Mhe. Spika, umeshaipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Wabunge 8 wa CUF?

Mkuu, yaani umeshindwa kuelewa kabisa kuwa hilo suala ni la kisheria? Huwa nasikitika sana kuona vyama vya siasa vinawatia ukungu kwenye bongo zetu.

Vv
Najua la Kisheria. Wewe una maslahi gani nalo? Mpaka unapoteza muda wako kulifuatilia badala ya kutafuta mkate wako wa siku?
 
Najua la Kisheria. Wewe una maslahi gani nalo? Mpaka unapoteza muda wako kulifuatilia badala ya kutafuta mkate wako wa siku?
Mkuu, kila raia ni mdau wa sheria, sheria inatakiwa kufuatwa na kutiiwa na wote isipokuwa wale wanaothibitishwa kuwa ni vichaa.
Vv
 
Hii mada again inadhihirisha ni jinsi gani hii so called mihimili ya utawala bora inavyofanya kazi kiwajibu wa kisheria,Tanzania sio siri ni mhimili mmoja ambao uko very powerfull to override maamuzi kutoka mihimili mingine bila hata ya kuangalia sharia zinasemaje;

Our no 1 ana uwezo wa kulivunja BUNGE hata kwa vitu kama bunge kukataa kupitisha mswada wa serikali!,tumeshuhudia watu wakivunjiwa nyumba zao wakati kesi zao zipo mahakamani(elewa mahakama ndio kimbilio la yeyote katika kutafuta haki au kutafisiliwa sheria inasemaje,

Ni chombo ambacho hata serikali inabidi kwenda inapokinzana na sharia au kupata tafsiri yake) na hii yote inadhihirisha jinsi nchi inavyoendeshwa bila kufuata sheria,tumeshuhudia tenda zikitolewa hadharani,mwombaji anajitokeza na kuomba na muda huo huo anapewa tenda hiyo,but si kuna kamati ya tenda ya wilaya?

Why agizo lingetolewa kwa watu wenye uwezo kuomba hiyo tenda ya kuuza sukari kwenye tender board then utaratibu ukafuatwa?maana hapa kukijitokeza mtu akalalamika mahakamani kuhusiana na hii tenda ,aliyeipata hiyo tenda hana documents halali za kuomba tenda hiyo ,tunaishi in a very trying time ila always TIME ni tiba nzuri,whats happening now in Zimbabwe ni matokeo ya muda kuchukua nafasi yake.
 
Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
Anangojea maelekezo toka kW JPM.
 
Walipwe tu stahiki zao zote kama Wabunge halali wa Jamhuri mpaka pale shauri la msingi likiamriwa. Tumeshazoea kulipa Wakurugenzi wapya na wale waliotumbuliwa wakisubiri "kupangiwa kazi mpya"
 
Back
Top Bottom