Mheshimiwa Rais, kuna tatizo zaidi ya lishe duni

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Pengine hili hulifahamu basi naomba ulizingatie kwenye mamlaka yako huko mbeleni pamoja na utafiti
Vumbi la kongo na supu ya pweza ni sehemu ndogo tu tena isiyo na madhara kwenye sehemu kubwa yenye tatizo kubwa zaidi kitaifa

1. Vijana legelege
Mashuleni hakuna tena kazi za kuwafanya vijana wawe wakakamavu, hakuna tena miradi ya kuwakomaza misuli na viungo vingine mwilini

2. Mashindano na vipindi vya michezo mbalimbali mashuleni kuanzia soka, mpira wa wavu, kukimbia, sarakasi nknk. Siku hizi michezo inayopewa chapuo ni kukimbiza kuku nk. Viwanja vya michezo vimeuzwa mitaani na mashuleni. Wizara ya michezo ipo busy na mambo mengine, kubet kumekuwa ndio kama mchezo wa taifa

3. Matumizi makubwa ya kujichua kwa jinsia zote mbili
Ambapo sasa teknolojia ya kutumia midoli/vikaragosi vyenye maumbo yanayofafa sana na sehemu za siri za jinsia zote mbili. Hili tatizo linatishia kupungua kwa kizazi cha kesho huko mbeleni

4. Mabinti kutokana na changamoto za maisha kuingia kwenye mahusiano kwenye umri mdogo sana na watu wazima sawa na baba na babu zao.. Kiasi kwamba wakikutana na vijana wa umri wao ni sawa na kipande cha mua kwenye rambo

5. Vyakula vinavyodumaza, kulegeza kusinyaza na kufubaza nguvu za mwili, kama haya mayai na kuku wa kufugwa wanaokuzwa kwa madawa yenye madhara makubwa mwilini

6. Matumizi makubwa ya energy drinks zinazonywewa kiholela na kwa wingi mno
Ni kweli viwanda vinatoa ajira lakini madhara ya hivi vinywaji vitaliangamiza taifa lenye vijana wakakamavu na wenye afya nzuri

7. Matumizi makubwa ya vilevi vikali vya bei rahisi
Hapa hakuna tofauti na namba sita na hili ni la mamlaka za nchi, TBS, MAMLAKA YA CHAKULA NA MADAWA, WIZARA YA AFYA NK.. Hivi vinywaji vinawamaliza vijana.

8. Ujio wa bodaboda
Pamoja na kwamba ni ajira lakini huu usafiri umeleta ulegevu mkubwa kwa vijana! Sasa hivi vijana hata kilometa moja wanapanda boda!

9. Miili na viungo vya vijana havishughulishwi tena, wakipata muda ni kubet, kucheza game kwenye simu, tv nk

Vumbi la kongo na supu ya pweza havina madhara kama hivyo vingine vyote hapo juu. Mchuzi wa pweza ni chakula cha kawaida kabisa cha kila siku. Kuna hii alkasusi nayo ni ya kuangaliwa kwa karibu.

Hawa wauza energy na mayai na mabroiler na pombe kali ni wahujumu uchumi wakubwa, kwakuwa wanatengeneza wagonjwa wa baadae watakaokuja kununua dawa zitakazaingizwa na hao hao waliowauzia hivyo vyakula na vinywaji.

Ni kama tu ujio wa bodaboda ulivyohamasisha na kukuza biashara ya vyuma, wheel chairs, miguu na mikono bandia, magongo nknk bila kusahau madawa na vifaa tiba.

Mama Samia ninayo mengi ya kukupa uyafanyie kazi lakini nisikuchoshe sana. Angazia hayo kwanza! Supu ya pweza ni tiba sio janga.
 
Mkuu Mshana umenena vyema sana. Kongole kwako.

Pengine ulitakiwa kuwa katika sehemu ya wafanya maamuzi katika hili taifa ungelisaidia sana

(Au na wewe ndio ungezikalia akili kama akina fulani joke)
 
Mkuu Mshana umenena vyema sana. Kongole kwako.

Pengine ulitakiwa kuwa katika sehemu ya wafanya maamuzi katika hili taifa ungelisaidia sana ...

(Au na wewe ndio ungezikalia akili kama akina fulani joke)
Hahahah
 
Naona mama anawaruka wateja wake wa sekta binafsi juu ya Maarifa wanayotoa kuwa ni sehemu ya vifaa vya kutufanya uharibifu, yaani Vyakula na madawa.

Maana haya maarifa wanayotoa ndio sabab kuu ya vijana kuwa hv tulivyo.
 
We are living in a confusing and corrupted world. Haya yanayotokea hapa kwetu yanatokea ulimwenguni kote. Kuna tafiti moja imefanyika Marekani,inaoonyesha zaidi ya 25% ya ndoa zinakabiliwa na changamoto ya kupata watoto. Ikiwa ni ongezeko kubwa.
 
Mazoezi na vyakula halisi siku hizi nadra mabungo, ukwaju, kungu, mapumbu ya paka, miwa, korosho,
 
Pamoja na visababishi vilivyoainishwa, kungekuwepo pia mkakati mahsusi wa kitaifa, wa kuhamasisha ulaji wa vyakula vyetu vya asili.. hizi 'chipschips' za mfululizo hazifai hata kidogo
 
Lifestyle inabadilisha vingi sana.

Ila bado kuna vingi vya kubadilisha.
 
Back
Top Bottom