Mh. Mnyika hebu angaika na jimbo lako kwanza umetusahau ss tulikuchagua achana na hiyo idea haitekelezeki. Barabara mbovu, uchafu, maji n.k
kwani bei ya bidhaa ikishuka itakuwa imemsaidia pia mkazi wa jimboni kwake na hata pia watz wote, na khs maji siku ya tarehe 5/9/2011 mbunge aliandamana na wakazi wa ubungo hadi makao makuu ya dawasco na kukutana na afisa mtendaji mkuu ndg midala kilifanyika kikao cha shinikizo la nguvu ya umma kwa masaa 5 na hali ya maji kwasasa wananchi wa ubungo wanasema kuna mabadiliko makubwa na pia huyo midala atakuwa na ziara na mbunge mwanzo wa mwezi wa 11 kwa ajili ya kutazama hali ya upatikanaji wa maji ktk jimbo la ubungo, khs barabara kuna zinginemeshanza kutengenezwa kama ya temboni hadi kwa abbas, brbr ya milenia ya3, golani na nk. na hili jambo linawezekana la kuwa na sheria ya bei na sio wakina pinda kusema kuwa sukari ishushwe na hakuna anayeshusha zaidi ya kupanda na ni kauli za kisiasa na pia uzalishaji ni mwingi na ndio maana zinapelekwa kuuzwa nchi za nje, mahindi watu wanalima, mpunga pia unalimwa kwa wingi, tunayo gesi asilia, nk hivyo vyote kama tukuwa na sheria inayosimamia tutafanikiwa na si kuwa soko holela, inayosababisha leo watz tunalipa ada ya chuo in terms of dollar, na hata bidhaa leo unakwenda kwy maduka mengine unanunua bidhaa kwa dollar. hii ni kutokana na soko holela.Mh. Mnyika hebu angaika na jimbo lako kwanza umetusahau ss tulikuchagua achana na hiyo idea haitekelezeki. Barabara mbovu, uchafu, maji n.k
Tatizo ni kwamba kwa kwetu bongo wafanyabiashara wengi hawako honest na huwa wanatafuta hata asilimia 100 au zaidi ya faida na kwa kuwa walaji ni walalamikaji katikanchii ambao huwa hawawezi kufanya movement yoyote...lazima kuwe na sheria kama hizi japo zinakuwa anti-free market! Lakini pia, nchi kama yetu vitu kama hivi lazima viwepo kwani haiwezekani kila mtu ana-peg bei yake kwenye dola halafu watu wakae kimya eti soko huria. Tazama karo za shule zetu sasa hivi baadhi ya shule na vyoo ambavyo viko tz vinachaji karo kwa dola tena kwa watanzania ambao hawauzi chochote kuipata hiyo dola!
Hivi Mnyika ana taaluma gani? Jamaa anaweza kuwa na degree ya LANGUAGE sijui ndio Linguistic! Mambo ya Inflation atayajulia wapi?
Gad , kuendesha uchumi inahitaji taaluma na si hisia.Tatizo ni kwamba kwa kwetu bongo wafanyabiashara wengi hawako honest na huwa wanatafuta hata asilimia 100 au zaidi ya faida na kwa kuwa walaji ni walalamikaji katikanchii ambao huwa hawawezi kufanya movement yoyote...lazima kuwe na sheria kama hizi japo zinakuwa anti-free market! Lakini pia, nchi kama yetu vitu kama hivi lazima viwepo kwani haiwezekani kila mtu ana-peg bei yake kwenye dola halafu watu wakae kimya eti soko huria. Tazama karo za shule zetu sasa hivi baadhi ya shule na vyoo ambavyo viko tz vinachaji karo kwa dola tena kwa watanzania ambao hawauzi chochote kuipata hiyo dola!
Mnyika azidi kucharukia mfumuko wa bei
Na Tamali Vullu
(Tanzania Daima 24th Oct 2011)
"Kutokana na kukithiri kwa mfumuko wa bei za bidhaaa mabali mbali mchini. Mbunge wa Ubungo John Mnyika,anakusudia kuwasilisha muswada binafsi Bungeni ili Serikali itunge sgeria ya kudhibiti bei za bidhaa muhimu.
Akizungumza na waandishi wa hahari jijini Dar es salaam, Mnyika alisema kutokana na mfumuka wa bei za bidhaa muhimi, hali ya maisha ya Watanzania imezidi kuwa ngumu kila kukicha.
Alisema hali hiyo ikiachwa hivi hivi ni hatari kwa uchumi wa nchi na kwamba Taifa linaweza kuingia katika machafuko makubwa."
