Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

We nae kichwa kigumu, smart phone gani??.
Una hisi wote walikuwa na smart phone mzee.

HAKU kuwa na computer??, simu za button zilikuwa Zina ingia online.
My father alikuwa nayo, na nime itumia sana
Labda unaongelea Blackberry curve, lakini Blackberry hizo zilikuwa ni smartphone, mwaka 2006 kama hauna access ya laptop wengi tulitumia Blackberry kuingia Jambo forum, mara nyingi sipendi kuzurura na laptop.
 
Ewaa, ni hiyo hiyo mkuu, ile kitu ilikuwa hatarii sana.

Sema black berry Ali shindwa kuendana na soko, I phone ana leta kitu Cha ku touch, ye ana leta ma button Tena.

Bora Nokia ali jiwahi mapema.
 
Mwenzenu napata taabu kidogo, sijui jinsi gani Mheshimiwa huyu ashawishiwe na kukubali ombi hili. Natamani sana John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama sio sasa kwa sababu za taratibu za CCM, basi zamu inayofuata.

Vyovyote iwavyo, naamini huyu bwana anafaa kila kona uwanjani anapocheza siasa. Hata PhD aliyoipata majuzi inaongezea chachandu tu, kwamba hatababaishwa na vyeti vya udaktari wa kupewa zawadi tu, maana anayo real one.

Sina uhusiano naye kabisa huyu mtu na wala sijawahi kukaa naye au kuonana karibu, lakini vitu vyake mwisho bwana. Naamini atachagua timu ya washauri inayofanana naye.

Hata kama anayo mapungu yake kama binadamu, the good outways the bad, wakati mwingine analazimika kufanya vitu vingine kwa kuwatii wakubwa zake, lakini akishika rungu mwenyewe nashawishika (sidanganyiki) kwamba ataifaa Tanzania ya sasa.

Leka
Kipindi hcho Niko mwaka wa kwnza by then
 
Najua JPM ni mchapakazi mzuri zaidi ya mawaziri wengine wengi kama siyo wote, ni mfuatiliaji mzuri wa watu wa chini yake, ana uwezo wa kujieleza, kujenga hoja na kizisimamia hata pale hoja hizo zinapokuwa na upinzani wa dhahiri - mfano ni uuzwaji wa nyumba za serikali.

Tatizo langu na huyu jamaa ni moja tu si msikilizaji mzuri na anaweza kuwa "dictator" mzuri sana hasa pale mitazamo na misimamo yake itakapokuwa kinyume na maslahi ya nchi - refer uuzwaji wa nyumba na ubadilishwaji wa ramani ya barabara kuu kupitia wilayani kwao. Wakati wa uuzwaji wa nyuma za serikali JPM alikuwa na majibu ya kejeli - kama ya bosi wake Mkapa - kwa wale wote waliokuwa wanahoji busara ya zoezi lile. Ni aina ya mtu ambaye anapenda kutumia hoja za nguvu badala ya nguvu ya hoja pale anapokabiliwa na wapinzani makini wanaohoji busara za maamuzi na matamshi yake.

Tatizo letu Tanzania ni la kimfumo zaidi kuliko kiongozi mmoja mmoja. Tuna mfumo ambao hauna vidhibiti mwendo kwa kiongozi mkuu kabisa wa nchi na wateule wake hasa pale wanapoamua kushirikiana kuifilisi nchi. Ninashawishika kuamini kuwa hata kama utamweka JPM kama mfumo ni huu huu wa kuwa na imperial president hakuna jambo la maana atakalofanya zaidi ya kujitwalia chake mapema. JPM katika mfumo wetu wa sasa hana tofauti na Benjamin William Mkapa.

Katika mfumo wa sasa nadhani JPM anaweza kuwa mtendaji mzuri akiwa waziri mkuu na apewe mamlaka kamili ya kuwasimamia na kuwawajibisha mawaziri wote.
Uliona mbali sn
 
Uliona mbali sana, na hakika ombi lako lilitimia nasi tukafaidika kwa kupata kiongozi bora wa muda wote

Mungu ampumzishe kwa Amani Mwamba

Back
Top Bottom