luhilaseko
Member
- Jul 1, 2017
- 24
- 65
Wana familia wa JF, Amani iwe kwenu
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi ni Mhenga mwenye umri wa miaka 36. Nimerudi nchini wiki mbili zilizopita baada ya kumaliza masomo yangu ya Shahada ya Uzamivu (PhD in Media Studies) katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Na degree yangu ya kwanza ya Mass Communication niliisoma hapohapo makerere University wakati degree ya pili (Masters) niliisoma hapa Tanzania.
Wakati nikisubiria Graduation itakayofanyika mwezi February 2018, na kwa kuwa wahenga wenzangu waliwahi kunena kwamba MFICHA UCHI HAZAI na wengine wakanena kwamba BIASHARA MATANGAZO basi nami naja mbele yenu kujinadi kwamba natafuta kazi katika field husika. Uzoefu na uelewa wa field hiyo ninao mkubwa sana.
Ijapokuwa lengo langu kubwa ni kuja kujiajiri mimi mwenyewe hapo baadaye kidogo, kwa sasa nimeona ni vema nitafute sehemu ya kuajiriwa wakati nasuka mipango ya kuja kujiajiri hapo baadaye.
Hivyo wakati nikikimbizana na bahasha kutafuta ajira, nakuja kwenu kuomba kwa yeyote mwenye connection ya ajira asisite kunijulisha kwa namba 0714 159 283. Nipo tayari kufanya kazi sehemu yoyote na katika mazingira yoyote maana mimi ni mpambanaji.
ANGALIZO ni kwamba PhD yangu isikutishe ukadhani kwamba nitahitaji mshahara mkubwa HAPANA. Nipo tayari kufanya kazi kwa mshahara wa kawaida tu maana toka nimerudi nchini nimekuwa iddle kiasi kwamba natamani heri ningerudi chuoni
Natanguliza shukrani