My Take:
Mtazamo wa utatuzi wa mfumuko wa bei nchini nasikitika kucomment kuwa si wa kisomi sana na nilitegemea fikra zaidi kutoka kwa Mh. mnyika juu ya hili.Nakubaliana na Mnyika as far as the EFFECTS za mfumiko wa bei na si zaidi ya hapo.
Si jambo linaloeleweka kuwekea sheria mfumuko wa bei-to the layman yes.
Tulikubali wenyewe zaidi ya miaka ishirini na tano iliyopita juu ya kutumia nguvu ya soko katika kuendesha uchumi.Sijui ni wangapi wanaoikumbuka SCOPO ya Ndg Wilfred Mwabulambo.
Ilifanya kazi tu katika misingi ya ujamaa na controlled economy. Leo tukipanga aei za vitu muhimu wakati uzalishaji hakuna hilo halieleweki wala si sustainable. Nilitegemea Mh Mnyika akazanie UZALISHAJI mali wa bidhaa hizo kwa nguvu zote na kwa tija ili bei ziweze kushuka.
Leo ukipangia bei ya sukari kuwa Tshs 1,900 wakati demand yake inadictate at Tshs 2,500 ni kujidanganya.
Bidhaa inakuwa muhimu kwako pale tu unapoweza kumudu kuinunua, bidhaa hiyo ikiwa nje ya uwezo wako ina-cease kuwa na umuhimu kwako.
Wabunge wetu vijana nawashauri msome sana hizi economical dynamics ili muweze kutumika vizuri katika vyombo mnavyo wawakilisha wananchi.
Kikubwa zaidi ni serikali yenyewe kubana matumizi yake ili matumizi yalingane na kipato chake. Kinachoelekea kuwa kimetokea (mfumuko wa bei)ni kuwa Serikali inaendelea kuchapisha fedha zisizo na backing ya uzalishaji, hivyo more money chasing the few commodities at large.Serikali ikiendelea na msimamo huu tuatuwa na pesa nyingi sana kwenye mzunguko wa biashara, fedha ambazo si halali kuwepo.
Nina uhakika economists waliobobea wana cheka juu ya hii suggestion ya Mh Mnyika kwa vile haitekelezeki.
Majoja,
Nashukuru sana kwa maoni yako. Natamani sana kama kuna mwanahabari ambaye alikuwepo kwenye mkutano wangu wa jana aeleze kwa kina zaidi niliyoyangumza jana. Suala la kupeleka muswada wa sheria ya udhibiti wa bei ya bidhaa muhimu ilikuwa ni moja tu ya orodha ndefu ya njia nilizozieleza ambazo Tanzania inapaswa kuzichukua kama sehemu ya hatua za dharura za kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha ambako kwa sehemu kubwa kumechangiwa na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu ya Tanzania. Suala la kuongeza uzalishaji nililisisitiza na kutaka hatua za dharura kwa msukumo wa Rais na Bunge. Katika kuongeza uzalishaji wa ndani naamini katika kupanua fursa kwa wazalishaji wadogo na wa kati katika sekta za kilimo na viwanda kama jambo la haraka. Hapa tutashughulikia tatizo la kutokuwa na uwiano wa urari wa kibiashara (balance of payment) ambapo sasa taifa letu ni la wachuuzi badala ya wazalishaji; tunanunua kuliko tunachouza. Lakini nilikwenda mbele zaidi kwa kueleza kwamba kutokana na matatizo katika nchi za magharibi hasa athari za mdodoro wa uchumi duniani na sasa matatizo ya kifedha Eurozone na udhaifu wa utegemezi wetu toka nje; hali ya kifedha ya nchi ni mbaya kwa kuwa serikali haijafunga mkanda- bado kuna ubadhirifu, ufisadi na matumizi mengine ya anasa wakati hali ya mapato hairidhishi. Kwa vyovote vile hatua za dharura zinahitajika na nikatoa mwito kwa Rais Kikwete akutane na tume ya mipango na baadaye akutane kwa dharura na baraza la mawaziri kuweka msukumo wa haraka kwa kuwa tunapokwenda kama taifa hali itakuwa tete; mfumuko wa bei umefikia 16.8%, kubadili dola moja kwenda shilingi ni 1700. Ni maoni yangu kwamba hatuwezi kuamini Wizara ya Fedha na Benki Kuu pekee katika kushughulikia hali hii; tunapaswa kuunganisha nguvu ya wadau wetu wote: wataalamu, sekta binafsi nk. Uongozi Mkuu wa nchi unapaswa kutoa msukumo unaohitajika kufikia azma hii. Naelewa kwamba