Mhe. Rais wanaotishia Utawala wako ni Hawa...

the analyst, post yako kiboko. Kwa mtu mwenye akili tulivu hiyo post angeichukulia as a guidance to achieve his plans. Lakini kwa huyu boss nina mashaka.
Tabia yake ni sawa na ya wale jamaa wauzao mashamba ili wakamcheze ngoma binti yao.
 
Umegusa panapotakiwa. Mawazo yangu ni je hii itawafikia vipi waTZ ambao sio member wa JF, habari hii inagusa inapaswa kufikiwa na watu ili waelimike.

Kwanza nampongeza sana analyst kwa hili. Pili nilitoa wazo kuwa JF tuanzishe gazeti, alfu useful post kama hizi........ ziwekwe pale na hilo gazeti lifike kila sehemu? Sio lazima gazeti hilo lijumuishe post zote isipokuwa issue kama hizi. Kwa sasa mkuu analyst naomba upost hii makala yako Mwanahalisi wakati tunajadiliana jinsi ya kuwa na gazeti la JF. Niliwaomba viranja wakuu wa Jf wacalculate gharama za kulianzisha alafu waweke jamvini waona wadau tutachanga kiasi gani, tujaribu tuuuu. Again analyst thanks a lot.
 
the analyst, post yako kiboko. Kwa mtu mwenye akili tulivu hiyo post angeichukulia as a guidance to achieve his plans. Lakini kwa huyu boss nina mashaka.
Tabia yake ni sawa na ya wale jamaa wauzao mashamba ili wakamcheze ngoma binti yao.[/QUOTE

aahaahaahaaaaaaaaaaaaaaaaa, kwani si anazaliwa hukohuko pwaniiiiiiii!!!!!!!!!! ahahahahahahahaaaaa mwana umeua
 
Nasikitika saana kwa nchi zetu hizi watu wenyemawazo mazuri kama wewe hawasikilizwi na hufa na mawazo yao mazuri, very sorry sir hatuna mda wakusikiliza mawazo yako cc ndo mataahila wenyewe tumepewa rungu tunalitumia, sanasana unataka tukuue! BCS UMETOA KAULI ZA UCHOCHEZI!

Thanx Friend,
Sometimes hufikia hatua nikatamani kuuawa na viongozi mafisadi baada ya kutoa mawazo yangu kuliko kufa kwa njaa inayotokana ukwapuaji wa watu wachache wakati nikishangilia Kidumu Chama Cha Mafisadi!... Zidumu mbinu dhalimu za RA na wote walioko katika payroll yake!
 
Naam, adui mwingine ni Uswahiba. Mheshimiwa katika kipindi hiki ambacho Serikali yako inapata misukosuko kutoka kila pande za nchi kutokana na utendaji mbovu wa Watenda kazi wako ulioteuwa, ningekushauri (kama ungekubali kunisikiliza) kuvunja Baraza lako la mawaziri na kuteuwa watendaji kazi kwa misingi ya Ufanisi wao na sio kwa vigezo ulivyotumia ambavyo vinajidhiirisha kuwa Urafiki umepewa kipaumbele. Matokeo yake badala ya kuwasiliana na wewe kabla hawajatoa misimamo yao, wanakurupuka kujibu hoja. Baada ya hapo unachokuja kukisema kinakuwa kinapingana na kauli za watendaji wako. Kwa mfano; wakati malipo ya Dowans yanakuuzunisha kiasi cha kutamani hiki kikombe kitupite, watendaji wako baadhi walishadiriki kusema hadharani kuwa ni lazima tulipe..
 
Shikamoo Mkuu! (Sijui hata kama una kawaida ya kusoma JF au la! Naomba walau Tiss wakufikishie ujumbe wangu) maana inadaiwa JF ni ya Chadema lakini na sie tunaitumia.

Nimesikitika sana kutokana na ulivyoupokea mwito wa Chadema kukutaka utoe tamko kuhusu malipo ya DOWANS ama u-face nguvu ya Umma.

Yaani na nguvu zote zinazokuzunguka bado unahofia uwezekano ("wa kufikirika") wa kukuondoa madarakani Mzee? Tena jambo la kusikitisha unadhani uchochezi wa CDM utapata nguvu ya kuleta machafuko hapa nchini kiasi cha kuing'oa serikali yako halali (inayoongozwa kwa remote na RA) madarakani? Pole sana kwa mshtuko kama ulipata kweli. Naomba kupitia fursa hii nikupe dodoso kidogo.

