Mhashamu Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa Angilikana Tanzania, John Ramadhani azikwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, akiambatana na viongozi mbalimbali leo Jumamosi tarehe 17 Septemba alihudhuria maziko ya Mhashamu Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa Angilikana Tanzania ambaye pia aliwahi kuwa Askofu wa Dayosis ya Tanga na Zanzibar , John Ramadhani.

Ibada ya Mazishi ilifanyika katika kanisa Kuu la Mkunazini na kuendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu William Mdolwa Maimbo.

Askofu John Ramadhani alifariki dunia tarehe 12 Septemba katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo uliokuwa ukivuja damu.
 
Hiyo picha mngeisogeza pengine ningetoa salamu zangu za mwisho kwa huyu Mtumishi wa Mungu.

Pumzika baba, heri yako hauna makandokando.

Raha ya Milele umpe ee Mungu.
 
Huyu alikuwa kati ya Watumishi Wa MUNGU wachache walioko Tanzania. Maana wengi tulio nao ni Viongozi wa Dini na sio Watumishi Wa MUNGU.
 
Hawajamzika ndani ya kanisa kama ilivyozoeleka kwa maaskofu wa kwanza kuzikwa kanisani Ref. Askofu wa kwanza wa Anglican Njombe Simalenga alizikwa ndani ya kanisa kuu la Anglican Njombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…