gharama za vyakula na nishati zinamchango mkubwa sana katika mfumuko wa bei. Hata hivyo, ieleweke kwamba matatizo yetu ya chakula ni zaidi ya uzalishaji na ukame; tuna tatizo pia la usambazaji. kwa kuwa hivi sasa wakati ambapo kuna maeneo yana njaa na maeneo yenye chakula cha bei juu; kuna maeneo ya nchi yetu chakula kinaoza au kinauzwa bei chee. Ushahidi wa kwamba kuwa tuna matatizo ya kimfumo na kiuongozi ni kuwa hata chakula kutoka hifadhi ya taifa ambacho kilitolewa kwa maelezo kuwa kinakwenda kupunguza bei kwa gharama yako na yangu lengo husika halijafikiwa; bei bado iko juu na sehemu ya chakula hicho kinatoroshwa na kuuzwa kinyemela nje ya nchi. Matamko ya viongozi pekee ya kwamba bei ya sukari na sembe iwe kwa kiwango kilichotangazwa hayajasaidia. Walau kukiwa na sheria, tutapata nguvu nyingine ya kuwabana badala ya kutegemea kauli zao za kisiasa pekee. Tunaona kwamba pamoja na udhaifu wa EWURA katika upangaji wa bei elekezi na pia serikali kushindwa kupunguza kodi kwa kiwango tulichopendekeza bungeni na kuweka mifumo mizuri zaidi ya haraka ya uagizaji wa mafuta; bado walau bei elekezi inayotolewa inafuatwa kwa kuwa hatua hizo zinafanyika kwa misingi ya sheria sio kauli tu za kisiasa za viongozi. Hivyo; pamoja na taasisi zetu za fedha kuchukua hatua za kisera kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shilingi; pamoja na hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa na Rais, Bunge na vyombo vingine za kimfumo na kitaasisi za kuboresha uzalishaji na usambazaji hususani wa vyakula na nishati (umeme, gesi asilia), tunahitaji pia kuweka mifumo ya kisheria. Mimi ni muumini wa mrengo wa kati, naamani katika soko la kijamii- yaani uchumi mchanganyiko; kwa kuweka pamoja misingi ya dola kuhusika katika uchumi (ambayo hutumiwa zaidi katika ujamaa) na uhuru wa soko (ambao hutumiwa zaidi katika mifumo ya kiliberali na kibepari). Hata hivyo, nasikitika kwamba nchi yetu haifuati ujamaa wala soko huria; ni nchi yenye mfumo wa soko holela. Wakati nikitoa mwito kwa Rais na Bunge kuzisimamia taasisi nyingine na kuongoza sekta binafsi na umma kunusuru hali ya mambo kwenye uzalishaji na usambazaji ili kupunguza mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shilingi yetu; napenda pia pawepo na nguvu za kisheria hususani katika bidhaa chache na muhimu; Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo; hata baadhi ya nchi zenye kuamini katika soko huria, serikali na dola huingilia kati pale soko linaposhindwa au pale ambapo kuna ulazima wa kulinda maslahi ya umma. Ugumu wa maisha unaochangiwa na kupanda kwa bei na gharama ni tishio kwa uchumi na usalama wa nchi na wananchi ni suala ambalo tunahitaji kuunganisha nguvu kulishughulikia; tusipoziba ufa tutajenga ukuta. Na kwa kweli ni kati ya mambo ambayo wananchi wa jimbo la Ubungo wamenituma niwawakilishe, nilihoji suala hili kwenye mikutano ya hadhara, na nimepata ridhaa yao. Tuendelee kujadiliana kupata maoni zaidi
JJ
Hii it never works.., huwezi kuleta wawekezaji na ushindani at one hand alafu kwa upande mwingine uwapangie bei, hii italeta scarcity na magendo.
Cha kufanya ni kuongeza production.., tena Ndugu Mbunge angepeleka muswada wa kuzuia huu ugawaji ardhi kwa wawekezaji ili walime bali hii ikiwa mikononi mwa jamii / state / vyama vya ushirika na kuzalisha surplus bei itashuka.. Alafu kumbuka hizi taasisi zitakuwa pale sio kwa ajili ya profit bali service.., hivyo basi wanaweza kuzalisha bidhaa za kutosha kwa bei nafuu kwa mwananchi.
Uwekezaji uletwe kwenye issues kama viwanda na usindikaji sababu huu utaleta ajira kwa watu