Chadema kama chama (pamoja na kuwasingizia udini) hawana jeuri ya kukutisha wala kukuondoa madarakani. Kwa uchambuzi makini, kama rafiki zangu wakusanya habari muhimu za taifa watafanya kazi yao kwa makini watagundua kwamba maadui wakubwa na wanaotishia madaraka yako ni hawa wafuatao na sababu za wao kufanya hivyo. Inawezekana wakawapo wengine lakini mpaka dakika hii nawajua hawa hapa.
  1. Adui yako wa kwanza na anayeweza kukuondoa madarakani muda wowote akitaka ni huyu unayemdhania kuwa Swahiba wako, Bwana "RA". Ushahidi wote wa kimazingira unaonesha ukweli usiopingika kwamba huyu jamaa amekusaidia kufika katika kiti hicho kwa kutumia fedha zake (japo alizipora serikalini kupitia KAGODA nk.). Kama rohoni unalikubaliana na hilo ujue wazi kwamba mkono wake umefanikiwa kuzifikia zilizokuwa zinalipwa kwa Dowans na kwa kutumia hizo (akitaka) unaondoka mara moja. Kwani, unaweza hata kusukiwa mbinu ukafukuzwa na vikao vya chama chako kwa kushindwa kuongoza ama kutekeleza Ilani ya chama. Naamini tupo pamoja hata kama utakataa hadharani. Maana wewe na weye kwa kukataa tu unaongoza. Hey...! kweli...., huyu jamaa ndiye mmiliki halisi wa DOWANS japokuwa umiliki wake umefunikwa na idea ya "Powers of Attorney" maana kuna siku ulisema humjui. Uwezo wa huyu jamaa unaweza kuwanyima Ubunge baadhi wa wabunge wa chama chenu na hata watu maarufu na wenye nguvu kupoteza Uspika kwa njia ya "Gender balance issues" pale anapoamua. Sikufichi, mwogope huyu jamaa kama moto wa Jehanam. Kwa nguvu mliyomuuzia (na wewe unaijua) anaweza kufanya lolote. Kama huamini; itisha tume huru ichunguze wizi uliofanyika EPA, Richmond na ushahidi utumike kumbana RA mahakamani halafu uanze kuhesabu sekunde utakazokaa madarakani. Zikifika 60 nakula sumu. Mkuu, huyu jamaa anaweza hata kukulazimisha ujiuzulu mwenyewe na ukalitangazia taifa unajiuzulu kwa sababu za kiafya. Najua utabisha lakini roho inakusuta kwa kuwa unajua ukweli wa ninachokisema.
  2. Adui yako wa pili ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Unajua kwa nini? Mfano, matamshi ya Hosea kwa Afisa wa Ubalozi wa Marekani (miaka hiyo na baadaye kufichuliwa na wikileaks) yanatuonyesha kwamba hata hawa waliokuzunguka kwa karibu hawakubaliani na unavyoiendesha (au niseme RA anavyoiendesha) nchi hii lakini, hawana mahala pa kuzungumzia yanayowakera. Hawa ni hatari kwa kuwa kuna siku utataka kuzuia maandamano ya wanachi wanaoendelea kuchoshwa na utawala mbovu, kwa kutumia mabavu ya dola na watakugeuka (baada ya damu kidogo tu ya wananchi kupotea) kama kwa wenzetu waarabu. Kwa kauli nasema hawa wakiamua utaondoka maana hata nguvu hawatumii. Wao ni kuuchuna tu wenye machungu yao waandamane.
  3. Wanafiki ndani ya Chama chako kama alivyo Katibu wenu mkuu, huyo jamaa kutoka mkoa wa wanaume hapo ofisini kwako, na wengine wengi wenye tabia ya kuropoka ropoka (hata pale mnapokuwa hamjawasiliana) kuhusiana na jambo husika. Unakumbuka kauli yako kuhusu uchungu wa kuilipa DOWANS? (Najua haikutoka rohoni lakini...ndo ulivyosema) Katibu Mkuu alishaibuka na vitisho "Anayepinga anaweza kukihama chama maana tayari uamuzi umeshapitishwa kuwalipa nk..nk..." What do you expect from