Mhando amkana mkewe mahakamani

Mhando amkana mkewe mahakamani

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,422
Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TANESCO, William Mhando, amemkana mkewe Eva Mhando mahakamani kwa kukataa kwamba Eva sio mke wake. Mkurugenzi huyo amefunguliwa kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na moja ya mashtaka yanayomkabili ni kula njama za kufanya ufisadi akishirikiana na mkewe, Eva, anayedaiwa kupewa zabuni ya mabilioni ya walipakodi kinyemela.

Source: Raia Tanzania.

MAONI YANGU
Naona wakili wa mhando ameamua kufanya hii kesi iwe complicated na kuchukua muda mrefu huku fisadi Mhando akizidi kutafuna fedha za umma alizojichotea. Haya ndio matatizo ya mawakili 'waganga njaa' tuliokuwa nao ktk nchi hii. Mawakili kama hawa hawana hata chembe ya uzalendo.

Mpaka vyeti vya ndoa vije vipatikane ili kuthibitisha uanandoa kati ya Mhando na Eva, kesi itakuwa imemaliza karne kabla ya kuamuliwa. Hivi nchi hii tumerogwa na nani?



ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi William Mhando, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kuwa mshitakiwa wa pili (Eva Mhando) katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka, si mke wake.

Mhandisi Mhando alitoa madai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Frank Moshi, alipokuwa akisomewa maelezo ya awali katika kesi hiyo na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai.

Mhando alikiri maelezo kuwa alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco tangu Juni 2010 hadi 2012, lakini alikana maelezo kuwa mshitakiwa wa pili (Eva Stephen Mhando) ni mkewe ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Santa Clara Supply Limited.

Kwa upande wake,- Eva alikubali kwamba aliwahi kuajiriwa na Tanesco kuanzia mwaka 1982 hadi 2009, mshitakiwa wa tatu, France Mchalenge pia alikubali kwamba alikuwa mwajiriwa wa shirika hilo, wakati uchunguzi unafanyika alikuwa mhasibu mkuu na alikuwa mjumbe wa Kamati ya Tathimini ya Zabuni namba Pa/001/11/HQ/G/011 ya vifaa vya ofisi, ikiwemo printa na kompyuta.

Swai alidai mshitakiwa wa nne, Sophia Misidai aliajiriwa na Tanesco na wakati uchunguzi unafanyika alikuwa mhasibu mkuu na mjumbe wa kamati iliyofanya tathimini ya zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi katika shirika hilo. Mshitakiwa alikubaliana na maelezo hayo.

Mshitakiwa wa tano, alikubali kwamba alikuwa mwajiriwa wa Tanesco na kuwa wakati wa uchunguzi alikuwa ofisa usambazaji na alikuwa mjumbe wa kamati iliyotathimini zabuni hiyo.

"Mheshimiwa Hakimu, Kampuni ya Santa Clara Supply Ltd inamilikiwa na Eva Stephen William, Fred William na Veronica Stephen Mhando, ilipata zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi yenye thamani ya sh milioni 884.5.

"Mhando akiwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo na Eva akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Santa Clara Supply Ltd alisaini barua ya kuipa zabuni huku akijua wazi kwamba kampuni hiyo inamilikiwa na familia yake, pia hakujitoa kuonyesha kwamba ana maslahi na kampuni hiyo," alidai.

Wakili Swai aliendelea kueleza kuwa Mhando aliwapa zabuni hiyo mshitakwa wa pili, Eva na watoto wake kinyume na utaratibu, walitaka kuiuza kampuni hiyo kwa mtu mwingine wakati tayari walishapata zabuni ya kusambaza vifaa hivyo vya ofisi, mshitakiwa wa kwanza (Mhando) alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kuonyesha kwamba ana maslahi binafsi na Kampuni ya Santa Clara," alidai Swai.

Swai alidai kwamba Eva alighushi taarifa za ukaguzi wa hesabu za Kampuni ya Santa Clara ya mwaka 2007/2008 akionyesha kuwa Kampuni ya Finx Capital House ilifanya ukaguzi.

Pia mshitakiwa huyo alighushi taarifa ya kuhamisha hisa akionyesha hisa 200 zenye thamani ya sh 10,000 zilihamishiwa kwa Eveta Shing'oma.

Eva alidaiwa kutoa taarifa ya ukaguzi wa fedha kwa Katibu wa Bodi ya Zabuni wa Tanesco akionyesha zilifanyiwa ukaguzi Desemba, mwaka 2010, akajipatia sh milioni 37.7 kutoka kwa shirika hilo.

Swai alidai Mchalange, Misidai na Naftali Kisinga walitoa taarifa katika Bodi ya Zabuni kuonyesha kwamba Kampuni ya Santa Clara walikuwa wana sifa ya kupata zabuni hiyo, walipata mkataba wa kusambaza vifaa vya ofisini wenye thamani ya sh 884,550,000. Washitakiwa hao walikana maeneo yote hayo.

Wakili Swai alieleza upande wa jamhuri unatarajia kuleta mashahidi 14 na wanawasilisha mahakamani vielelezo 18.

