Mhe.Rais Magufuli wananchi tunaomba uifute NECTA kwa kushindwa kubaini watumishi wenye vyeti feki

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
616
Mhe .rais magufuli tunaomba wananchi uifute NECTA maana imeshindwa kuwabaini watumishi wenye vyeti feki Mara nyingi wananchi wamekuwa wakitoa taarifa za watumishi wenye vyeti feki lakini baraza hili la necta haliwashughulikii hata kidogo mfano askari polisi wa musoma central police mkoani Mara wapo wengi wana vyeti feki na taarifa zimetolewa necta lakini wao hawalifanyii kazi wapo kimya wanapenda rushes kila kona .

Tunaomba fumua uongozi wa necta wanafanya kazi kwa mazoea uhakiki wa watumishi hewa sasa unamaliza mwaka mzima lakini necta haijawahi kutoa takwimu sasa za watumishi wa umma wenye vyeti feki je ? Hawapo ? Kama hawapo kwanini mnahakiki vyeti ? Mwaka mzima ? Huu ni uzembe mnawaumiza watumishi wenye vyeti halali hii siyo sahihi hata kidogo .
 
Ha ha ha suala vyeti fake ni gumu sana na lingefuatiliwa ipasavyo si ajabu hata Ndali mwenyewe angekutwa na cheti fake,kwa hiyo wameamuwa kulindana kwa mfumo wa kama ulifoji cheti cha kidato cha nne na ukaajiliwa kama mtu wa kidato cha nne,sasa utaajiliwa kama darasa la saba,kama ulipata ajira kwa cheti cha kidato cha sita cha kufoji sasa utaajiliwa kwa cheti cha kidato cha nne,kama ulikuwa na degree ya kufoji utaajiliwa kama mtu wa vidato.
 
Hapana mkuu

Tuache tumalize kwanza episode ya ngada halafu ndiyo uje na ombi lako...!!
Kwa sasa tuko busy na mambo matatu, ngada, kumtafuta Mbowe na kuhakikisha Lissu hapati urais wa TLS, mambo ya vyeti siyo issue...!!

Tafakari...!!
 
Necta wana uwezo Wa kubaini vyeti feki vya form iv na vi. Vyeti vingine vinatolewa na vyuo vyenyewe Mf. Vyuo vikuu haviko chini ya necta, hivyo chuo chenyewe binafsi ndio kinaweza kujua vyeti vyake halisi na feki, mwingine hawezi.

Bahati mbaya hakuna mfumo mmoja(database) Wa kusajili vyeti vyote nchini, hivyo ukaguzi unaoendelea in Wa kubahatisha tu. Wengi waliokimbia Kazi ni waoga tu, au walikuwa na vyeti vya watu wengine na hao watu wakawa wanavihitaji kwa ajili ya uhakiki.

Lakini wale waliofoji vyeti vya vyuo vikuu au diploma na certificate zilizo chini ya nacte hakuna mfumo Wa kuwabaini

Hii inafanya zoezi zima liwe ni adakabradakabra
 
Tuache tumalize kwanza episode ya ngada halafu ndiyo uje na ombi lako...!!
Kwa sasa tuko busy na mambo matatu, ngada, kumtafuta Mbowe na kuhakikisha Lissu hapati urais wa TLS, mambo ya vyeti siyo issue...!!

Tafakari...!!
mnatia hadi huruma, mbowe yupo dar wanashindwa mbeba angekua mkoa je
 
Mhe .rais magufuli tunaomba wananchi uifute NECTA maana imeshindwa kuwabaini watumishi wenye vyeti feki Mara nyingi wananchi wamekuwa wakitoa taarifa za watumishi wenye vyeti feki lakini baraza hili la necta haliwashughulikii hata kidogo mfano askari polisi wa musoma central police mkoani Mara wapo wengi wana vyeti feki na taarifa zimetolewa necta lakini wao hawalifanyii kazi wapo kimya wanapenda rushes kila kona .

Tunaomba fumua uongozi wa necta wanafanya kazi kwa mazoea uhakiki wa watumishi hewa sasa unamaliza mwaka mzima lakini necta haijawahi kutoa takwimu sasa za watumishi wa umma wenye vyeti feki je ? Hawapo ? Kama hawapo kwanini mnahakiki vyeti ? Mwaka mzima ? Huu ni uzembe mnawaumiza watumishi wenye vyeti halali hii siyo sahihi hata kidogo .
Wangekuwa walimu au ma dk au kada zingine tofauti na askari nadhami wangesha fyekwa kitambo lakin kwa askari hao huu ndio mwaka wao naa wameteuliwa na aliye juu kama fungu jema kwake haina shida.
 
Back
Top Bottom