Mhe.Tundu Lissu ndani ITV

Nakumbuka kijana Albert Msando alivyomtoa nduki Lissu kwenye matumizi ya kugha ya kiingereza wakati wa kesi ya Zitto mpaka Lissu akaomba poo kwa kuomba mahakama itengue matumizi ya lugha ya kiingereza na kutumia kiswahili
 
Nakumbuka kijana Albert Msando alivyomtoa nduki Lissu kwenye matumizi ya kugha ya kiingereza wakati wa kesi ya Zitto mpaka Lissu akaomba poo kwa kuomba mahakama itengue matumizi ya lugha ya kiingereza na kutumia kiswahili

Lissu anafikiri kujua sheria ndiyo kujua kiingereza nini?
 

Ulichotaka kutuambia hapa ni kuwa ulikuwa nje ya nchi na si vinginevyo. Tumekupata na hongera kwenda nje ya nchi.
 

Bunge hutumia lugha ya kiswahili kufikisha ujumbe kwa wananchi.

Ni muhimu kumkumbusha Tundu Lisu kuwa hatutumii kisukuma, kindengeleko, kijerumeni wala kiingereza kwenye bunge wala kwenye kampeni za kugombea Ubunge. Na wala si sherti kuwa mbunge LAZIMA AJUE KIINGEREZA kwani wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui kiingereza.

Ushauri wangu kwa T. Lisu: Kama umeshindwa kufanikisha AJENDA KUU YA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI NI BORA UJIUZULU UBUNGE. HATA SIKU MOJA SITOCHAGUA MBUNGE KWA KIGEZO CHA KIINGEREZA BALI KWA UADILIFU, KUJALI WANANCHI, KUWA MBUNIFU WA UTATUZI WA MATATIZO YA WANANCHI NA KUWA SEHEMU YA WANANCHI.
 
Ulichotaka kutuambia hapa ni kuwa ulikuwa nje ya nchi na si vinginevyo. Tumekupata na hongera kwenda nje ya nchi.

Thatha kwi kwi kwi hapana kiongozi, suala sio kwenda nje ya nchi, la hasha. Nilichokuwa nawekea mkazo ni jinsi watanzania tunavyoaibika kwenye viwanja vya kimataifa kwa kukosa umahiri juu ya lugha ya ki-ingereza. Ni hilo tu mkuu, ni hilo tu.
 

wangekuwa mabubu hapo ningeona kuna tatizo lkn kama wanajua kuongea kiswahili safi sana mana kiingereza si lugha ya taifa ili
 
Lissu anataka sifa baada ya kuona Zitto amekaa kimya kwa mda mrefu anatafuta hoja za kutaka ajulikane na wa TZ.
Kama kingereza ndo tatizo kuu ya wabunge kutokuwajibika basi Mbowe ahombe kura kwa kingereza na Lissu arudi mahakamani kutetea kesi dhidi ya Zitto mbele Albert Mzande kwa kingereza.
 
Sugu, lema, mbowe, mdee, hebu waanze mijadala rasmi kwa lugha hiyo 2one!
 

Kuna njia nyingi za ufumbuzi wa tatizo hilo. La karibu sana ni kuwa na MKALIMANI ambalo hutumika katika nchi nyingi. Ni aibu kumchagua mtu kuwakilisha watanzania eti kwa vile ni mzuri kwa KIINGEREZA na (si kwa uzuri wa kujua mada husika) wakati watanzania milioni 40 wanazungumza kiswahili. NAFIKIRI WAKATI UMEFIKA SASA WA KUZUNGUMZA LUGHA YETU YA KISWAHILI KATIKA MIKUTANO YA KIMATAIFA HUKU WAKALIMANI WAKIFANYA KAZI YAO. Tuna malinguist wengi tu sasa hivi.

Watoa hoja huliangalia hili swala kwa rangi mbili tu "BLACK and WHITE". Ongezeni rangi mtapata majibu mazuri yenye ufumbuzi mwafaka.
 

Nakubaliana na wewe kamanda. Ila tatizo ni kuwa hata hiki Ki-Swahili wengi wetu hatukijui vizuri. Ki-Swahili fasaha sio mchezo. Watanzania ki-ingereza hatukijui na ki-swahili fasaha nacho hatukijui, majanga.
 

Kamaliza vita na ZITTO, sasa anamuingilia MWENYEKITI WAKE MBOWE. Pengine hata na LEMA na wengine kibao.

Pazuri hapooooooooooooooooooo! Yangu macho.
 

Hivi umeelewa Lissu alichokuwa akisema? Au umekurupuka. Lissu anahimiza matumizi ya lugha ya kiswahili bungeni. Anashangaa bunge linatunga sheria zinaandikwa kwa kiingereza wakati hata spika wa bunge bi Kiroboto hajui lugha hiyo.
 
Kamaliza vita na ZITTO, sasa anamuingilia MWENYEKITI WAKE MBOWE. Pengine hata na LEMA na wengine kibao.

Pazuri hapooooooooooooooooooo! Yangu macho.

Ukweli huwa haubagui. Km mwenyekiti wake hajui kiingereza huo utabaki kuwa ndio ukweli.
Hoja ya Lissu iko kwenye uelewa na uchangiaji. Labda niwaulize wote wanaopiga vijemba; Je, kuna ushahidi kuwa Mbowe ameshindwa kuchangia hoja kwa ufasaha wakati wowote?
 
utaifakwanza unapotosha; alichosema ni kuwa miswada ya sheria huandikwa kwa Kiingereza hivyo wabunge huishia kupiga makofi kwa maana hawajui kiingereza. Na alisema kuna watu wenye elimu na vyeo vikubwa lakini hawajui kiingereza alichoshauri ni kuwa miswada ya sheria iandikwe kwa kiswali ambacho kinazungumzwa na kila mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…