Hakimu Mushi aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 29-30, mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
 
Kwi kwii Mke alisemaje pale alipokanwa hadharani mahakamani? Kama Eve naye amekubali/atakubari kirahisi, hiyo ina implication kubwa, baadaye katika mgawanyo wa mali in case of anything. Eve anaweza huko usoni asipate kitu kwenye mali za Mhando kama ataachia hili liende hivi hivi na mahakama iamue kwamba Eve kweli sio Mke wa Mhando. Hii inanikumbusha kesi ya jamaa mmoja aliyefunga ndoa "fake" na mwalimu mmoja kwa kusudi la kumsaidia ahamie shule za mjini. Bahati mbaya yule bwana akafariki, yule mwalimu aliyefunga ndoa "fake" na huyo jamaa akajitokeza baada ya kifo akidai mgawanyo wa mali, kwamba na yeye ni mke halali wa ndoa wa marehemu kwa kuonesha marriage certificate!
 
Kwi kwii Mke alisemaje pale alipokanwa hadharani mahakamani? Kama Eve naye amekubali/atakubari kirahisi, hiyo ina implication kubwa, baadaye katika mgawanyo wa mali in case of anything. Eve anaweza huko usoni asipate kitu kwenye mali za Mhando kama ataachia hili liende hivi hivi na mahakama iamue kwamba Eve kweli sio Mke wa Mhando. Hii inanikumbusha kesi ya jamaa mmoja aliyefunga ndoa "fake" na mwalimu mmoja kwa kusudi la kumsaidia ahamie shule za mjini. Bahati mbaya yule bwana akafariki, yule mwalimu aliyefunga ndoa "fake" na huyo jamaa akajitokeza baada ya kifo akidai mgawanyo wa mali, kwamba na yeye ni mke halali wa ndoa wa marehemu kwa kuonesha marriage certificate!

Kuliko aingie jela kwa kujifanya mke wa Mhando ili tu apate mali huko mbeleni, bora hizo mali azisamehe huko mbeleni lakini leo asiingie jela!!
 
Iwapo mke atakubali kuwa Mhando sio mume wake issue itàkuwa imekwisha. Waendesha mashtaka hawataleta vyeti, Mhando ataleta cheti cha kuonyesha mke ni mtu mwingine kabisa.
 
wakili wake yuko kazini, yeye anachokifanya ni kutoa huduma kwa mteja wake,

je , ya tundu Lisu umeyasahau

Safi sana wakili! Tayari serikali ya magamba imeshalizwa hapo! Ooh mbona wanaishi nyumba moja? Mhando anasema alikuwa mpangaji wangu! Magamba kwishney!!
 
[
USIJIFANYE MJUAJI WA KILA KITU?KWANI WEWE NDIE NJAGU ULIOCHUNUZA SUALA HILI?YAELEKEA UNA MAFRASRESHENI YAKO

QUOTE=tpaul;9803541]Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TANESCO, William Mhando, amemkana mkewe Eva Mhando mahakamani kwa kukataa kwamba Eva sio mke wake. Mkurugenzi huyo amefunguliwa kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na moja ya mashtaka yanayomkabili ni kula njama za kufanya ufisadi akishirikiana na mkewe, Eva, anayedaiwa kupewa zabuni ya mabilioni ya walipakodi kinyemela.

Source: Raia Tanzania.

MAONI YANGU
Naona wakili wa mhando ameamua kufanya hii kesi iwe complicated na kuchukua muda mrefu huku fisadi Mhando akizidi kutafuna fedha za umma alizojichotea. Haya ndio matatizo ya mawakili 'waganga njaa' tuliokuwa nao ktk nchi hii. Mawakili kama hawa hawana hata chembe ya uzalendo.

Mpaka vyeti vya ndoa vije vipatikane ili kuthibitisha uanandoa kati ya Mhando na Eva, kesi itakuwa imemaliza karne kabla ya kuamuliwa. Hivi nchi hii tumerogwa na nani?[/QUOTE]
 
Ukoo wa panya,nchi hii imeishalizwa na wengi,ukianza na ndugu Change aliyesema ni vijisenti na hakuna aliyeuliza swali mpaka leo.Na huu ni mwendelezo,kama kweli watanzania tunataka mabadiliko,tuondoe ukoo wa panya kwanza.
 
...bonge la trick,kwani definition ya ndoa/mke ni nini ? Kama walikuwa wakiishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tayari ni mke na mume...

Mahakamani unatakiwa ushahidi mzuri usiotia shaka..."kuishi naye kwa miaka kadhaa" unaweza kukuthibitishaje mahakamani? Mahakama wanataka cheti halali cha ndoa (official document)kilichotolewa na mamlaka inayotambulika kisheria. Hapa ndipo penye ugumu. Usidhani kwamba wakili aliyemfundisha kumkana mkewe amekurupuka. Atakuwa amefanya legal analysis ya kutosha akaona kwamba Mhando akijitetea hivyo anaweza kuchomoka kwenye kesi hii. Sio kwamba ninatetea uhuni huu ila kwa mahakama zetu jinsi zilivyo ni vigumu sana kupokea ushahidi wa maneno/kusikia.
 
Back
Top Bottom