polokwane
JF-Expert Member
- Dec 16, 2018
- 3,359
- 5,808
Kwa hili TAMISEMI kaeni mfikiri upya mzigo mnao watwisha walimu ukiachilia mbali mzigo wa vipindi walio nao si haki na si sawa
Na CWT mpo kimya hata hamfuatilii mkaona ni madhila gani walimu walio chini ya chama chenu wana nyanyasika na kusurubishwa kwa kazi ambayo hawakuisomea na wala hawana ujuzi nayo.
Wakuu wa Wilaya wanadhalilisha walimu , wanawaweka ndani na maneno ya dhihaka sababu ya ujenzi wa madarasa? Mlifikiriaje kuwatwisha mzigo huu walimu?
Kwanini hizo pesa za ujenzi msiziingize kwenye account za vijiji au kata au hata halmashauri ili walimu waendelee na kazi yao ya kufundisha watoto? Mda mwingi walimu wanahangaika na mambo ya ujenzi hao wananchi wenyewe ushiriki wao duni sana sababu mmesha ingiza siasa huko, kwanini mnawaongezea majukumu walimu tena mazito yenye masimango na kuviziana?
Nasema kuviziana sababu vitu vingi vilivyo andikwa kwenye BOQ zenu haviakisi uhalisia wa bei zilizoko sokoni pia kuna vitu vingi sana havipo kwenye BOQ zenu wakati katika uhalisi vina gharimu pesa tena sana
Wakuu wa wilaya wana waweka ndani walimu kisa ujenzi umechelewa au upo chini ya kiwango, jaman hivi mwalimu aliye jifunza kushika chaki na kupiga kelele na wanafunz darasa la pili leo anahangaika na size za nondo ? Anahangaika na ratio za cement , ahangaike na mafundi wezi na wadokozi ambao ukipepesa macho tu wameshafichaa kilo 2 za misumari yaani siku nzima upo na ujenzi hayo kayasoma wapi kwenye cheti chake hata akastahili kusimangwa nankuwekwa mahabusu akiyakosea?
Lakini pia swala hili limeathiri sana ufundishwaji wa watoto huko madarasani maana mda mwingi ni vikao vya kamati na kuandaa mihutasari ya vikao kusimamia mafundi bado asimamie mitihani na asahihishe na kupanga matokeo ya mitihani ya wanafunzi hapo achilia mbali kuingia darasani kufundisha vipindi vyote tabu tupu huko.
Kibaya zaid TAMISEMI tarajieni kupata majengo ya hovyo kuwahi kutokea kwa sababu zifuatazo
1. Kuna baadhi majengo yamejengwa na tofali mbichi kabisa
2. Hatua za ujenzi kitaalamu hazikuzingatiwa kabisa kwenye majengo mengi kwa sababu:-
Tofali inafyatuliwa leo kesho inajenga 😅😅😅😅 speed ya mwanga bora majengo na sio majengo bora kila mkuu wa wilaya anataka kabla tarehe 15 decemba 2021 awe wakwanza kukabidhi bora jengo sio jengo bora.
muwe na huruma nyie watu fedha hizi ni za mkopo tutalipa wakati majengo yatabomoka ndani ya miaka 5-10.
USHAURI: Kwanini TAMISEMI fedha hizi msiingize mapema sana ili kupunguza huku kufanya kazi kwa pressure kubwa na speed ambayo inachochea kabisa kupata majengo majengo yasiyo bora kabisa?
Lakini pia kwanini TAMISEMI msiingize fedha hizi kwenye account za vijiji au kata ili wao waunde kamati zao huko za vijiji na wananchi wasimamie ujenzi na walimu muwaache waendelee na wajibu wao ambao ni mzito sana kulingana na wingi wa wanafunzi? Hebu kaeni mlitafakari upya na kwa umakini swala hili hali si nzuri hata kidogo.

- Mkuu wa wilaya naye ni makandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
- Mkurugenzi naye ni mkandarasi akienda site naye anamaelekezo yake
- Afisa elimu naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
- Ofisa tarafa naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
- Mwenye kiti CCM wilaya naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake hapo bado mkuu wa mkoa, afisa tawala mkoa, Mwenyekiti wa Ccm mkoa na wengineo yaan miluzi hadi mbwa haelewi aende wapi.
- Engineer wilaya naye ni mkandarasi akienda site naye anatoa maelekezo yake tena ya kitaalam