Mhe: Edward ngoyai lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe: Edward ngoyai lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Nov 26, 2011.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila binadamu amejaliwa kuwa na kipaji chake na kipaji halisi hutoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndiye Muumbaji na mgawaji wa vyote kwa wanadamu ila kuna vipaji vingine ambavyo hutokana na mambo mbali mbali mathalan elimu n.k. Naungana na NOVA aliyejitahidi kuwakilisha hisia zake kwa Ushairi na kuonesha yale yaliyo moyoni mwake.

  Binafsi nianze kwa kukupongeza kwa ujasiri, uvumilivu na hatua uliyofikia kuzungumzia yale uliyokuwa nayo ambayo kwayo baadhi ya Watanzania wasio na ushabiki na wenye nia njema kwa Watanzania wenzao wameweza kugundua yaliyokuwa sirini yatosha kusema kuwa japo ulichelewa ila sasa UMESHAFIKA. Mhe. Lowassa yaliyokupata naamini kama ni mwanadamu mwingine asiye na uvumilivu, staha na hata ujasiri basi ungekuta ameshazikwa ila ninacho amini ni kweli kwamba MTETEZI wako yu hai. Natambua una familia na umezungukwa na marafiki ambao wengi wao hawakuwa wakipendezwa kabisa na jinsi ulivyokuwa unashambuliwa kwa kejeli, matusi na dhihaka zisizo kuwa na kikomo yapata miezi saba kama mwenyewe ulivyosema ila sasa naamini wote wamepata japo kwa uchache kujua kuwa mchele ulikuwa upi na chuya vile vile.

  Si rahisi sana kuamini kwamba ulijaribu kushawishi kuvunjwa kwa mkataba uliosababisha wewe kufikia hapo ulipo lakini vile vile si rahisi mtu wa kawaida kuamini kuwa uliwajibika kwa maslahi ya Chama na Serikali yako pia, ila tamko lako basi litufungue fikra na mawazo yetu. Na kama kweli "urafiki wenu si wa barabarani Israeli na aseme sasa." Kuna baadhi ya vyombo vya habari vilieleza kuwa wakati ukiwasilisha hoja yako kuna baadhi ya Wajumbe walionekana kutaka kulia ukweli ni kwamba kama hayo uliyoyasema ndivyo ilivyokuwa sintashangaa hata mtu akili na nashawishika sasa kuamini yale maneno yako kwamba "ulionewa sana na ulidhalilishwa sana" huu msalaba, haya mateso na hatimaye udhalilishaji na matusi yote na jina ulilobandikwa la kifisadi hukustali ila naamini umwaminiye alisimama imara katika kuhakikisha hutetereki.

  Yatosha kusema unastahili pongezi, na sasa hata mimi binafsi naweza kusimama mbele ya umati wa watu nikasema neno juu yako kwa kuwa nitakuwa na ujasiri si tu wa kuwasilisha mada ila vile vile ya kutetea na kujenga hoja kwa hoja kwa nadharia na ushahidi. Samehe mara Saba Sabini sisi ndio vijana mlio tuzaa na tunajaribu kwa namna moja ama jingine kuhakikisha majina yetu yanajengeka katika mwamba imara japo tunaonekana kukosa hekima, busara, maarifa, uwezo, vigezo na hata staha katika kufanya hayo ndiyo maana tunaishia kukutukaneni tukiamini kuwa kwa kufanya hivyo basi tutakuwa na wakati mzuri na wakati mwingine tunaonekana kutumiwa na pande zisizotutakia mema. Mhe kwa kuwa vijana tumepotoka na utukufu wa Mungu unaelekea kupungua kwetu tusamehe manake naamini si wote walio hivyo kwa hiyo kwa kupitia wale wachache basi na wengine nao wapata msamaha naamini nao pia watakaa na kutafakari na kisha watatubu.

  Nikutatakie heri katika yote na naamini wana Monduli, wana wa Arusha na vitongoji vyake wanakusubiri kwa hamu kwani "Mlifurahi pamoja, Mlihuzunika pamoja na mtasonga mbele pamoja"

  Ni mwanzo mwingine wa hatua 1,000 mbele....................... I believe as we goby the game will change now from an enemy of the to a man of the people..............
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Natamani pangekuwepo maandamano ya kwenda kumpokea huyu shujaa
   
 3. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Naunga mkono hoja, Edo is a state man, ingekuwa ni SITA amatukanwa namna hiyo tungeshuhudia vita, kubenea kumwandika vibaya kidogo kampakazia kununuliwa na mafisadi,Nape kasemwa kidogo jamiiforums kaanza kulia na kwenda kushtaki facebook, Edo hakugombanaa na waandishi, ameendelea kuwa mpole na mmnyenyekevu, this is a kind of a leader we want
   
 4. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Siyo Edward Lowasa tu bali ni Edward Ngoyai Laigwenan Lowasa.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Lowassa mjanja sana! anajua kucheza na akili za wabongo!
   
