alipita.

Nitoe pia pole zangu kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) kwani najua kuwa tulikuwa na ' ushirikiano ' mkubwa na mzuri mno na Watu wa Cuba hasa ukizingatia kuwa ' Marehemu ' alilipenda na kuliheshimu mno Jeshi letu la Tanzania na hakuna ubishi kuwa asilimia fulani za ' uzuri ' na ' ufanisi ' wa ' kiutendaji ' wa Jeshi letu pendwa na zuri la JWTZ pia zilichangiwa na Millitary Philosophies za Mzee Fidel Castro.

Nimtakie tu maziko mema Mzee Castro na may his soul rest in peace. Jembe la ukweli na la Kimapinduzi limeondoka na ' ubora ' na ' utamu ' wake.
Mkuu bukoba imemshinda ndiyo itakuwa Cuba
 
Very ' foolish ' Mkuu. Wewe unajua labda muda huo Marehemu Castro alikuwa na ratiba gani au amekumbwa na nini? Kwa umekaa mwenyewe ukatafakari na kujipanga kisha ukaona uje na a very ' blanket ' post kama hiyo yako humu kwa Ma Great Thinkers? Unajua maana ya dharura? Wewe hujawahi kuwa na ' Msiba ' labda wa ' Mshikaji ' wako kabisa lakini kutokana na kukumbwa au kubanwa na ratiba fulani ukashindwa kuhudhuria mazishi yake? Halafu nadhani ungeusoma vizuri ' uzi ' wangu wala usingetudhihirishia ' uwehu ' wako wa ' kifikra ' humu kwani kuna mahala nimesema kabisa kuwa namwomba tu Mheshimiwa Rais ' akatuwakilishe ' huko ' mazikoni ' Havana ila sijamlazimisha aende kwani sijajua ratiba zake. Nilichokifanya ni kumwaomba na kumshauri tu na siyo kumlazimisha hasa ukizingatia sina pia huo uwezo wa kumpangia na kumlazimisha yeye nini cha kufanya. Siku nyingine jikite mno katika kuelewa ' content ' ya ' uzi ' tafadhali.

Duh. .....povu jingi kama la foma vile kwa kiswali kidogo tu cha kizushi

hata sijahangaika sana kusoma hilo povu lote baada ya kujijibu wewe mwenyewe hapa;

"Wewe unajua labda muda huo Marehemu Castro alikuwa na ratiba gani au amekumbwa na nini?"
 
kwa sisi wengine tuliokulia miaka ya 80 tunajua na tunakumbuka jinsi gani Cuba walivyo tusaidia kwa hali na mali ( Nasubiri kusoma makala za Ma professa Nizar Visram, Rweikiza Mkandala,mke wa marehem Haroub Othman, Issa Shivji, na bila kumsahau jenerali ulimwengu)

Je Mtukufu Rais wetu John Magufuli atakwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye huu msiba ambao marais wengi toka Africa ambao wanakumbuka mchango wa Cuba kwenye liberation movements.

Natumai Magufuli atakwenda kwenye Mzishi na sio kutuma watu waende kuiwakilisha nchi
Kaka ni afadhali asiende atatutia aibu. Ataongea kwa lugha ipi?
 
Nyerere alivyoaaga dunia, Castro alikuja TZ?
Hadi anakufa, Castro alinusurika majaribio zaidi ya 600 ya kutaka kumuua. Wamarekani na CIA yao walifanya kila njia lakini hawakufanikiwa.
Ilikuwa lazima asafiri kwa tahadhali kubwa sana!
 
Upo sahihi Mkuu japo naona katika hao Marais ' Wastaafu ' umemsahau na Vasco Da Gama jr ila sina uhakika kama ' Kiprotokali ' italeta picha fulani hivi nzuri hasa hasa kwa ' urafiki ' wetu mkubwa niliouelezea hapo juu. Kama Mheshimiwa Rais yupo vizuri na anaweza tu aka ' adjust ' ratiba zake kwenda kwake Havana ' mazishini ' kutaimarisha mno ule ' Ukomredi ' wetu.
Vasco Da Gama ni mliberali zee la North hapa alikua ana fit huyu mzee au inawezekana siasa zake anazozifanya hazijui ni za mlengo gani?
 
Upo sahihi Mkuu japo naona katika hao Marais ' Wastaafu ' umemsahau na Vasco Da Gama jr ila sina uhakika kama ' Kiprotokali ' italeta picha fulani hivi nzuri hasa hasa kwa ' urafiki ' wetu mkubwa niliouelezea hapo juu. Kama Mheshimiwa Rais yupo vizuri na anaweza tu aka ' adjust ' ratiba zake kwenda kwake Havana ' mazishini ' kutaimarisha mno ule ' Ukomredi ' wetu.
Unapata sifa gani duniani na mbinguni kuacha kuhani kwa msiba wa mwanao wa kumzaa badala yake ukaomboleza wa majirani?
 
Very ' foolish ' Mkuu. Wewe unajua labda muda huo Marehemu Castro alikuwa na ratiba gani au amekumbwa na nini? Kwa umekaa mwenyewe ukatafakari na kujipanga kisha ukaona uje na a very ' blanket ' post kama hiyo yako humu kwa Ma Great Thinkers? Unajua maana ya dharura? Wewe hujawahi kuwa na ' Msiba ' labda wa ' Mshikaji ' wako kabisa lakini kutokana na kukumbwa au kubanwa na ratiba fulani ukashindwa kuhudhuria mazishi yake? Halafu nadhani ungeusoma vizuri ' uzi ' wangu wala usingetudhihirishia ' uwehu ' wako wa ' kifikra ' humu kwani kuna mahala nimesema kabisa kuwa namwomba tu Mheshimiwa Rais ' akatuwakilishe ' huko ' mazikoni ' Havana ila sijamlazimisha aende kwani sijajua ratiba zake. Nilichokifanya ni kumwaomba na kumshauri tu na siyo kumlazimisha hasa ukizingatia sina pia huo uwezo wa kumpangia na kumlazimisha yeye nini cha kufanya. Siku nyingine jikite mno katika kuelewa ' content ' ya ' uzi ' tafadhali.
Wrong answer to a very simple question.
 
Wakuu hivi wapi panauzwa mashati ya kikamanda kama ya fidel...

Nataka ninunue hata mawili hivi..!
Just to keep his revolutionary thoughts with me..
 
Naona asiende Bali hiyo hela ya kugharamia safari ikafanyie ukarabati shule za ruvu, kibiti, kilosa na ifakara zote za sekondari zilizojengwa na watu wa CUBA miaka 1970s
 
Back
Top Bottom