Mhe. Spika, umeshaipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Wabunge 8 wa CUF?

Hawa wapya ni 'uteuzi kutoka juu' Spika naye ni mteule..Nasfasi ya spika aliweza Sita na amekufa na karama yake!
Napenda kukufahamisha kuwa nafasi ya Uspika si ya kuteuliwa, ila ni ya kugombea kasome katiba itakupa maelezo yote ni nafasi zipi za utezi na zipi za kugombea.
 
Unapoandika ni lazima ufikirie kwa kutumia kichwa na si kutumia mgongo, wale wabunge waliapishwa baada ya yeye spika kuletewa majina kutoka mamlaka nyingine zinazohusika na wabunge wa vyama. Hivyo spika hana kosa lolote alilofanya kwani yeye alitimoza wajibu wake kama spika, acheni ushabika usiokuwa na maana.
Alipelekewa majina yeye akiwa nje ya nchi kufika tu akawaapisha,
 
Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
So far speaker ameamuaje hasa kuhusu wabunge wapya alioapisha?
 
Napenda kukufahamisha kuwa nafasi ya Uspika si ya kuteuliwa, ila ni ya kugombea kasome katiba itakupa maelezo yote ni nafasi zipi za utezi na zipi za kugombea.
Katiba ya mbinguni? Spika ametokana na chama cha mapinduzi,Spika ni mwanachama wa chama cha mapinduzi ambaye mwenyekiti wake unamjua,kwa influence ya mwenyekiti anampendekeza kisha anapigiwa kura na lazima azipate kwa wingi wa ndiyooooo unategemea huyo spika atakuwa na meno? Hiyo katiba inatumika kuapishia tu wateule basi!
 
Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
Kisheria huo uamuzi wa mahakama Ni redundant. Huwezi kutoa maamuzi ya ku maintain status quo wakati hiyo status quo imeshabadilika. Mombi hayo tayari yalikuwa yameshapita Na matukio. Uamuzi huo unawafaa nyie academicians kwa kuwafundisha watoto
 
Uamuzi wa Mahakama hauwezi kuwa redundant Mkuu.
 
Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
Kwa ufahamu wangu kumaintain status quo ni kama ulikuwa namba mbili hutakiwi kwenda tatu au kurudi moja unabaki kwenye mbili mpaka itakavyoamuliwa vinginevyo hivyo basi waliovuliwa uanachama wanabaki kama walivyo na walioapishwa wanabaki kama walivyo hivyo basi hiyo amri haina impact yeyote kwa walioapishwa
 
Ushauri wangu;
Warudi bungeni na wale waliopewa ujiko kwa upendo wa spika, waondoke tu. Nadhani spika atajifunza kitu hapa na kujua kuwa, hakutenda sawa huwapokea na kuwaapisha haraka hivyo.
Kama ni uwakilishi, walikuwepo tiyari alio wafurumua nje ya ulingo. Pia kulikuwa na kila hali iliyoonesha kuwa, Haki haikutendeka lakini kwa sababu alizozijua yeye, akawafurumua hata kabla ya barua ya cuf.
Swali; Je, Kwa kuwa waliapishwa kikatiba na kisheria, na kwa kiapo hicho kuwa wabunge halali, na kuhudhuria vikao halali vya bunge; Je! hao wanaoondolewa sasa, watapewa haki zao stahiki watakapo ondoka?? Wesha jivutia mishahara kadhaa, ambapo hawa wa mahakama wakirudi mle, itabidi nao walipwe mishahara na posho walizozuiwa kuhudhuria kwani sio kosa lao. Ni nani atalipa hasara hii??
Si ajabu na magari walishavuta. Ni nani atawalipia?? Nawaza sana
 
Back
Top Bottom