such guys". Wanawakera sana watu walio na mwanga juu ya upuuzi mnaoufanya huko madarakani na hii inachochea chuki kuliko mikutano na maandamano ya Chadema. I tell you, viongozi wengi wa Afrika ama ni waporaji au wametumwa kuwezesha matajiri waporaji, lakini wanafanya mambo hayo pasipo kuwashtua waliolala na wakishtuka hawawajibu kwa jeuri kama mnazotumia nyie. Mara "kelele za mpangaji...." Hivi unajua mtu mwenye kuelewa ulivyohandle maswala kama EPA, Richmond nk anavyojisikia uchungu mnapotoa majibu ya ki-mipasho penye malalamiko ya msingi? Yaani inawezekana mtu akatamani kufanya makosa yote ya Sehemu ya pili, Sura ya Saba ya Kanuni ya Adhabu. Unajua kwa nini? Mnajua wazi wenye makosa ni nyinyi halafu mnataka kutumia kutojua kwa wafuasi wenu masikini kumdharau mtu anayejaribu kusema ukweli. Tabia hii na hasa watu wanaokusaidia kuzifanya vinaweza kuvuruga nchi kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa sana kwa nchi na watu wake. Kama ni mapinduzi dhidi ya ungozi wako yanaweza kutoka hapa. Jamani mnakera! Raisi anasamehe suspect halafu anapohojiwa anajibu mipasho!
  4. Adui mwingine umeanza kumpandikiza wewe ukishiriana na Katibu mkuu wa chama chako. Mnasema nchi imeanza kuingia ktk udini baada ya kuona siasa zenu zilizokosa mwelekeo zinaanza kukosolewa zaidi. Kilichokupunguzia kura si udini! (na hata busara yako inakwambia ni kweli). Watu wameanza kushtukia promises za uongo ndani ya smiles zenu. Wameanza kuelewa ni jinsi gani watu ambao wao wanawashabikia wanaitafuna nchi kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu. They are not always ignorant, you know? Udini mnaodai umeanza kujitokeza, upo katika kutafuta mchawi wa failures zenu. Mimi na wewe tunajua wazi watanzania wenye uelewa wa chini na wa wastani hupendelea kuona mtu wa imani yao anashika madaraka kwa kuwa wanaona fahari hata pasipo kujua anawaletea nini. Wanaojua ndo utakuta wanamponda kiongozi mbovu pasipo kujali dini yake. Sasa unaposema udini umeanza unajua watu wa aina hiyo wanadhania nini? Wanadhani unapingwa na wafuasi wa dini nyingine kwa kuwa wewe ni dini tofauti (wakati wewe binafsi unajua wazi si kweli) na hatimaye wanaanza kuchukiana hata kwa kubishana tu. Waliosema wewe ni chaguo la Mungu mwaka 2005 walikuwa dini yako pekee? Tena wengi hawakuwa dini yako. Kwa nini wamebadilika basi? Umewaangusha na matarajio yao. JK! bado hatujawa na udini huo mnaodai unaanza kujitokeza isipokuwa kushindwa kwenu ndo kumewafanya mseme hivyo ili kuondoa kudharaulika kwa failures zenu.
  5. Kitakachokupindua ni tabia ya kutosema kweli kama... "Siwajui Richmond, Dowans, Kagoda wala sijawasamehe kwa wizi wao......" Hii ni hatari kwa kuwa mambo yanapofunuliwa na wanaojua inawakera wananchi wanaojua na baadaye wanaweza kuyafikisha kwa wasiojua vizuri and you know their reactions.
Ushauri wangu: Kama huwezi kufanya lolote kuisaidia nchi yako kupambana na matatizo ya msingi labda kweli angalia uwezekano wa kumrejeshea aliyekupa mamlaka achague mtu mwingine. Au yeye mwenyewe RA aongoze nchi tuone uwezo wake. Pengine atapunguza tamaa. Unajua hadi najikuta sijui nikuombe vipi ili uwe man enough to clear your own mess.

