Mhasibu wa jiji la Arusha atakiwa kujisalimisha Polisi akidaiwa kutafuna Tsh. Milioni 85 kila mwezi za mzani wa mazao ya chakula

Kwani makwapukwapu hutakiwa kurejesha fedha alizokwapua kwa kubembelezwa huku akitokea nyumbani kwake?
Shauri yako na pole sana mkuu...kwa taarifa yako mali ya serikali hasahasa Tanzania huwa haina mwenyewe, wanaanzaga kwa mikwara ya kuwaweka ndani mwisho wa siku kesi zinakosa ushahidi watu wanarudi kitaaa kama kawaida. Bila shaka ushasikia maskendo kibao makubwa kwa madogo watu wakiwekwa ndani ni nani kati ya hao ulimsikia akihukumiwa au akirudisha hzo pesa??
 
Kweli aisee maana Kuna watu wengine Wana mahesabu makali na roho ya kujitoa mwanga akijua kwamba atakaa jela miaka 5 Kisha atarud uraiani kuponjoa mamilioni yake.
Kesi nyingi za serikali mara nyingi huwa ni za kukurupuka tu..mwisho wa siku huwa ni ushahidi hakuna watu wanarudi kitaani.
 
Ilibidi ullize hivi...

"kwahiyo bw mhasibi alitakiwa aongezewe mshahara wake tokea mwaka gani ili asiibe?"

Haya, rudia kuuliza kama nilivyokufundisha ili nikupe jibu!
siasa kila sehemu ndio zinafanya mshindwe kuwa na agenda maalum awamu hii.

sasa mhasibu anaonekana ni halali yake kuiba sababu ana mshahara mdogo
 
Ded anaongea kwa hisia Sasa hapo kwenye maelezo mbona hakuna namna ilioonyesha kaiba kwa namna gani maana fedha inakatwa kwenye mashine ambazo zimeunganishwa na mfumo wa LGRCIS ambapo mashine ikikata fedha inaonekana sehemu nyingi Sasa kala fedha au hakati huo ushuru anachukua rushwa magari hayakatii? Atoe ufafanuzi milion85 ni fedha nyingi sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom