Mhasibu wa jiji la Arusha atakiwa kujisalimisha Polisi akidaiwa kutafuna Tsh. Milioni 85 kila mwezi za mzani wa mazao ya chakula

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,283
2,000
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amemtaka mhasibu wa jiji hilo, Charles Jacob kujisalimisha polisi kwa madai ya kutafuna Sh85 milioni za makusanyo ya kila mwezi kuanzia Machi, 2019 katika mizani wa mazao ya chakula.

Amesema tangu mizani hiyo ilipoanzishwa Machi, 2019 imekuwa ikiingiza Sh3.3 milioni kwa mwezi badala ya Sh88 milioni, kwamba Sh85 milioni kila mwezi hazijulikani zinapokwenda.

Jacob, msimamizi wa mizani hiyo pamoja na wafanyakazi wake wawili, Thobias Julius na Agness Loishiye wanadaiwa kusababisha upotevu huo wa fedha.

Madeni amewaweka ndani wafanyakazi hao na kuagiza Jacob ambaye hakuwepo kazini kujisalimisha mwenyewe kituo cha polisi kati Mkoa wa Arusha.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 20, 2019 Dk Madeni amesema kituo hicho cha kukusanya ushuru hakifanyi vyema na kusababisha fedha nyingi kuishia mikononi mwa wakusanyaji na mhasibu huyo.

“Nilifuatilia muda mrefu ukusanyaji wa mapato nikagundua kuna ulaji mkubwa wa fedha unaofanywa na mhasibu huyo ndio maana leo hajaja hapa.”

“Anaelewa mchezo anaoufanya na wafanyakazi wake nitahakikisha nawaweka ndani wote wanaojaribu kucheza na fedha ya Serikali sitamwonea mtu yeyote huruma,” amesema Dk Madeni

Amebainisha kuwa kuna wafanyakazi wachache wanaiibia Serikali mapato, kuahidi kupambana nao.

Awali, wafanyakazi hao walipewa nafasi ya kujitetea na kubainisha kuwa wameshindwa kukusanya mapato kutokana na magari kuwa machache, hawafahamu kama fedha wanayokusanya kama inafika au haifiki katika halmashauri.

Mchumi wa Jiji la Arusha, Anna Mwambene amesema wamekuwa wakifuatilia vyanzo vya mapato mbalimbali kuangalia utendaji wa kazi, kubaini upotevu wa fedha unaofanywa na watendaji wasio waaminifu.
 
stanleyRuta

JF-Expert Member
Jul 19, 2014
818
500
Heheheheheh kwani kuwaweka ndani ndo kunasaidia kurejesha hzo pesa!!!!.Ishakuwa fashion kuweka watu ndani siku hzi.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,522
2,000
Nchi hii kuna watu wana ujasiri wa kuiba haijapata tokea!

Imagine kuna watu wametafuna pesa za Vitambulisho vya Wamachinga vilivyotolewa na Rais pamoja na Mikwala yote siku ya kuwakabidhi ma RC

Halafu hadi kina Mama nao wamo siku hizi

Kuna Mtendaji sijui wapi huko kauza vitambulisho kakusanya pesa zote kaenda kuzinywea Pombe kama vile zake
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,896

USIPO BORESHA MAFAO YA WATUMISHI USITARAJIE UPIGAJI UTAPUNGUA!!
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,896
2,000
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amemtaka mhasibu wa jiji hilo, Charles Jacob kujisalimisha polisi kwa madai ya kutafuna Sh85 milioni za makusanyo ya kila mwezi kuanzia Machi, 2019 katika mizani wa mazao ya chakula.

Amesema tangu mizani hiyo ilipoanzishwa Machi, 2019 imekuwa ikiingiza Sh3.3 milioni kwa mwezi badala ya Sh88 milioni, kwamba Sh85 milioni kila mwezi hazijulikani zinapokwenda.

Jacob, msimamizi wa mizani hiyo pamoja na wafanyakazi wake wawili, Thobias Julius na Agness Loishiye wanadaiwa kusababisha upotevu huo wa fedha.

Madeni amewaweka ndani wafanyakazi hao na kuagiza Jacob ambaye hakuwepo kazini kujisalimisha mwenyewe kituo cha polisi kati Mkoa wa Arusha.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 20, 2019 Dk Madeni amesema kituo hicho cha kukusanya ushuru hakifanyi vyema na kusababisha fedha nyingi kuishia mikononi mwa wakusanyaji na mhasibu huyo.

“Nilifuatilia muda mrefu ukusanyaji wa mapato nikagundua kuna ulaji mkubwa wa fedha unaofanywa na mhasibu huyo ndio maana leo hajaja hapa.”

“Anaelewa mchezo anaoufanya na wafanyakazi wake nitahakikisha nawaweka ndani wote wanaojaribu kucheza na fedha ya Serikali sitamwonea mtu yeyote huruma,” amesema Dk Madeni

Amebainisha kuwa kuna wafanyakazi wachache wanaiibia Serikali mapato, kuahidi kupambana nao.

Awali, wafanyakazi hao walipewa nafasi ya kujitetea na kubainisha kuwa wameshindwa kukusanya mapato kutokana na magari kuwa machache, hawafahamu kama fedha wanayokusanya kama inafika au haifiki katika halmashauri.

Mchumi wa Jiji la Arusha, Anna Mwambene amesema wamekuwa wakifuatilia vyanzo vya mapato mbalimbali kuangalia utendaji wa kazi, kubaini upotevu wa fedha unaofanywa na watendaji wasio waaminifu.
MHASIBU KAPIGA VIMILIONI 85 MNAMUWEKA NDANI MBONA BWANA YULE KAPIGA TRILLION 1.5 PLUS KIVUKO HAMNA ALIYEMGUSA??

SOMO LA KUJIFUNZA:

UKIPIGA KIDOGO UNASWEKWA NDANI UKIPIGA TRILLIONS HAMNA MTU ANAKUGUSA, Sasa wapigaji jiongezeni!!
 
Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
17,722
2,000
Ķuna njemba ya nchi ya Malimali uko (katika sauti ya kinana) ilipiga 1.5 tril na bado inapumua tu sasa hivi inajistukia na kuanza kujiitwa mfungwa wa badae
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
12,381
2,000
MHASIBU KAPIGA VIMILIONI 85 MNAMUWEKA NDANI MBONA BWANA YULE KAPIGA TRILLION 1.5 PLUS KIVUKO HAMNA ALIYEMGUSA??

SOMO LA KUJIFUNZA:

UKIPIGA KIDOGO UNASWEKWA NDANI UKIPIGA TRILLIONS HAMNA MTU ANAKUGUSA, Sasa wapigaji jiongezeni!!
Unaachiwa kwa manufaa ya Taifa.
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,896
2,000
kwahiyo bw mhasibi alitakiwa alipwe shilingi ngapi ili asiibe?
Ilibidi ullize hivi...

"kwahiyo bw mhasibi alitakiwa aongezewe mshahara wake tokea mwaka gani ili asiibe?"

Haya, rudia kuuliza kama nilivyokufundisha ili nikupe jibu!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom