Mhe. Spika, umeshaipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Wabunge 8 wa CUF?

Petro E. Mselewa hili jambo limeshakuwa gumu Kikatiba na kisheria. Kama ulivyosema haraka ya kuwaapisha wale nane wengine ilitokana na nini?
Haraka ya kuwateua na kuwaapisha wale wengine ulikuwa mpango maalum wa kumkomoa Seif na Ukawa, na kuiongezea nguvu CCM bungeni kupitia "wabunge hao wa Lipumba" ili "ndiyooo" ziwe nyingi zaidi!
 
du hapo mm sio mtaalamu wa sheria
naamin spika hajaipata ;
na wale si walisha vuta na mpunga nasikia wana v8 itapidi ofisi ya spika ilipe
 
Petro,

Tangu limeanza hili jambo nimekushangaa kitu kimoja ingaw ani haki yako. Ninachokushangaa ni kwamba suala zima unaliweka kama vile ni swali kwa sisi tusio wanasheria wakati sisi ndiyo tulitakiwa tuulize na nyinyi wanasheria muwe watu wa kutoa majibu.

Hata kama majibu yako yangezusha ubishi humu mtandaoni hicho ni kitu kidogo sana na cha kawaida maana kubishana ndiyo unanasheria wenyewe na mahamakamni ndipo mahala mnapoonyesha ugwiji wa kubishana.

Mimi si mwanasheria lakini nimeshashiriki kesi kadhaa za kushitaki na kushitakiwa na majibu yangu kwa hili yako hivi.

Mzozo haukuwa kati ya mahakama na Bunge. Mzozo ni wanachama waliovuana uanachama hivyo hapo Spika hahusiki kabisa.

Mahakama imehesabu kwamba uanachama wao umeendelea hadi suala litakapokuwa determined by the court. Hapo mahakama haihitaji kujua Spika alifanya nini au msajili alifanya nini.

Kinachotakiwa ni kwamba kama umerudishiwa uanachama wako (albeit temporarily) ni kazi yako wewe kuzunguka kote ambao uliathirika na kuvuliwa uanachama wako.

Kama ni bungeni, wewe ulipaswa kuandika barua na ukahakikisha (proof off service) kwamba imemfikia Spika, ama kwa dispatch, ama kwa deliver note ya Courier kama DHL, EMS, Post Register au fax tramsimtal report.

Hivyo, kama wale waliofukuzwa hawajafanya hivyo, siyo kazi ya Jaji kupeleka hilo ofisini kwa spika, kama ambavyo si kaiz ya Jaji kuwarudishia uanachama kwa kusikia tu redioni au kwenye TV.

Kama hawa waliofukuzwa hwajamfikishia Spika ile Judgement basi huu pia ni uzembe mwingine wa CUF na tunapaswa tusiwape sympathy.

Pia hataka kama wamemfikishia Spika naamini Spika atakuw akatika hali ngumu lakini anaweza kukataa kw aibu. Hii si tatizo kwani hawa wabunge walitakiwa kuwa wamemaliz hayo yote na sasa hivi wangeshakuwa wamefungua kesi ya pili kumshitaki Spika kutowarudisha bungeni.

CUF wanacheza itakula kwao kama walivyozembea kumtimua Lipumba inawaletea matatizo. Sijui wanasheria kama Jussa wanafana nini huko.

Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
 
Hiyo nakala ingekuwa inatoka kwa Lipumba siku hiyo hiyo ingekuwa imeshajibiwa na Ofisi ya Supuka wa nyumba za tembe.
 
Hongera Petro! Leo andiko lako liko professional; halina bias!
 
Habari hii siyo nzuri kwao lazima waipotezee,,,
 
ule uamuzi wa Spika ulishangaza sana. Alitolea maelezo na maamuzi akiwa nje ya nchi as if ni dharura
 
Mutungi na Ndugai watafungwa muda si mrefu , hata Mugabe alikuwa na kiburi kama hivi .
 
Hizi ndiyo busara na hekima zako ambazo zilikupa heshima nyingi na kwa wengi humu na kwa kipindi kirefu Mkuu.

Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
 
Hawa wapya ni 'uteuzi kutoka juu' Spika naye ni mteule..Nasfasi ya spika aliweza Sita na amekufa na karama yake!
 
Yule mb aliempiga mtu rungu akili zke huwa haziko sawa,huwa anafanya vitu ili mkuu wke aridhike kiroho.kageuza bunge kua la hovyohovyo kuwahi kutokea
Unapoandika ni lazima ufikirie kwa kutumia kichwa na si kutumia mgongo, wale wabunge waliapishwa baada ya yeye spika kuletewa majina kutoka mamlaka nyingine zinazohusika na wabunge wa vyama. Hivyo spika hana kosa lolote alilofanya kwani yeye alitimoza wajibu wake kama spika, acheni ushabika usiokuwa na maana.
 
Hujui kitu wewe mgogo , tulia .
 
Back
Top Bottom