Hivi tukiacha politics, hapa tulipofikia, unaweza kuwakaripia watendaji wowote wanaokula rushwa na kutumia vibaya madaraka na mali ya umma kama hao wanaojilipa mabilioni kama lunch allowance katika maofisi yenu, wakakusikia?. Unaweza kusimama mbele ya wanaohitimu uafisa mathalani jeshi la polisi na kuwaambia rushwa ni mbaya? Unaweza kumwonya mtumishi wa Halmashauri anayelipa miradi hewa kwa fedha za walala hoi kuacha tabia hiyo vinginevyo umfukuze kazi?

Kama inafikia kipindi nafsi inakusuta hata unakosa ujasiri wa kuwaonya waliopo chini ya himaya hako ujue ndo chanzo cha kila tatizo ndani ya utawala wako. Watu mtapuuza hili lakini amini usiamini nchi maskini haiwezi kuendelea kama kiongozi wa nchi atakuwa hawezi kukaripia maovu hata kama ni kwa unafiki uliofichika na kuwafanya watu kuhofia adhabu. TAFAKARI!

Need we (tunaoitakia mema TZ) say more? Hongera mkuu kwa uchambuzi mahiri na kuweka kweli tupu juu ya hujuma dhidi ya serikali inayoratibiwa na JK!

A little comment kupinga madai juu ya udini unaohubiliwa na JK na clonies. Kwamba JK afahamu kuwa yeye si kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu muislamu hapa TZ kwa hao waliotangulia hatujawahi sikia swala la udini kwa sababu walikuwa wachapa kazi wa kweli!
 
Adui mwingine wa utawala huu ni wabunge wa ccm ambao ni wanafiki wakidhani wanamsaidia kumbe wanaibomoa serikali yake mbele ya jamii
 
Just a matter of time, lazima CCM itaanguka tena anguko kuu, na hakita simama tena, sati zetu zitasikika, maumivu yetu yatapungua kama sio kwisha kabisa.
 
Mimi sioni haja ya kuogopa machafuko ktk nchi hii ambayo waislam wameanza kudhulumiwa tokea ukoloni hadi uhuru. Njia ya kujikomboa ni lazima tanganyika yaje machafuko makubwa ya kidini ili baadae tuje na suluhu ya amani yenye haki sawa. Mimi sioni haja ya waislam kuogopa machafuko hapa. Nyie chadema anzisheni kama chadema kupitia kanisa na sisi waislam tutajibu mapigo. Ingieni barabarani kumn'goa rais dsm na sisi tunangia barabarani kumlinda. Kwani askofu hafi? Tunajua mutatuibia majumba yetu ya wapemba kariakoo nk lkn poa tu bora yaje machafuko tuwaone hao maaskofu wasiokufa kama kweli hawatakufa.
 
wewe mtabe wa nini unakua na mawazo mafupi kama maisha ya funza?analyst kapoteza muda wake kudadavua mambo muhimu yanayojiri ktk nchi yetu na kuyaanika hapa jamvini wewe unaongea vitu ambavyo vipo contrary kabisa na mada husika...hebu tuambie uislam wa RA au MNJ Na jk unakusaidia nini?try to think beyond your race,beyond your tribe,beyond your religion ndio uanze kuchangia mada kama hizi. . .
 
Kama kawaida ya jk na wapambe wake, watasoma yataingilia sikio moja na kutoke jingine then wanaendelea na mambo yao kama kawaida. Sikio la kufa hilo......
 
Mimi sioni haja ya kuogopa machafuko ktk nchi hii ambayo waislam wameanza kudhulumiwa tokea ukoloni hadi uhuru. Njia ya kujikomboa ni lazima tanganyika yaje machafuko makubwa ya kidini ili baadae tuje na suluhu ya amani yenye haki sawa. Mimi sioni haja ya waislam kuogopa machafuko hapa. Nyie chadema anzisheni kama chadema kupitia kanisa na sisi waislam tutajibu mapigo. Ingieni barabarani kumn'goa rais dsm na sisi tunangia barabarani kumlinda. Kwani askofu hafi? Tunajua mutatuibia majumba yetu ya wapemba kariakoo nk lkn poa tu bora yaje machafuko tuwaone hao maaskofu wasiokufa kama kweli hawatakufa.

Ndugu yangu Mtabe,
Asante kwa kuchangia mada niliyoitoa hapo awali (japo kwa kuingiza mada tofauti). Mwingine anaweza kukuona kama usiyefanana na JF (Home of Great Thinkers) lakini mimi nakuona kama miongoni mwa changamoto zilizopo nchini. Naamini nchi yetu haiwezi kutoka hapa ilipo pasipo kuaddress changamoto za aina hii.
Wewe ni miongoni mwa wale wanaoshabikia saaaana...! lakini wagumu saaana....! wa kutafakari japo kiduchu (Usijisikie vibaya kwa kuwa upo hivyo, maana hata hao Maaskofu uliodai hawafi baadhi yao ni wa aina yako). Watu wa aina yako wapo wengi kiasi kwamba natamani kungekuwa na platform ya kuwafikia wote kwa pamoja ili tujaribu kuwapa changamoto kidogo ambayo ingewafanya wapate mwanya wa kutafakari japo kiduchu.

