Mhe. Mbowe hakukamatwa polisi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Mbowe hakukamatwa polisi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Isike, Dec 12, 2011.

 1. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Labda kama kuna maana nzuri zaidi au maneno ya kitaalam juu ya weledi wa kazi ya kipolisi, lakini Mwenyekiti Mbowe hakukamatwa na polisi kama ilivyoripotiwa katika moja ya thread hapa jamvini, chanzo cha habari ikiwa ni stori kutoka Gazeti la Nipashe.

  Polisi walifika pale usiku, wakisema walishtushwa na milio ya fataki zilizopigwa usiku katika hafla hiyo ya shughuli mbalimbali za kijamii zilizofanyika siku hiyo ya Desemba 10. Kwanza wasingeweza kuonana na Kamanda Mbowe moja kwa moja, walilazimika kuzungumza na mmoja wa wakurugenzi wa CHADEMA, John Mrema. Walimwomba na kumsihi sana Mrema awadasaidie waweze kuonana na Kamanda Mbowe maana ndiye mwenye hafla, wajue hasa kulikoni.

  Waliingia ndani. Vijana kadhaa kama wanne watano hivi, walikuwa na sare na silaha, waliingia pamoja na OCCID (kama sijakosea, cheo cha Mkuu wa Upelelezi Wilaya). Huyu bosi wao ndiye aliyekwenda kuzungumza na Kamanda Mbowe. OCCID akamwomba Kamanda Mbowe baada ya hafla, actually it was a cocktail party, apitie kituoni, akiahidi kuwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA taifa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni (government in waiting) hatachukua zaidi ya dakika 20, atakuwa ameshamaliza kuandika maelezo juu ya milio ya fataki, kisha ataondoka kwenda nyumba. Ndicho kilichotokea na kufanyika!
   
 2. n

  noma Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  asante kwa ufafanuzi. Ilikuwa saa ngapi na baada ya mkia wa jogoo kuisha mbowe alichukua muda gani hapo kituoni
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  fataki si ziliruhusiwa kwa mbwembwe mnazi moja kawe na mbagala??
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Magwanda at work.
   
 5. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Huu ni ushahidi wa UBWEGE wa magamba na polisi. Huenda wakasema Mbowe alikuwa anatoa mafunzo kwa kikundi cha ugaidi. Na ushahidi wao ni fataki. Ha ha ha ha...........................
   
 6. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Asante kwa ufafanuzi.
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Magwanda walipotosha umma.
   
Loading...