Mhando hakufikishwa mahakamani

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Mhando hakufikishwa mahakamani

Na Mhariri (Nipashe) | 7th October 2012

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), William Mhando, hakufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi, kama ilivyoripotiwa na Gazeti hili jana.

Jana Gazeti hili liliongea na Mhando kwa njia ya simu na kubaini kuwa habari hiyo haikuwa sahihi.

Habari hiyo ilieleza kuwa Mhando alifikishwa Mahakama ya Kisutu majira kati ya saa 8:30 na saa 9.00 alasiri lakini hakusomewa shitaka lake taarifa ambazo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ilizikanusha.

"Mimi jana nilikuwa nyumbani sikwenda kokote na hakuna ofisa yeyote wa Takukuru aliyekuja kunichukua kunipeleka mahakamani, nashangaa kusoma kwenye gazeti lenu kuwa nimefikishwa mahakamani…Siku nikipelekwa mahakamani nitawapigia simu mje kuripoti lakini msiandikie habari zisizokuwa za kweli," alisema Mhando.

Mhando alisema habari hiyo imemfanya ahisi ameonewa na kufadhaishwa mbele ya Watanzania.

NIPASHE inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa Mhando na familia yake na wasomaji wetu.
 
Wamemdharilisha, wamlipe na PCCB wafuatilie hilo gazeti maana limewafanya hawana akili kwenda mahakamani muda ukiwa umeisha
 
Back
Top Bottom