Leo naanza na wewe: Tafadhali naomba utumie muda wako wa mapumziko kujibu maswali yafuatayo kisha tafakari upya mtazamo wako. Kama bado unapata tabu kuelewa usimame wapi nitumie private message niangalie nitakusaidia vipi ili uwe Mtanzania kifikra lakini wakati huo huo uendelee kufuata Amri za Mwenyezi Mungu kwa dini yako na upunguze masononeko yasiyokuwa ya lazima.
  1. Je, hii nchi ina watu wenye imani kutoka madhehebu mangapi tofauti ya dini?
  2. Je unajua uwiano wao wa idadi kwa uhakika? Waislamu...?, Wakristo...?, Wahindu....?,Wabudha...?, Wenye dini za asili.....? Wapagani...?,
  3. Je unajua kwamba baadhi yao hubadilika kutoka dini moja kwenda nyingine au dhehebu moja kwenda lingine na ktk nyakati tofauti?. Je Unajua kwamba kuna watu wamewahi kubadili dini au madhehebu zaidi ya mara moja?
  4. Je kazi ya serikali ni nini hasa?, Kazi ya Rais...?, Waziri...?, Watumishi wa Umma...?
  5. Je unadhani ni bora kuwa na rais aliyeshindwa majukumu yake kutoka dini yako kuliko anayefanya vizuri majukumu yake lakini wa dini tofauti?............. Kama jibu lako katika swali hili ni NDIYO, Usihangaike kutafakari zaidi maana utaugua kichwa. Watu wanaoamini rais akiwa Mkristo kumshutumu ni kushutumu au kuwaonea wakkristo wana tatizo ambalo linahitaji ushauri nasaha kutoka kwa professionals.
CHADEMA SI WADINI KAMA UNAVYODHANI. CC-MAFISADI WANAWEZA KUSEMA LOLOTE KWA SASA ILI WAHURUMIWE MAANA KWA UTUMBO WALIOUFANYA WANANCHI WAMEANZA KUWASHTUKIA NA HAWAJUI WATAKWEPA VIPI HUKUMU YA WALIOWADHANIA KUWA WADANGANYIKA SIKU ZOTE.
******************** POLE SANA FRIEND, SI KOSA LAKO! *************************************
 
Maneno msumari,HONGERA.
CCM wasome maandishi haya na wakubali kubadilika.
Naandika kuhusu kitengo cha propaganda cha CCM kwani nimeshtushwa na walemavu waliokuwa wanatoa maneno ya kupinga maandamano,nahisi wamenunuliwa.
 
Shikamoo Mkuu! (Sijui hata kama una kawaida ya kusoma JF au la! Naomba walau Tiss wakufikishie ujumbe wangu) maana inadaiwa JF ni ya Chadema lakini na sie tunaitumia.

Nimesikitika sana kutokana na ulivyoupokea mwito wa Chadema kukutaka utoe tamko kuhusu malipo ya DOWANS ama u-face nguvu ya Umma.

Yaani na nguvu zote zinazokuzunguka bado unahofia uwezekano ("wa kufikirika") wa kukuondoa madarakani Mzee? Tena jambo la kusikitisha unadhani uchochezi wa CDM utapata nguvu ya kuleta machafuko hapa nchini kiasi cha kuing'oa serikali yako halali (inayoongozwa kwa remote na RA) madarakani? Pole sana kwa mshtuko kama ulipata kweli. Naomba kupitia fursa hii nikupe dodoso kidogo.

