Kipapatiro
JF-Expert Member
- May 18, 2017
- 1,129
- 1,497
Mkuu naomba elimu, tattoo INA madhara gani jeshini?Alimaliza kozi ya jkt (jeshi la kujenga taifa) baadae ajira zilipokuja akajiunga na jwtz akafaulu kwenye usaili, nakumbuka wakati tupo kwenye kozi kipindi cha kubadilisha roho ya raia na kuingiza roho ya kijeshi (six week) nakumbuka tulikuwa kwenye mchakamchaka tupo hoi porini tukapewa tano (mapumziko ya muda mfupi) pembeni kuna bwawa la maji tukawa tunaoga bahati mbaya ndugu Amani Temba alijisahau akavua kombat ya juu mkufunzi akaiona ile tattoo yake akaitwa, basi tangu siku ile hatukumuona tena kikosini mpaka nakuja kusikia jamaa yupo uraiani kawa msanii. Ila jamaa aliwahuzunisha watu wengi sana kutokana na ucheshi wake, baadhi ya maofisa pia walihuzunika maana kuingia kwake jkt mpaka jwtz ulikuwa mpango ili baadae aje kuwa mchezaji wa kikapu kwenye timu ya jeshi ndio maana hata uingiaji wake ulikuwa ni hamasa kutoka kwa walimu wa michezo (wanajeshi) pale jitegemee sekondari.