Ndugu yangu "senior expert member" sitaki kuamini kwamba tunachokijadili hapa hukijui na ndo maana unatoa mapendekezo ambayo kwa mtazamo wangu "hayawezi kusaidia". Nataka nikukumbushe tu kwamba hitaji la umeme sio hitaji dogo la kufanyia harambee kama mnavyofanya kwa ajili ya kicheni party, send-off, harusi au kuchangia mtoto aliyekosa ada ili aende shule. Tunaongelea hitaji la mamilioni, kama sio mabilioni ya pesa ili kuendesha miradi mikubwa ya kuzalisha umeme.
Mkuu gharama unazotoa sasa na unazoingia sasa kwa kukosa umeme ni maradufu kuongeza na kodi zako pia unazotoa.., ni ukweli usiopingika kwamba gharama ya kutumia generator moja moja ni zaidi ya gharama za kutumia generator za Tanesco za mafuta mazito.., ofcourse long term solution ni kuondokana na tegemezi la umeme wa mafuta na Tanzania tuna vyanzo vingi sana, hapa ndio serikalin inabidi ije na miradi ya kufaa (ambacho mpaka sasa hawajafanya..) hivyo basi tufanye nini ili tuweze kuwaforce wafanye kazi zao..., iwapo sisi wananchi tunaweza kuonyesha njia tutawaondolea kile ambacho kila siku wanasema hakiwezekani (kama wewe ulivyosema hapo juu) na hivyo basi watashindwa kuwadanganya wananchi kwa issue ya umeme ni ngumu...
Pia tunaweza kuwahamasisha vijijini watu wakatumia Bio-fuel ambako umeme hautafika leo wala kesho.
Kumbuka pia kwamba mafuta yanayohitajika si kwa kiasi cha kufanyia harambee kama unavyopendekeza. Hayo yote tisa, la mwisho, ambalo kimsingi ndiyo hoja yangu, nataka kukumbusha kwamba kama ni harambee wananchi tumefanya nyingi na za kutosha, na bado tunaendelea kufanya kwa ajili ya kutatua matatizo tuliyonayo kwa maendeleo ya nchi yetu-ikiwa ni pamoja na umeme.
Pengine utajiuliza tunafanya harambee hizo kwa njia gani! Jibu liko wazi: Ni kupitia kodi yako na yangu, na ya watanzania wote. Mimi binafsi nalipa zaidi ya Tsh 150, 000 kama kodi ya mapato kila mwezi-achilia mbali kodi kubwa ninayolipa kupitia kununua bidhaa na huduma itokanayo na VAT. Wewe pia unajua ni kiasi gani unalipa na wengine wote. Hata kama hulipi kodi ya mapato kwa maana ya kwamba wewe si mfanyabiashara wala mfanyakazi katika sekta rasmi (serikali na taasisi zake au mashirika ya umma na binafsi), bado unalipa kodi nyingi tu kupitia kila kitu unachonunua maana kuna kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ambayo inajumuishwa katika garama ya kila bidhaa unayonunua au huduma unayolipia.
Mkuu hakuna mtu anayeibisha kwamba serikali inabidi ituangalie kwa pesa inazochukua, na maliasili zetu inazochezea, tena inabidi sio kutupa umeme tu, bali hata afya ya bure, elimu ya bure na uhakika wa kutuangalia tunapozeeka.., lakini swali ni kwamba je wanafanya hivyo...?, au tuendelee kukaa tu mpaka watakapoanza kufanya hivyo...??
Hivyo ni vema watanzania tukajua kwamba heal inazozitumia serikali ni hela zetu. Kwa lugha nyingine: Watanzania tunaji-mobilize kila siku kufanya harambee kupata hela ambazo ndizo akina Jairo na wengine wanazitumbua. Kwa msingi huo sioni mantiki ya hoja ya watanzania "kuji-mobilize kwa hali na mali" ili kondokana na matatizo tuliyo nayo ilihali tayari tumejimobilze vya kutosha. Itoshe watanzania tukaelewa kwamba wale tuliowapa dhamana ya kuzitumia hela hizo kutuletea maendeleo wameamua kuzitumia kwa namna wanayojua wao ili wajiletee maedeleo yao binafsi kwa jasho letu watanzania.
Ndio maana nikauliza upinzani (ambao kila siku unatuambia kwamba wenyewe wakiingia madarakani mambo yatakuwa mazuri) tena nikamuuliza na waziri kivuli wa hii wizara.., kwamba tunafanya nini?, kama ataweza kumobilize watu na kufanya kitu hata kama ni kidogo tu na kwa kitongoji au mtaa mmoja anaweza akasema unaona nilichofanya..?, tena bila kuwa na kodi za wananchi..., kwahiyo tukipewa serikali tutafanya makubwa zaidi..., na huu utakuwa mtaji mkubwa wa kuweza kuwangoa serikali kwa upinzani kuonyesha they can do better.
KWA MSINGI HUO, NAKUBALIANA NA HOJA YA WATANZANIA "KUJI-MOBILIZE" LAKINI KWA LENGO MOJA TU, NALO NI "KUIONDOA SERIKALI YA SISIEMU AMBAYO IMELEWA NA KUJISAHAU KIASI KWAMBA HATA SERIKALI YENYEWE INAPINGANA KIMAAMUZI. MFANO WA HIVI KARIBUNI NI LILE SUALA LA NDG DAVID JAIRO. WATANZANIA TUMEONA NAMAN SERIKALI YETU ILIVYOSINZIA KIASI KWAMBA KILA KIONGOZI ANAKUJA NA MAAMUZI YAKE AMBAYO NAWEZA KUSEMA NI MAWAZO BIANFSI YA MTU HUSIKA KWA MASLAHI YAKE..
Kwa hiyo mkuu waTanzania watajimobilize lini (ambayo ni kazi kubwa sababu wengi wetu wapo usingizini); na hata kama tutafanya maandamano mpaka miguu ikaingia tumboni kwa kutembea ni kweli tutaleta mabadiliko...????
Kumbuka serikali ina-spin hayo maandamano kwamba ni fujo na hata hao wapinzani wakiingia madarakani hali itakuwa mbaya zaidi ( na watu wanaamini..).., sasa je mkuu huoni kwamba ni vema kuwa na plan nyingine (njia nyingine ya kuonyesha watu kwamba wapinzani ndio wanaweza kuleta mabadiliko..?)
Ndio maana mkuu nikauliza mmoja wa wapinzani Ndg Mnyika kwamba... Tunajua Plan A ya Serikali imeshindikana..., na Plan B ya kuandama ikishindikana ni nini kifuate..?? ni nini Plan C...???....., na mkuu kumbuka (there is more than one way to skin a cat)... na wapinzani wanaweza kufanya mambo ambayo hayawezi yakawa misqouted na mtu yeyote..... Hivi upinzani ukianzisha mradi wa biogas huko kijijini na kuweza kuwaletea wanakijiji energy ya kutosha ya kupikia hicho kijiji kweli kitawasahau come 2015..... na gharama ya kutengeneza hii sio zaidi ya mifuko kadhaa ya cement.., pesa ambayo hata wakiamua wabunge wanne tu hawashindwi...