Mhe. Rais: Vunja Baraza na Bunge!

Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.

Mzee mwanakijiji,
You made my day!
Unanidai crate moja ya bia na tukikutana pale pahala basi nidai kwa nguvu zako zote!
Jamani haya sio yaliyoandikwa kwenye ule ujembe - TANZANIA TUMEKWISHA???? na akina Bluray wakalalamika kuwa eti yaliyoandikwa yalikuwa ni sawa na treason na kuwa itapelekea JF ifungwe na jamaa zake?
Ni kweli kabisa kuwa, ilikuendelea Tanzania must start afresh - ikiwa ni kwa mapinduzi, ikiwa ni kwa people's insurrection, ikiwa ni kwa kuvunja bunge, ikiwa ni kwa kuivunja serikali yenyewe, etc etc - ni lazima uozo uliopo uangamie mara moja ndio tena hapo tutaweza kuibuka. Bila ya hivyo, tutaendelea na ufisadi wetu maisha.
Kuvunja bunge na baraza la mawaziri haitosaidia kitu, lakini at least Mwanakijiji unafahamu kuwa hii serikali ya sasa haina faida kwetu wananchi and it has to go!
Mtu yoyote miongoni mwetu anaesema kuwa kuiangamiza hii serikali ya hivi sasa ni treason, basi huyo ni fisadi kati yetu. Tutakapoanza tena mafisadi wote watakula risasi kama alivyokula Ceacescu wa Romania!!!
There is no other way!!! Piga risasi mafisadi wote - this is the only way!!!
Almost miaka 50 ya uhuru sasa imepita and still watoto wetu wanakaa chini shule!!! Is this not treason by itself??????????
 
Hivi nini msingi wa hoja hii? Mwanakijiji nahisi kunakitu ume-smell au vi-inzi vimeleta na umetunyima sisi. Maana sioni kama JK anaubavu wa kufanya jambo lolote kubwa. Ameshindwa kufanya maamuzi juu ya EPA, Richmond, Muungano, muafaka nk leo avunje baraza na bunge?
 
Naona wewe ni dizaini ya mbugua wa miaka ile ya 90!! Labda Mwanakijiji atukatie kidogo kama anazo tips zozote. Hapa hatuna mtu mwenye ubavu wa kufanya hata 1% ya hayo anayoyasema. Na bahati mbaya hatuoni mtu yeyote mwingine anayeweza kutusaidia kuigeuza hii serikali, bunge na mahakama kichwa chini miguu juu. Safari bado ni ngumu na ndefu na Masia wetu hajazaliwa.
 
hapo kwenye red sijakuelewa kabisa, huenda kiswahili changu ni kidogo sana. ufafanuzi tafadhali.
 
hapo kwenye red sijakuelewa kabisa, huenda kiswahili changu ni kidogo sana. ufafanuzi tafadhali.

Pole ndugu yangu naona miaka ya 90 hukuwepo nchini au ulikuwa bado hujasikia habari za Nkrumah Hall pale Mlimani. Kuna jamaa anaitwa Bethuel Mbugua alitishia usalama wa watu kwa kuonesha kuwa ni kipanga wa ajabu tena akiwa na umri wa miaka 9 tu. Hebu fuatilia habari zake zaidi katika hii link: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-elimu-education-forum/4709-mtoto-kipanga-2.html.
 
Thubutu! Sidhani kama anaweza kuvunja bunge ili aanze upya. na yeye aweza kutokomea hukohuko. Kwa sababu kamati kuu watasema ameshindwa kuilinda katiba ya CCM JUU chama kileleta mapinduzi ya wanyonge kukandamizwa na mafisadi. hongera baba wa mtandao ............. umeleta EPA Richmond na buzwagi
 
akivunja bunge na kufukuza mawaziri sina kumbukumbu ya haraka hapa ila nahisi maana yake kikatiba tunafanya uchaguzi tena, itamfanya aitishe uchaguzi....
na hatakuwa na uhakika wa kuchaguliwa na kupata uraisi tena...No one is ready to risk!!
 
Anaweza kulivunja, lakini hiyo ina maana inabidi tufanye uchaguzi kabla ya 2010, endapo atalivunja.

Rais hana control ya Bunge (in terms of its constituency) maana members wake wanaingia mle kwa kuchaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi mkuu. Of course ukiachilia mbali wachache anaowateua. So hata akilivunja uchaguzi ukafanyika, watarudi anawataka na asiowataka.

Kwa upande wa baraza la mawaziri sawa; anaweza kulivujna na kuliunda jinsi atakavyo. Ingawaje hata akifanya hivyo mara kumi kwa siku, sioni cha tofauti anachoweza kukifanya. Tatizo nadhani ni yeye mwenyewe na wala sio wanaomzunguka. Wapo watu wazuri mno nchi hii; wenye uwezo wa kuleta mabadiliko ya ajabu. Mimi na ujinga wangu wote kama ningekuwa kwenye position yake, ningeji-surround na hawa watu wanifanyie kazi.

