Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwa mara ya kwanza tunasikia mbunge akiona ni kero anapoombwa fedha na wananchi. Tena anaenda mbali na kujifananisha na ATM. Hii ni kauli ya ajabu sana kuweza kutolewa na mwakilishi wa wananchi. Nidiriki kusema kuwa sijapata kusikia wabunge wanalalamika eti wananchi wanawaomba sana fedha. Hii ni mara ya kwanza kusikia kauli hiyo. Kama wapo wabunge walikuwa wanalalamika basi huenda walikuwa wanafanya hivyo kimya kimya.
Mheshimiwa Mwita Waitara, Ubunge ni dhamana. Ukumbuke kuwa hizo fedha unazolalamika zinatolewa kama kwenye ATM zinatokana na wananchi wenyewe. Hao wananchi unaowalalamikia ndio waliokupigia kura na ndio wenye fedha. Hivyo ni haki yao wanapokueleza kero zao na wewe usaidie kuzitatua. Uliomba kazi hiyo kwa kuamini utaweza na utabeba mizigo yote hivyo una wajibu wa kuwatumikia.
Hizo fedha ulizonazo si zako bali ni za wananchi. Wewe ni kama mashine za ATM tu na wananchi wana haki ya kuchukua wakati wowote ili watatue shida zao. Ni kama zile ATM za kwenye mabenki. Itakuwa ni jambo la ajabu ikitokea meneja wa Tawi la Benki akilalamika eti wananchi wanachukua sana fedha walizoweka kwenye akaunti zao kupitia ATM Mashine za matawi yake. Ikifikia hatua hiyo basi huyo meneja anapaswa kupimwa akili.
Wana Ukonga wana kero nyingi, kubwa na ndogo. Ni wewe ndiye uliyeomba kazi ya kutatua kero hizo. Hivyo si jambo la ajabu wananchi wanavyokuomba fedha kwani ni haki yao kufanya hivyo. Waulize wabunge wazoefu akina Zitto Kabwe, Halima Mdee na hata John Mnyika. Watakuambia. Na wao wanaokbwa fedha na hawalalamiki kwa vile wanajua ni wajibu wao kuombwa. Waombe wakupe ushauri watakusaidia na si kulalamika hovyo hovyo.
Najua hofu yako inatokana na kutafuna hovyo fedha za mfuko wa Jimbo. Tangu upate fedha hizo, hujapeleka hata senti moja kwenye miradi ya wananchi. Tunasikia tu wabunge wa maeneo mbalimbali wakitoa fedha kuchangia maendeleo. Ila kwa upande wako hujafanya hivyo licha ya wananchi kukabiliwa na changamoto mbalimbali.
Nikushauri tu ndugu yangu Waitara. Kazi ya Ubunge huiwezi. Tena imekushinda mapema hata miaka miwili haijafika. Umechoka mapema mno. Kama unaona ubunge unakutesa, si lazima ukae madarakani kwa miaka yote mitano. Unaweza kuachia ngazi mapema ili wachukue Wanyamwezi waliozoea kubeba mizigo mizito.