Chadema kama chama (pamoja na kuwasingizia udini) hawana jeuri ya kukutisha wala kukuondoa madarakani. Kwa uchambuzi makini, kama rafiki zangu wakusanya habari muhimu za taifa watafanya kazi yao kwa makini watagundua kwamba maadui wakubwa na wanaotishia madaraka yako ni hawa wafuatao na sababu za wao kufanya hivyo. Inawezekana wakawapo wengine lakini mpaka dakika hii nawajua hawa hapa.
  1. Adui yako wa kwanza na anayeweza kukuondoa madarakani muda wowote akitaka ni huyu unayemdhania kuwa Swahiba wako, Bwana "RA". Ushahidi wote wa kimazingira unaonesha ukweli usiopingika kwamba huyu jamaa amekusaidia kufika katika kiti hicho kwa kutumia fedha zake (japo alizipora serikalini kupitia KAGODA nk.). Kama rohoni unalikubaliana na hilo ujue wazi kwamba mkono wake umefanikiwa kuzifikia zilizokuwa zinalipwa kwa Dowans na kwa kutumia hizo (akitaka) unaondoka mara moja. Kwani, unaweza hata kusukiwa mbinu ukafukuzwa na vikao vya chama chako kwa kushindwa kuongoza ama kutekeleza Ilani ya chama. Naamini tupo pamoja hata kama utakataa hadharani. Maana wewe na weye kwa kukataa tu unaongoza. Hey...! kweli...., huyu jamaa ndiye mmiliki halisi wa DOWANS japokuwa umiliki wake umefunikwa na idea ya "Powers of Attorney" maana kuna siku ulisema humjui. Uwezo wa huyu jamaa unaweza kuwanyima Ubunge baadhi wa wabunge wa chama chenu na hata watu maarufu na wenye nguvu kupoteza Uspika kwa njia ya "Gender balance issues" pale anapoamua. Sikufichi, mwogope huyu jamaa kama moto wa Jehanam. Kwa nguvu mliyomuuzia (na wewe unaijua) anaweza kufanya lolote. Kama huamini; itisha tume huru ichunguze wizi uliofanyika EPA, Richmond na ushahidi utumike kumbana RA mahakamani halafu uanze kuhesabu sekunde utakazokaa madarakani. Zikifika 60 nakula sumu. Mkuu, huyu jamaa anaweza hata kukulazimisha ujiuzulu mwenyewe na ukalitangazia taifa unajiuzulu kwa sababu za kiafya. Najua utabisha lakini roho inakusuta kwa kuwa unajua ukweli wa ninachokisema.
  2. Adui yako wa pili ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Unajua kwa nini? Mfano, matamshi ya Hosea kwa Afisa wa Ubalozi wa Marekani (miaka hiyo na baadaye kufichuliwa na wikileaks) yanatuonyesha kwamba hata hawa waliokuzunguka kwa karibu hawakubaliani na unavyoiendesha (au niseme RA anavyoiendesha) nchi hii lakini, hawana mahala pa kuzungumzia yanayowakera. Hawa ni hatari kwa kuwa kuna siku utataka kuzuia maandamano ya wanachi wanaoendelea kuchoshwa na utawala mbovu, kwa kutumia mabavu ya dola na watakugeuka (baada ya damu kidogo tu ya wananchi kupotea) kama kwa wenzetu waarabu. Kwa kauli nasema hawa wakiamua utaondoka maana hata nguvu hawatumii. Wao ni kuuchuna tu wenye machungu yao waandamane.
  3. Wanafiki ndani ya Chama chako kama alivyo Katibu wenu mkuu, huyo jamaa kutoka mkoa wa wanaume hapo ofisini kwako, na wengine wengi wenye tabia ya kuropoka ropoka (hata pale mnapokuwa hamjawasiliana) kuhusiana na jambo husika. Unakumbuka kauli yako kuhusu uchungu wa kuilipa DOWANS? (Najua haikutoka rohoni lakini...ndo ulivyosema) Katibu Mkuu alishaibuka na vitisho "Anayepinga anaweza kukihama chama maana tayari uamuzi umeshapitishwa kuwalipa nk..nk..." What do you expect from such guys". Wanawakera sana watu walio na mwanga juu ya upuuzi mnaoufanya huko madarakani na hii inachochea chuki kuliko mikutano na maandamano ya Chadema. I tell you, viongozi wengi wa Afrika ama ni waporaji au wametumwa kuwezesha matajiri waporaji, lakini wanafanya mambo hayo pasipo kuwashtua waliolala na wakishtuka hawawajibu kwa jeuri kama mnazotumia nyie. Mara "kelele za mpangaji...." Hivi unajua mtu mwenye kuelewa