Mheshimiwa Rais, December daraja halikuisha na Mhandisi hajajinyonga...

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,374
72,891
Ukiwa Mwanza ulijiapiza kuwa daraja la waenda kwa miguu Rock city Mall kuwa lazima liwe limeisha na kuanza kutumika kabla ya Chrismas 2016 na kuwa kama litakuwa bado basi Mhandisi muhusika kwa vile ni Mhehe ajinyonge kabisa.

Watu tulikuamini, lakini pamoja na tabia zetu watu wa nchi hii kupiga makofi na kusahau hili hatujasahau.

Je, ahadi ile ilikuwa ya uongo? Daraja bado na hakuna taarifa zozote za mtu kujinyonga kwa kushindwa kumaliza kazi kwa wakati.

Je, tujenge tabia ya kuamini kuwa usemayo majukwaani ni promo tuu na sio jambo la kutilia maanani kuwa ni kauli thabiti? Huoni kuwa hii inajenga hulka ya kuona kuwa unatoa kauli kwa mtindo wa comedy?

Tungoje wale watu wako waje wakujibie kuwa tulikunukuu vibaya kwani zile zilikuwa mbwembwe tuu!
 
Huyo Mkandarasi huenda ana sababu za msingi.Ni bora apewe nafasi ya kujieleza kwanza kabla ya kuhukumiwa.
 
Kama ungefuatilia ziara aliyokuwa Kagera majibu yalikuwa wazi kabisa pale
 
Ukiwa Mwanza ulijiapiza kuwa daraja la waenda kwa miguu Rock city Mall kuwa lazima liwe limeisha na kuanza kutumika kabla ya Chrismas 2016 na kuwa kama litakuwa bado basi Mhandisi muhusika kwa vile ni Mhehe ajinyonge kabisa.
Watu tulikuamini, lakini pamoja na tabia zetu watu wa nchi hii kupiga makofi na kusahau hili hatujasahau. Jee ahadi ile ilikuwa ya uongo? Daraja bado na hakuna taarifa zozote za mtu kujinyonga kwa kushindwa kumaliza kazi kwa wakati.
Jee tujenge tabia kuwa usemayo majukwaani ni promo tuu na sio jambo la kutilia maanani kuwa ni kauli thabiti? Huoni kuwa hii inajenga hulka ya kuona kuwa unatoa kauli kwa mtindo wa comedy?
Tungoje wale watu wako waje wakujibie kuwa tulikunukuu vibaya kwani zile zilikuwa mbwembwe tuu!

Ukiwa Mwanza ulijiapiza kuwa daraja la waenda kwa miguu Rock city Mall kuwa lazima liwe limeisha na kuanza kutumika kabla ya Chrismas 2016 na kuwa kama litakuwa bado basi Mhandisi muhusika kwa vile ni Mhehe ajinyonge kabisa.
Watu tulikuamini, lakini pamoja na tabia zetu watu wa nchi hii kupiga makofi na kusahau hili hatujasahau. Jee ahadi ile ilikuwa ya uongo? Daraja bado na hakuna taarifa zozote za mtu kujinyonga kwa kushindwa kumaliza kazi kwa wakati.
Jee tujenge tabia kuwa usemayo majukwaani ni promo tuu na sio jambo la kutilia maanani kuwa ni kauli thabiti? Huoni kuwa hii inajenga hulka ya kuona kuwa unatoa kauli kwa mtindo wa comedy?
Tungoje wale watu wako waje wakujibie kuwa tulikunukuu vibaya kwani zile zilikuwa mbwembwe tuu!
789c583d54caabc09cec3525bef7b778.jpg

Kama haliko tayari hili hapa juu ni kitu gani?,mleta uzi acha uchochezi basi
 
Haya atakusoma na labda kutomtumbua sababu, mengi hutokea ambayo yanaeleweka kwanini ado hawajamaliza.
 
Back
Top Bottom