 6. P

  Paul Makonda Verified User

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mungu huwaacha waovu wadumu ili kulilejesha Taifa katika haki au kulikomboa,kama alivyo mwacha Falao ktk taifa la Misri ili kuwakomboa Waisraeli ndivyo Mungu amemwacha Edward Lowassa afanye uovu wake ili Taifa lipate kulejea kwa Mungu.kwani matendoyake yanatosha kabisa kuwafanya watu wakeshe Makanisani na Miskitini.Mh Lowassa nakuomba uendelee kuwa FISADi wakimataifa kama ulivyosema sikumoja bungeni,nanukuu ( watanzania wanajuwa,na mataifa yanajuwa)mwisho wa kunukuu.
   
 7. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  I support EL.
   
 8. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Jamani tuelezane basi huyo Lowassa anakugawieni ngapi ngapi? mbona watu wanatoka povu bila sababu? EL tayari keshajichimbia shimo na hatoki, JK lazima atammaliza kiaina kwani kaamuumbua mbele ya wajumbe wa NEC, kumbukeni kuwa JK ni mtu wa visasi sana kwa historia ya nyuma tunavyomjua...wangapi leo wanalima huko mashambani kisa hawakumuunga mkono alipokuwa unautafuta urais?
   
 9. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Ebwana eeh! Utadhani tushafika 2015. Mpeni kichwa chetu naye tuone, labda anaweza akawa na nafuu kidogo.
   
 10. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hahaha! Hana ubavu wa kumpeleka Laigwanan mkuu kulima!
   
 11. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,802
  Likes Received: 17,890
  Trophy Points: 280
  sitegemei mfuasi wa shetani kuwa mcha Mungu, Kuna mzee alinambia Lowassa anaweza kuabudiwa, na sasa nimeamini
   
 12. e

  emalau JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  When "Great thinkers" don't sound like great thinkers! Why JF members keep talking about Lowasa, we should think big let's talk about issues not people.
   
 13. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  WAKUU naona kama vile EL ameanza kuzipangua tuhuma moja baada ya nyingine na amesema wanaomwita fisadi wanamtukana. JE ukweli uko wapi? Si ilinenwa kwenye ukweli uongo hujitenga, mbona imekua kana kwamba EL ndio mkweli hata kuvuta hisia za WATU? Au ni usahaulifu ndio tatizo. Some one pump in what wrong has EL done to his country now that he has punched out the famous Richmond saga? Tena kwenye mkutano.
   
 14. fige

  fige JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere alimuuliza siri ya utajiri wake sidhani kama aliwahi kujibu.Kama wenzetu mlioanza kutuaminisha ni msafi mnajua tunaomba mtuambie siri hiyo ambayo ilishindikana kuitoa kwa mwalimu !

  Namna ya uongozi wa Lowasa hata akiwa Raisi kuharibu ni sekunde hilo halijafichika.Mfano ,wazo la shule za kata lilikuwa zuri lakini utekelezaji ukawa mbovu kwani badala ya shule tumepata majengo ya shule(mabovu) na wanafunzi (wasiojua hata kusoma) .Na makovu kibao kwa kushurutishwa kuchanga.Sijui tunamsifia kwa lipi ?au ile michango ya makanisani na misikitini ?au TB Joshua kaanza kazi ya kinaijeria ?
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Nov 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Let CCM support EL to contest for presidency so that he paves the way for the Peoples Power!
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,601
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  Hadi usawa huu,aliowakubali Nyerere na aliowakataa wote sawa tu.

  Chama chake hakifai,na since is no longer(RIP) unategemea nini?

  Kipindi kile cha nyuma alisema kina "Ufa" kuanzia kwenye msingi...Sasa sijui angesema nini this time?

  Unajuwa hata yule alie ji brand "Mr Clean" alichofanya mara baada ya mwalimu kufariki?

  Ule ushetani wao ndo ukanonekana wazi wazi,huwa nashangaa mtanzania wa aina gani anayeweza kuitendea nchi yake uhuni kama huo.

  Yani sipati majibu.
   
 17. fige

  fige JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hakika hakuna anayefaa sembuse Lowasa,je yeye ndiye leo hii anaonekana msafi kati ya hao wachafu ?Au sifa ya ziada ni ipi ,pengine jicho langu la tatu ni bovu ?
   
Loading...