Mheshimiwa Engineer Samawati Mbunge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Engineer Samawati Mbunge!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Jul 14, 2011.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  TBC hapa kuna Waziri anatumia muda mrefu kweli kwenye majumuisho ya Wizara yake...
  anataja waheshimiwa kibao waliochangia kwenye majadiliano, kwa majina...na kumalizia..Mheshimiwa ....."mbunge".Hii imefanya atumie muda mrefu sana wakati sisi wananchi tunachotaka ni kusikia hoja na siyo majina.

  Najiulizayafuatayo:
  1. Kuna ulazima gani kuwataja majina na ubunge wao?
  2. Je mtu asiye mbunge angeweza kuchangia?
  3. Nini mantiki ya orodha hiyo badala ya kujibu hoja?

  Tuelimisheni wajuaji wa mambo.

  ******Niwie radhi bibie Samawati.... nakutakia kila la kher!
   
 2. m

  mapinno Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  huu ni utaratibu kuendana na kanuni za bunge, mabadiliko ya kanuni ndo yanaweza leta sura tofauti
   
 3. Samawati

  Samawati Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 13
  Dada Wos asante kunipandisha cheo. Itabidi nikazane sana nisikuangushe 2015
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kumbe kuna mtu kaona hiki kioja. Imekuwa ni desturi kwa mtoa hoja - yaani bajeti (i.e Waziri) wakati wa mahitimisho wa hoja yake anawatajwa wabunge wote waliochangia. Kitu ambacho najiuliza kuna umuhimu gani kuwataja kwa majina wachigiaji? hii time wasting ilitokana na nini hasa? Bado naweza kusema bunge na hata serikali inaendeshwa kwa mazoea, hakuna idea mpya kabisa.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi huu mtindo wa kumtambulisha ama kumuita mtu kwa kutumia fani yake mbele ya jina lake umeanza lini? Manake siku hizi mtu ukiwa mhandisi basi utaitwa 'mhandisi' flani wa flani...ukiwa mhasibu utaitwa 'mhasibu' flani wa flani.

  Labda mimi kumbukumbu yangu ni ndogo lakini hapo zamani wahandisi, wahasibu, n.k. hawakuitwa kwa fani zao. Ila sasa naona huu utaratibu umeshika kasi sana. Sijui kwa nini tu?
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kichekesho ni pale wanapesema....fulani fulani - "mbunge'.
  Hivi kuna anahudhuria au kutoa mchango kama sio mbunge! vilaza!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ninavyofikiri mimi ( naweza nisiwe sahihi), enzi za mwalimu, wanasiasa walikuwa wanasiasa na wenye fani zao walikuwa kwenye fani. Ni miaka ya sasa tu tunaona wenye fani wakipigana vikumbo majimboni kugombea ubunge! Na pia ni miaka ya sasa tunaona kila mwanasiasa akihangaika sana kupata shahada ya Uzamivu (PHD) na kufanya PHD iwe kama cheti cha darasa la 12!

  Huenda kuna sababu pia ya kujaribu kujitofautisha na wale wasiokuwa na shahada au "professions adimu"!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Nchi yetu ni kama maigizo hivi....
  Watu wa rekodi za guiness wakija hapa
  watafaidi...
  Kuna mambo tunayafanya.....made only in tanzania.....
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sababu yeyote ile lazima pia tufanane na dunia inavyokwenda......

  Wewe umewahi sikia
  mheshimiwa professa condoleeza rice....

  Sisi ndo wasomi saaana wa dunia au?????????
   
 10. T

  The Priest JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huyu waziri amekaa kweli hapa nchini?,hajui hata kutaja majina ya wabunge na hata mawaziri wenzake!
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hmm..okay!

  Kwenye nchi za wenzetu ambazo zimekomaa kisiasa na kidemokrasia, kwenye mabunge yao wabunge huwa hawajitambulishi kwa fani zao. Mfano bunge la Marekani (chemba zote mbili) limesheheni wasomi wa ukweli lakini hata siku moja sijawahi kumuona Newt Gingrich akijitambulisha kama Dr. (wa PhD) Newt Gingrich, Speaker, US House of Representatives au Dr. (surgeon) Bill Frist, Senate Majority Leader, au sijui Advocate Barack Obama, US Senator, Illinois....

  Sisi tunapenda sana ujiko wa kwenye makaratasi kuonyesha tumesoma. Hovyo kabisa....
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Au umewahi kusikia Advocate Bill Clinton au George W. Bush, MBA? Yaani sisi bana....eti advocate so and so au engineer so and so....hahahahaaa who cares about what they went to school for? Sana sana wanajiaibisha tu kwa sababu hakuna la maana hata walifanyalo huko bungeni achilia mbali majimboni mwao.
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Boss,
  Kama kuna kitu kinanifanya nione aibu mbele ya wenzetu ughaibuni ni hulka yetu watanzania (hata wanaijeria ) kupenda kujitukuza kwa "credentials' .Haishangazi kuona kila mtu akitaka kuitwa Dr tena kwa muda mfupi sana - miaka 2 !

  Siyo siri PHDs siku hizi ni kitu cha kawaida na wengi wanazo tena wanazipata wakiwa na umri mdogo in their 30s na huwezi kuona mtu anajitutumua kujulikana ni Dr X,Y,Z! Na hata hawapendi kuitwa Dr.... kama ni doctoral degree..na wanapenda kujiita kwenye maandishi zaidi -mfano: The Boss..( Phd)!

  Inabidia tuanze kampeni kupunguza matumizi mabaya ya "Dr".Wajiite madaktari wa binadamu tu ili tuwatambue kwa urahisi tunapotaka huduma!
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  WOS..
  I am sure ukisafiri umewahi pia kukuta kwa mfano mtu
  ni ceo lakini hata kwenye bussiness cars yake unakuta jina tu na adress ya kampuni..

  sasa ukija sisi....

  unakuta ceo.director general,dr,shaaban malinyingi,.mjumbe wa nec ccm....

  yaani aibu zingine bana....
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  tutaanza kuonekana matapeli kama wa nigeria hata kama sio
  kwa upuuzi kama huu...
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Jul 14, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hii kampeni isianze na kuishia kwenye u-Dr. tu. Hata wahandisi, wahasibu, mawakili, na wengineo manake huko tunakokwenda sasa hata hakueleweki. Sitashangaa siku moja Michuzi naye akaanza kujitambulisha kama 'Photojournalist Issa Michuzi'.....au Kibonde kuanza kujiita 'Presenter Ephraim Kibonde'.

  Mtu ni raisi wa nchi lakini bado unaitwa Dr. tena udokta wenyewe wa kupewa mezani. Sielewi kabisa mimi.
   
 17. n

  ngarauo Member

  #17
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mgamba plus
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  NN,
  Unatangaza vita?....mwendo mdogo mdogo kwanza lol
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mkuu..
  mimi nimekutana kabisa na mtu
  ambae bussiness card yake amejaza title tele
  na title ya mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm....
  tunapoelekea ni kuwa watu wataanza kuitwa
  mheshimiwa mmiliki wa gazeti la ijumaa,john shigongo
  mheshimiwa mmiliki a coud media joseph kusaga...

  na wengine itakuwa mheshimiwa diwani na mmilikiwa bar ya batotoz john robert...
  very upuuzi
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Comedian Dr Boss..acha kunichekesha hahahahah
   
Loading...