Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Usafiri wa treni jijini Dar es Salaam kwa sasa umekuwa maarufu sana na umeondoa adha kubwa ya usafiri iliyokuwepo kabla. Wakazi wanaoishi maeneo ya Pugu, Gongolamboto, Ubungo pamoja na maeneo yote yanayopitiwa na treni hiyo watakubaliana nami kuwa usafiri huu ni mkombozi wao mkubwa.
Ni usafiri wa haraka na hauna bugudha kama kwenye dala dala. Kama itatokea usafiri huu ukasitishwa linaweza kuwa janga la jiji. Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe ndiye aliyeanzisha huu usafiri katikati ya jiji. Nampongeza sana kwa maono yake ambayo yametusaidia sana wana Dar es salaam.
Hakika anastahili TUZO, ingekuwa kule kwetu UK angepewa heshima ya kuitwa"SIR” kama akina Fergeson. Hongera Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe