Humphrey Polepole
Member
- Nov 15, 2010
- 19
- 230
Kwa heshima kubwa nauliza, kwanini mnataka kukimbiza mambo? kuna lipi tusilolijua mnalotaka kulitimiza? Mnajua muda hautoshi, kwanini mnalazimisha kila kitu kifanyike kabla ya tarehe 4 Oktoba. Ilhali mnajua tumeshindwa kukubaliana, kujenga muafaka na kufanya maridhiano, Dhambi iko wapi, si tuache wenye busara zaidi yetu waendelee na mchakato 2016. Au unahofu Bunge la 2016 halitakuwa na busara kama yetu na kwamba wao watashindwa kujenga muafaka wa kitaifa, kufanya maridhiano na kuwa na uelewa wa pamoja wa misingi.?
Wengi wenu mnajua hata Rasimu Toleo la Pili hamkuisoma vizuri na wengine hamkuielewa mpaka leo na mmekuwa nayo kwa miezi kadhaa, je Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa iliyotoka kwa Kamati ya Uandishi tarehe 24 Mtakuwa mmeweza kuisoma, kuielewa na kuweza kuifanyia maamuzi kabla ya tarehe 4 Oktoba?
Je Muhimu kwenu ni kupiga kura ili kazi iende au ni kuwa na uelewa, ufahamu na uhakika wa kwamba mnachokifanyia maamuzi ndicho kitatuvusha kutoka sasa hadi miaka zaidi ya 50 ijayo? Je mmejipa muda, siku 10 zinawatosha, please lets be serious to our country Tanzania, Please Please, For once tuahirishe tuendelee 2016.
Nina uhakika Historia itatukumbuka, kila mmoja mmoja wetu kwa kazi aliyofanya kwa Taifa letu leo.