Mhe. Spika, umeshaipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Wabunge 8 wa CUF?


Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,292
Likes
13,294
Points
280
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,292 13,294 280
Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
 
Skywalker3

Skywalker3

Senior Member
Joined
Nov 22, 2016
Messages
154
Likes
175
Points
60
Age
28
Skywalker3

Skywalker3

Senior Member
Joined Nov 22, 2016
154 175 60
Ya ngoswe mwachie ngoswe
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,292
Likes
13,294
Points
280
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,292 13,294 280
Sasa hawa wapya nao watatenguliwa?
Ñao wakienda kwa Court ili kumaintain hiyo status quo itakuaje?
Vijana hiyo huiita 'weka niweke'. Busara ilikuwa kusubiri Uamuzi wa Mahakama wakati ule.
 
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
8,929
Likes
13,699
Points
280
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
8,929 13,699 280
Ñao wakienda kwa Court ili kumaintain hiyo status quo itakuaje?
Wao hawana sifa ya kwenda mahakamani ingawa wana haki ya kufanya hivyo. "Status quo" anayoingolea Petro ni uanachama na hao nane waliopishwa kama wanakwenda kuzima moto hawatavuliwa unachama.
 
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2017
Messages
2,527
Likes
2,417
Points
280
Che mittoga

Che mittoga

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2017
2,527 2,417 280
Petro E. Mselewa hili jambo limeshakuwa gumu Kikatiba na kisheria. Kama ulivyosema haraka ya kuwaapisha wale nane wengine ilitokana na nini?
Kumwunga mkono Profesa Lipumba.
Natoa Pole kwa usumbufu mkubwa aliopata Mwalimu wangu mpendwa Shahari Mngwali.
Mmoja wa wabunge walioathirika na maamuzi ya ajabu ya Lipumba.
 
Gangongine

Gangongine

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Messages
3,864
Likes
1,749
Points
280
Age
48
Gangongine

Gangongine

JF-Expert Member
Joined Dec 31, 2015
3,864 1,749 280
Wewe inakuhusu nini? Una wadhifa gani huko CUF.
 
ZENJIBARIA

ZENJIBARIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Messages
538
Likes
907
Points
180
ZENJIBARIA

ZENJIBARIA

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2014
538 907 180
pengine hajafahamu maana ya zuio,manake na hizo mahkama zetu nazo zinatoa matamshi yasiyowekwa wazi, zuio hapa lina maana kua "kilichozuiwa kiendelee kuwa na hadhi na hali yake iliyokuwa kabla bila ya kuathirika" kwa kauli ya mahkama wabunge wale 8 bado ni wabunge rasmi mpaka uamuzi tafauti utakapotolewa.

kwa walivyo hawa wanaweza kujifanya kesi tu ndo ilozuiwa
 
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,255
Likes
11,692
Points
280
Consigliere

Consigliere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,255 11,692 280
Yule mb aliempiga mtu rungu akili zke huwa haziko sawa,huwa anafanya vitu ili mkuu wke aridhike kiroho.kageuza bunge kua la hovyohovyo kuwahi kutokea
Hivi alimpiga mtu rungu au alijipiga rungu? Maana akili zake tunavyoziona kupitia maamuzi yake ni kama vile alijipiga rungu.
 
VAPS

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
1,733
Likes
2,852
Points
280
Age
32
VAPS

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
1,733 2,852 280
Wakubwa hawakosei bali wanasahau,taasisi ya bunge ilipaswa tumia busara subiri maamuzi mahakama.
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,292
Likes
13,294
Points
280
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,292 13,294 280
Mkuu Gangongine, una lengo la kuuharibu huu uzi au? Maana tangu uanze kuchangia umekuja na matusi, kejeli na dharau. Hebu kuwa mstaarabu. Kama unahitaji kuandika unayoyaandika, tafuta mahali pengine. Si hapa.
 
tweenty4seven

tweenty4seven

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2013
Messages
8,201
Likes
6,161
Points
280
tweenty4seven

tweenty4seven

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2013
8,201 6,161 280
Hivi alimpiga mtu rungu au alijipiga rungu? Maana akili zake tunavyoziona kupitia maamuzi yake ni kama vile alijipiga rungu.
Alimpiga rungu bdae alivyoapishwa akawahi india kujazia cd4 mana hali ilikua si hali
 
M

Mdakeo

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2017
Messages
556
Likes
680
Points
180
Age
43
M

Mdakeo

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2017
556 680 180
Hasara ya Kukurupuka!

Mnaona sasa mnapoipeleka nchi kwa maamuzi yenu.
 
M

MzalendoGANI

Member
Joined
Nov 6, 2017
Messages
17
Likes
1
Points
5
M

MzalendoGANI

Member
Joined Nov 6, 2017
17 1 5
Hapo hakuna kupepesa macho wabunge wa Lipummba waachie ngazi mara moja
 
V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Messages
4,143
Likes
2,561
Points
280
V

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2014
4,143 2,561 280
Wewe inakuhusu nini? Una wadhifa gani huko CUF. Tafuta riziki yako acha umbeya. Ada za watoto zinakushinda!
Mkuu, yaani umeshindwa kuelewa kabisa kuwa hilo suala ni la kisheria? Huwa nasikitika sana kuona vyama vya siasa vinawatia ukungu kwenye bongo zetu.

Vv
 

Forum statistics

Threads 1,236,877
Members 475,318
Posts 29,270,623