Mhe. Rais, Watanzania Tunakuunga Mkono, Yataje Magazeti Chochezi,Tutayasusia Yajifie Natural Death!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,770
121,823
Wanabodi,
Kwa mujibu wa katiba yetu, Uchochezi ni kosa la jinai, hivyo chombo chochote cha habari kinacholeta uchochezi wowote hakihitaji kuonewa huruma yoyote bali kifungiliwe mbali mara moja.

Mhe rais wetu ametoa onyo kwa magazeti mawili ama yaache uchochezi, ama atayaadhibu kwa kuyafungia bila huruma!.

Naamini Watanzania wote wenye kulitakia mema taifa letu, wataungana na rais wetu kuyalaani haya magazeti mawili chochezi kwa kutaka yachukuliwe hatua kali za kisheria kwa kufungwa toka jana.

Kwa vile Tanzania ni sehemu ya global Village, inawezekana kabisa huo unaoitwa uchochezi ni uchochezi kwa kijiji kimoja na freedom of expression kwa kijiji kingine.

Mfano gazeti likiibua kashfa fulani kubwa kutokana na data kwenye confidential document, gazeti likichapisha habari hiyo, litakuwa limefanya kosa la kuchapisha siri za serikali hivyo inabidi lifungiwe! .

Lakini kwenye "open government initiatives" media inayoibua madudu ya serikali ndio yenye kupaswa kupongezwa kwa sababu japo kweli ni siri lakini ndio ukweli wenyewe.

Ila katika kumuunga mkono rais wetu, na wakati huo kuilinda nchi yetu tusitengwe na jumuiya ya kimataifa, jee mnaonaje kama turamshauri rais wetu, ayataje tuu hayo magazeti, halafu sisi Watanzania wote katika umoja wetu, tukayasusia kabisa kuyanunua, hivyo badala ya kuyafunga na kusababisha kelele nyingi, yatadodea kwenye meza za magazeti na kujifia natural death! .

Mnaliona hili? .

Paskali
 
Kwa mtu mwenye upeo mkubwa atafahamu majina ya magazeti yaliyopewa salamu za mwaka mpya.

Ninafahamu unajua majina ya hayo magazeti lakini unataka kuanzisha mjadala tu wenye mwelekeo mwingine kwa faida uzijuazo.

Chunguza hii sentesi ya Rais kama una fikra pana na utajua majina ya magazeti.

''Hatuwezi tukaiacha Tanzania ikawa dump la eneo la kuweka maneno ya uchochezi'', Alisema Rais.

Ninaamini kama Rais angetaja majina ungekuja hapa na thread nyingine ya kupinga.

Kumbuka pia kuna utaratibu na sheria ya kupata habari za siri za serikali. Kwa mfano Waziri ataenda gerezani hata kama akitoa siri za baraza la Mawaziri lilikuwa linajadili jinsi ya kufanya ufisadi nchini.

Freedom of expression ina mipaka yake katika nchi yoyote. Hoja ya msingi ni mipaka ipi katika kila nchi na kwa nini kuna hiyo mipaka.

Watu wenye hekima na busara wanasema ni vizuri kupambana na sheria badala ya kupambana na anayesimamia sheria.
 
Concept tu ya Rais ni nani hapa ndo shida...

Je Rais ni kama 'mfalme' ambae kila mtu na kila kitu ni mali yake?

na kwa utashi wake anaweza kuamua lolote tu?

Au Rais ni mtumishi wa wananchi na hao wananchi wako huru kuuliza chochote?

Magazeti mawili,Jamiiforums.....who is next?
 
Kwa mtu mwenye upeo mkubwa atafahamu majina ya magazeti yaliyopewa salamu za mwaka mpya.

Ninafahamu unajua majina ya hayo magazeti lakini unataka kuanzisha mjadala tu wenye mwelekeo mwingine kwa faida uzijuazo.

Chunguza hii sentesi ya Rais kama una fikra pana na utajua majina ya magazeti.

''Hatuwezi tukaiacha Tanzania ikawa dump la eneo la kuweka maneno ya uchochezi'', Alisema Rais.

Ninaamini kama Rais angetaja majina ungekuja hapa na thread nyingine ya kupinga.
Mimi sina upeo mkubwa nisaidie hayo magazeti ni yapi mkuu
 
Nauliza tu kuna tatizo tukayajua hayo magazeti natukaambiawa uchochezi waliouandika,isije ikawa wameandika habari zisizo mfurahisha mkuu zikaitwa ni habari za uchochezi ingawa habari hizo zikawa ni zakweli maana wakuu wa wilaya waliambiwa watakao tangaza katika eneolake kunanjaa atakuwa amejifukuzisha Kazi mwenyewe naikumbukwe kunamtangazaji wa ITV aliwai kureport katika wilaya flani kunanjaa akawekwa ndani kwa amri ya mkuu wa wilaya.Wananchi wenzangu tuwe tunafanya uchunguzi wakile kinachosemwa na tupime ukweli niupi sio tu kasema bwana mkubwa tukubali mengine tohoji tujue sisindio waajiri wao
 
Kwa mtu mwenye upeo mkubwa atafahamu majina ya magazeti yaliyopewa salamu za mwaka mpya.

Ninafahamu unajua majina ya hayo magazeti lakini unataka kuanzisha mjadala tu wenye mwelekeo mwingine kwa faida uzijuazo.

Chunguza hii sentesi ya Rais kama una fikra pana na utajua majina ya magazeti.

''Hatuwezi tukaiacha Tanzania ikawa dump la eneo la kuweka maneno ya uchochezi'', Alisema Rais.

Ninaamini kama Rais angetaja majina ungekuja hapa na thread nyingine ya kupinga.
Hebu weka hapa huo uchochezi uliochochewa na hayo magazeti,kisha tumjue na aliyechochewa,na utuambie alichochewa kwa nani,na huyo aliyechochewa aliathirika vipi na huo munaouita uchochezi! Usiishie hapo tu bali pia utuonyeshe reaction ya hao/huyo muliochochewa kwake!! Na uonyeshe lack of authenticity kwenye huo uchochezi ili u-fit kwenye shelf ya uchochezi!! Uweke na source ya huo uchochezi wa mchochezi ili tupime reliability yake--- baada ya hayo tutaweza kuongea lugha moja!!! Nimekuelewa mkuu Pascal Mayalla
 
Kinachonishangaza kuhusu viongozi wa kiafrika ni kuwa wanapenda sana kusifiwa. Wakikosolewa wanasema ni uchochezi. Pamoja na kupenda kwao sifa wameshindwa kujibebea sifa za bure kwa kuondoa njaa, maradhi, umaskini uliokithiri, ubovu wa miundombinu, elimu ya kichokoraa ambapo shule za msingi na sekandari hazina hata matundu ya vyoo kwa ajili ya watoto kunya....

Cha kushangaza anayepinga kukosolewa kama kuna njaa serikali yake imeondoa ruzuku ya mbolea toka bilioni 76 hadi bilioni kumi. Haijanunua chakula cha akiba zaidi ya kutegemea tani elfu 90 alizoacha Kikwete. Jamani sifa inatakiwa uzitafute achaneni na hizi sifa za kijinga za kutaka kusifiwa hakuna njaa wakati wananchi hata mlo mmoja hawaumudu
 
Back
Top Bottom