Mhe.Rais Samia,Je,unafahamu/unajua unavyo hujumiwa Katika Manispaa ya ILEMELA?

Mar 6, 2018
21
15
Kwanza kabisa Nianze kwa kukupongeza kwa namna unavyotekelaza majuku yako kwa namna ya kipekee kiasi kwamba nchi imetulia. Kama ilivyo kwaida ya Binadamu, wapo wanaobeza utendaji wako, wapi wanaofurahia,wapo wanaotoa ushauri, wapo wanaokosoa na wapo wapambe ambao kazi yao ni kukusifu mchana lkn usiku wanakuhujumu.
Mhe. Rais chapa kazi wote hao ni Watanzania ,Wasikilize na yaliyo mazuri fanyia kazi Mama.
Katika Manispaa ya ILEMELA tunaye mkurugenzi mpya, Ambaye alichukua nafasi Paul Wanga uliyemhamishia geita. Hakika mkurugenzi huyu amakuwa msaada mkubwa Sana kwa wananchi/wakazi wa Ilemela hasa kutatua kero za ardhi, Kukusanya mapato ya ndani kwa bidii na kusikiliza na kutatua kero za wananchi mmoja mmoja bila ya matatizo yoyote. Aidha, matatizo ya Raia yanayohitaji kutatuliwa na mamlaka zingine amekuwa akiekeza kwa lugha inayostahili na kuelekeza uende wapi. Wanna Ilemela tunakupongeza Sana kutuletea mkurugenzi huyu.
Pamoja na hayo Mhe.Rais, wapo Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya Manispaa hi wa hasa wa idara ya ardhi wakishirikiana na Baadhi ya wateule wako na Baadhi ya madiwani kukuhujumu wewe na kumkwamisha mkurugenzi Katika kutekwleza majukumu yake kikamilifu. Baadhi ya watendaji hao ni pamoja Kyando, Brigitte,Bwana mmoja Ambaye yupo ofisi ya Afisa ardhi wa Manispaa wakiwemo madiwani ndugu Swila na diwani wa nyakato Huku Vita hivi vikisimamiwa na kukingiwa kifua na Wateule wako wawili.
Mhe.Rais, hujuma dhidi ya mkurugenzi ipo kwa kiasi kikubwa ktk migogoro ya ardhi.
Kwa mfano. Kuna Bwana mmoja ni marehemu anaitwa manumbu.alnunua shamba miaka ya tisini na akapanda miti.Upumaji ulipofantika Katika eneo hili, vikipatikana zaidi ya kumi na tano. Genge la Kyando wakataka kuwapa warithi wa marehemu viwanja 4 tu.Warithi walipokataa,Genge hili liliandaa mkataba bandia wa mauziano Kati ya marehemu manumbu na Bwana mmoja aitwaye Lauson wa Dar Huku wakimuomba mkurugenzi huyu ashiriki dhuluma hii. Mkurugenzi alikataa katakata na akawambia mwambieni mnuuzi alete hati ya mauziano. Genge la Kyando kuona hivyo walianza mchakato na mpango mahususi wakishirikiana na Wateule wako wawili kumchafua mkurugenzi ili umuondoe mkurugenzi huyu hapa Ilemela. Mpango huu unafanywa kwa Siri kubwa Sana mhe.Rais. Katika tuhuma hi ya ardhi Wateule wako ambao wamenufaika na ardhi na kuandika majina ya ndugu zao ili wasijukukane yapo.Mhe.Rais naomba uunde au tuma kikosi kazi wako waje Ilemela ili ushuhudie uozo uliyopo na namna wanavyokuhujumu wewe binafsi......inaendelea
 
Back
Top Bottom