Mhe. Rais Kikwete na ziara ya Mabwepande

Mhe. Rais Kikwete na ziara ya Mabwepande

kajima

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2009
Posts
1,289
Reaction score
514
Kutoka katika taarifa ya habari ya TBC saa mbili usiku wa 20/03,mkuu wa kaya amedadisi maswala yanayowasibu wakazi wa eneo hilo lakini katika hali isiyotarajiwa akaamua kukutana na viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa wa jiji la Dar kujadili suala la maji jijini humo baada ya kuelezwa kama moja ya matatizo

Je Serikali imeanza kuonja joto ya changamoto ya wananchi, suala la maji limekuwa hoja mbichi kiasi cha kuandaliwa maandamano kwa suala hilo. Hongera JF, hongera wadau wa maendeleo wakiongozwa na Mbunge wa Ubungo, Mhe Mnyika.

Tanzania bora ipo KARIBU
 
Leo naona ameamka vizuri mkulu angekuwa anafanya hivi kila siku tungekuwa mbali. Sasa aendelee hivihivi na isiwe geresha
 
Napenda kuwajulisha kuwa kichwa cha habari original kilikuwa:

JJ MNYIKA ANAVYOJICHEKESHA KWA JK



Ama kweli CHADEMA mna kazi TENA NZITO.....halafu mnatafuta mchawi wenu ni nani wakati wasaliti mnao kibao chamani kama huyu JJ MNYIKA.

Huyu Mnyika na DEDI yao kule CHADEMA walitamka wazi kuwa HAWAMTAMBUI DR JAKAYA MRISHO KIKWETE kama rais halali wa Tanzania aliyechaguliwa kwa kura za haki....haya LEO KIKO WAPI?

Waswahili wanasema kuwa CHURA KARUDI MAJINI au ndio MWANA MPOTEVU amerudi tena tazama body language....Mnyika anajichekesha na kukenua meno ili aonekana na furaha ya kukutana na DR KIKWETE.


Kwa kuonyesha his TUE COLOURS, kwa kusudi kabisa kaacha kuvaa zile sare (khaki ) wanazovaa watalii wakija Tanzania kutazama ndezi, KINYONGA, nguchiro na nguruwe pori.

Unless hii nayo CHADEMA waseme kuwa imefanyiwa photoshop ili kumwonyesha Mnyika akiwa na furaha wakati kumbe alikuwa kakasirika....na ndio nini kuvaa suti kama ya JK au ndio bas tuu?

8E9U7951.JPG


8E9U7984.JPG
 
Nalipinga wazo lake la kuwapa wana mabwepande kila familia mifuko 100 kwani najua wataiuza mtaani na nyumba hawatajenga!bora govt ingejenga au kutoa muongozo na usimamizi wa nyumba zao
 
Asee hii picha ikiwekwa kwa projector naweza kuambia mnyika anameno mangapi ila suala linakuja ivi ht ww ukikutana na JK must utamkenulia ila daah mnyika nampa red card kazidisha asee
 
Inaelekea hoja ya Mnyika kuhusu maji imegusa watu!
 
Lazima Mnyika acheke JK anavyojitahidi kujiponya udhaifu
 
Huyu si ndiye alisema jk ni dhaifu?

Ndio na hajawahi na wala hatakaa aufute usemi huo, hapo mkulu nafikiri alikuwa anampa big up kijana kwa jinsi anavyoipeleka puta serikali yake. Nothing more
 
Kuna mmoja hapo anatamani auvunje mkono wa mwenzie kwa hasira alizonazo dhidi yake....si unaomwona mama na huyo askari walivyo 'standby' kutoa msaada endapo hasira zake zitakapomzi nguvu?
 
Weweeee. acha uchochezi wa gasia hapa. Mojawapo ya sifa za mwanasiasa ni kuchekacheka kila mahali... na kuinua mikono kusalimia watu kumbe anataka watu wamuone anapita. Mnyika ni mwanasiasa. Unategemea nini....
 
Huu ni ukomavu wa kisiasa, kimawazo na ustaarabu. Hawa wote wana lengo la kuitumikia nchi kwa njia pengine tofauti. Na inabidi hata wakiwa wapinzani wafanye kazi kwa ushirikiano kwa maslahi ya taifa. Sasa wakinuniana si itakuwa balaa ?
 
Back
Top Bottom