ulivyohandle maswala kama EPA, Richmond nk anavyojisikia uchungu mnapotoa majibu ya ki-mipasho penye malalamiko ya msingi? Yaani inawezekana mtu akatamani kufanya makosa yote ya Sehemu ya pili, Sura ya Saba ya Kanuni ya Adhabu. Unajua kwa nini? Mnajua wazi wenye makosa ni nyinyi halafu mnataka kutumia kutojua kwa wafuasi wenu masikini kumdharau mtu anayejaribu kusema ukweli. Tabia hii na hasa watu wanaokusaidia kuzifanya vinaweza kuvuruga nchi kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa sana kwa nchi na watu wake. Kama ni mapinduzi dhidi ya ungozi wako yanaweza kutoka hapa. Jamani mnakera! Raisi anasamehe suspect halafu anapohojiwa anajibu mipasho!
  4. Adui mwingine umeanza kumpandikiza wewe ukishiriana na Katibu mkuu wa chama chako. Mnasema nchi imeanza kuingia ktk udini baada ya kuona siasa zenu zilizokosa mwelekeo zinaanza kukosolewa zaidi. Kilichokupunguzia kura si udini! (na hata busara yako inakwambia ni kweli). Watu wameanza kushtukia promises za uongo ndani ya smiles zenu. Wameanza kuelewa ni jinsi gani watu ambao wao wanawashabikia wanaitafuna nchi kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu. They are not always ignorant, you know? Udini mnaodai umeanza kujitokeza, upo katika kutafuta mchawi wa failures zenu. Mimi na wewe tunajua wazi watanzania wenye uelewa wa chini na wa wastani hupendelea kuona mtu wa imani yao anashika madaraka kwa kuwa wanaona fahari hata pasipo kujua anawaletea nini. Wanaojua ndo utakuta wanamponda kiongozi mbovu pasipo kujali dini yake. Sasa unaposema udini umeanza unajua watu wa aina hiyo wanadhania nini? Wanadhani unapingwa na wafuasi wa dini nyingine kwa kuwa wewe ni dini tofauti (wakati wewe binafsi unajua wazi si kweli) na hatimaye wanaanza kuchukiana hata kwa kubishana tu. Waliosema wewe ni chaguo la Mungu mwaka 2005 walikuwa dini yako pekee? Tena wengi hawakuwa dini yako. Kwa nini wamebadilika basi? Umewaangusha na matarajio yao. JK! bado hatujawa na udini huo mnaodai unaanza kujitokeza isipokuwa kushindwa kwenu ndo kumewafanya mseme hivyo ili kuondoa kudharaulika kwa failures zenu.
  5. Kitakachokupindua ni tabia ya kutosema kweli kama... "Siwajui Richmond, Dowans, Kagoda wala sijawasamehe kwa wizi wao......" Hii ni hatari kwa kuwa mambo yanapofunuliwa na wanaojua inawakera wananchi wanaojua na baadaye wanaweza kuyafikisha kwa wasiojua vizuri and you know their reactions.
Ushauri wangu: Kama huwezi kufanya lolote kuisaidia nchi yako kupambana na matatizo ya msingi labda kweli angalia uwezekano wa kumrejeshea aliyekupa mamlaka achague mtu mwingine. Au yeye mwenyewe RA aongoze nchi tuone uwezo wake. Pengine atapunguza tamaa. Unajua hadi najikuta sijui nikuombe vipi ili uwe man enough to clear your own mess.

Hivi tukiacha politics, hapa tulipofikia, unaweza kuwakaripia watendaji wowote wanaokula rushwa na kutumia vibaya madaraka na mali ya umma kama hao wanaojilipa mabilioni kama lunch allowance katika maofisi yenu, wakakusikia?. Unaweza kusimama mbele ya wanaohitimu uafisa mathalani jeshi la polisi na kuwaambia rushwa ni mbaya? .
mkuu hii kitu itafutie nafasi kwenye moja gazeti yetu imesimama
 
Big up Analyst , umegusa angles zote ambazo mwenye timamu ataafiki.
Tazizo ni sikio la kufa halisikii dawa! Hawa viongozi wetu wamejaa viburi mno..ila u have done ur part
 
magazeti yakiandika hayo yatafungiwa ingawa ni ukweli mtupu.
Kuna mchangiaji mmoja kasema,habari hiyo itumwe ikulu kwa njia ya barua/pepe. Ni wazo zuri nami naongeza,ushauri/maoni hayo ya bandikwe kwenye mbao za matangazo mbali mbali nchi nzima hata kwenye miti.
 
Back
Top Bottom