Labda Mwanakijiji anamaanisha 2010 iko mbali mno ukilinganisha na jinsi nchi inavyojiendesha bila uongozi - so bora atangaze kuachia ngazi ili uchaguzi mkuu ufanyike tupate rais?
 
Rais hana control ya Bunge (in terms of its constituency) maana members wake wanaingia mle kwa kuchaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi mkuu. Of course ukiachilia mbali wachache anaowateua.

Hivi unajua wanachi wanaletewa mgombea kutoka katika vyama? kifupi hiyo kitu ya wanachi kuchagua wawakilishi wao hai exist hapa Tanzania, klatiba haitoi fursa hiyo kwani imevipa vyama uwezo wa kuchagua wagombea pia sheria za uchaguzi zinaweza kumvua mtu ubunge iwapo chama kitaamua hivyo..unakumbuka habari ya Mrema? Kifupi powers za rais hapa tanzania kikatiba hazipimiki.
 
Ili uwafunge goli wabaya wako. Tuanze upya kwani sasa unajua urais ni zaidi ya ving'ora na saluti.

Mwanakijiji,
Once again you are sending us a coded message that appears undecipherable to some of us ordinary mortals. Surely Prez cannot dissolve Parliament hardly a year before the next scheduled general elections, as you would have us believe, so that is clearly not in the cards. It serves no useful political purpose that I can think of, other than perhaps flexing his Presidential biceps and throw his weight around, but to what end? It makes no sense to me.

Normally, when you release these short “Mwanakijiji-ciphered” messages, it’s sign that you’ve been told something by what you consider to be a reliable source along the lines of something major percolating underneath the national political scene and ready to spill over. There is no point keeping it secret you might as well spill the beans for JF readers’ benefit!

OK, Tueleze, Kainzi kamekuambiaga kitu gani? Mwaga muchele!
 
Anaweza kulivunja, lakini hiyo ina maana inabidi tufanye uchaguzi kabla ya 2010, endapo atalivunja.

Ndiyo, inawezekana mkuu na ndio maana tunalia kila siku katiba yetu inampa nguvu nyingi raisi.

Kichekesho namna gani wakati sheria inamruhusu rais kufanya hivyo!!!???!!!

Okay...naona wote mmetoa majibu positive bila evidence yeyote. Nimepitia Katiba chapchap na vifungu nilivyoona ni hivi:

46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii,
Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa
mujibu wa masharti ya ibara hii.

....

na hii hapa:

65.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano.

Sasa waheshimiwa...ningeomba evidence kutoka kwenu inayoonyesha Rais ana nguvu ya kuvunja bunge, badala ya maneno matupu.
Shukran...
 
Safi sana ndugu yangu. Sina katiba hapa ila naomba uangalie kipengele kinachohusu nini kinaweza kutokea endapo Bunge litakataa kupitisha hoja ya serikali kama vile bajeti. Na labda kama kuna kipengele kinachogusia nini kifanyike endapo Rais atatofautiana na Bunge katika maamuzi mengine yaliyofanywa na Bunge!
 
Jamani suala sio rais kuvunja baraza la mawaziri wala bunge, ushauri huo mnaompa rais ni wa woga. Kwa mamlaka aliyonayo Rais na madaraka makubwa aliyopewa na katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania au tuliompa wananchi, anao uwezo wa kuwaondoa madarakani mawaziri wote ambao yeye anadhani wameshindwa kazi au hawafai. Kwa maana hiyo kwa Rais kumtoa waziri madarakani hahitajiki kuvunja baraza la mawaziri wala bunge labda utuambie kuwa Rais anawaogopa mawaziri ambao yeye mwenyewe aliwachagua
 
watanzania inatakiwa tufike sehemu tujue kuwa kuna mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa rais kuyarekebisha na sio lazima avunje baraza zima la mawaziri. Ila usipotenganisha urafiki na utendaji kazi inakuwa ni vigumu sana kugundua kuwa rafiki yako anakuangusha na hawezi kazi. Nadhani hilo ndilo linalomsibu Rais kwani alichagua mawaziri kwa kigezo cha urafiki zaidi ya uwezo wa watu kufanya kazi ndio maana mawaziri wote wenye PhD feki ni wale ambao wapo karibu na Rais, mfnao Kamala na Nchimbi ambaye tayari kesha muasi raisi na kujipenyeza kwa Lowassa
 
Kwa suala kama hili kwa sisi wasomi hatuhitaji katiba kwani suala hapa msio kuvunja bunge au kuvunja baraza la mawaziri, suala ni kuwatoa mawaziri wenye uwezo dhaifu wa kitendaji, hapa hapahitajiki kuvunja baraza. ila kama tunaamini kuwa wabunge wote ni hovyo na mawaziri wote ni hovyo hapo inabidi Rais avunje bunge lakini kama suala ni mawaziri tu, kikatiba hahitajiki kuvunja baraza la mawaziri labda kama waziri mkuu akijiuzuru
 
Back
Top Bottom