Mhadhiri wa UDSM Bashiru Ally na BBC

Uko sahihi kiongozi,wasomi wengi wa Bongo wanatumia hisia zaidi badala ya ukwel wa mambo.
 
Watanzania tunasaidi amani DRC.je utalaumu kwa nini hatuendi somalia pia.

kwani sisi ni polic wa dunia ?.waamerica wanajiita police wa dunia au wewe ujui ?. Sasa inakuwaje polic akiona msokoto wa bangi anakamata akiona fisadi anamwachia hapo kuna walakini.
 
Mbona muhadhiri nimempenda buree kajibu hoja vizuri sana shauri yenu msiyependezwa na maelezo yke

Tatizo watu wanaendeshwa na udini mbona Bashiru aliongea vizuri tu?

Na ni kweli hakuna ambapo Marekani alishaenda kutuliza vit na akaleta amani kote alikofanya hivyo aliacha civil war,mbona hili liko wazi?
 
kwani sisi ni polic wa dunia ?.waamerica wanajiita police wa dunia au wewe ujui ?. Sasa inakuwaje polic akiona msokoto wa bangi anakamata akiona fisadi anamwachia hapo kuna walakini.

Wakulaumiwa ni mwenye bangi na fisadi.wasijifiche kwenye mgongo wa yule anayetumia nguvu yake kurekebisha mambo.
 
Hivi mijadala ya kuongelea mambo mf. ya iraq au palestine kama anavyofanya bashru au makwaia uwa inasaidia?
 
Tabu ni pale unapopinga udini kwa udini!wakoloni nuksi kweli wamewafanya watu weusi wazione hizi dini ni zao hadi wanatukanana,chukiana na hata kuuana wakat wenyewe wanapiga hela kwa ujinga wetu

mkuu shushia na kitu bariiiid
 
Huwa ni kelele za mbu nje ya neti yenye ngao. Lakini mikutano ya kujadili katiba mpya ndyo haramu..
 
Wewe ndio nashangaa umakini wako wakati Israel inakwangua pale gaza na kulipua mabomu hovyo kule gaza hukushangaa hata siku mmoja marekani imeshindwa kulaani achilia mbali kuwasupport wapalestina? Nani mdini kati yako na Bashiru?????

Tatizo la Israel na Gaza ni la mataifa ya kiarabu na taifa la Israel.sio la kidnini.Wayahudi na Waarabu walikuwa maeneo hayo tangu miaka ya BC.ndio sababu wanatakiwa waachane na uhasama waheshimiane
 
Unapojichomeka katika siasa za mashariki ya kati lazima uwe makini ni mizozo ya muda mrefu na iliyo'ota mizizi mirefu....Mashariki ya kati kuna dini nyingine ndogo ndogo mbali ya Uislam na Ukristo kuna YAZIDIS-DRUZE-ALAWIS na hawa waliishi kwa pamoja kabla ya uvamizi wa wa Marekani nchini Iraq...hapa ni ukweli usiokatalika chanzo cha yote haya ni marekani kwani pamoja na ubaya wa Saddam Hussein hawa aliwakalia rohoni hakukuwa na hali kama hii ya kubaguana kidini au kikabila na hii ndio namna ya kutawala waarabu....Na ukitazama nyuma nchi kama Syria,Iraq,Libya na Misri dini hizi zilikuwepo na pengine tulikuwa hata hatujui,lakini tazama baada ya kuondoka watu kama Ghaddaf ,Mubarak na jitihada za kumuondoa Bashar al Assad watu wa dini hizi na watu wa kabila Kurd wamekosa amani kabisa...Halafu tusiwe wanafiki hawa ISIS kwao adui sio dini hizo na kabila la Kurd adui yao mkubwa ni waislam wenzao wa dhehebu la SHIA na ukitazama ni kama vile mtusi kumbagua mhutu ukitafuta utakuta ni chuki za kutengwa pale watu wa dini au dhehebu fulani wanapokuwa madarakani kujipendelea.
 

Siwezi kuendelea kubishana na mtu kama wew ambaye hata hujui unasimamia nini! Kuna mdau huko nyuma kaeleza situation zote za maeneo mengine kama yale mfaransa aliyoingilia mf. CAR. Mogadishu kuna kundi la watu wamekaa kwa amani then watu wenye silaha wanaenda kuwaua?
 

Kwahiyo jibu liko wazi awaendi kwasababu ni against Humanity wanakwenda kwasababu wana interest zao pale.Though wote tunajua mauaji na ugaidi vyote avifai kwa mtu yoyote.
 
sema upeo wako umeishia hapo
 
Haya masuala ya sasa huko Iraq inanikumbusha vita vya Kosovo, Bosnia, Serbia ambazo ziliyokuwa sehemu ya Federation of Yugoslavia na NATO ikiongozwa na USA, UK, France wakaigilia kati matatizo ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani.

Muungano wa NATO ni kawaida yao kuingilia kati matukio mbalimbali kama wao ndiyo watetezi wa 'wanyonge' au 'wachache' sehemu nyingi huko ulaya na mashariki ya kati, historia inatufunza iwe ya ISIS ya Iraq, Serbia, Kosovo n.k

Tutizame yale ya Bosnia, Kosovo na Serbia yanavyoshahabiana na ya sasa Iraq ambayo Mhadhiri wa UDSM pia angeyapitia kutupa uchambuzi wa siasa za mahusiano ya kimataifa ktk eneo hili:

Kosovo lies in southern Serbia and has a mixed population of which the majority are ethnic Albanians. Until 1989, the region enjoyed a high degree of autonomy within the former Yugoslavia, when Serbian leader Slobodan Milosevic altered the status of the region, removing its autonomy and bringing it under the direct control of Belgrade, the Serbian capital.

Facts and figures
  • Between March 1998 and March 1999, before NATO governments decided upon military action, over 2000 people were killed as a result of the Serb government's policies in Kosovo.
  • During the summer of 1998, a quarter of a million Kosovar Albanians were forced from their homes as their houses, villages and crops were destroyed.
  • In January 1999, evidence was discovered, by a United Nations humanitarian team, of the massacre of over 40 people in the village of Racak.
  • By the beginning of April 1999, the United Nations High Commission for Refugees estimated that the campaign of ethnic cleansing had resulted in 226,000 refugees in Albania, 125,000 in the former Yugoslav Republic of Macedonia (1), and 33,000 in Montenegro.
  • Assistance given by NATO forces to alleviate the refugee situation included providing equipment and building camps to house 50,000 refugees in Albania; assistance in expanding camps in the former Yugoslav Republic of Macedonia (1); providing medical support and undertaking emergency surgery on the victims of shootings by Serb forces; transporting refugees to safety; and providing transport for humanitarian aid and supplies.
  • By the end of May 1999, over 230,000 refugees had arrived in the former Yugoslav Republic of Macedonia (1), over 430,000 in Albania and some 64,000 in Montenegro. Approximately 21,500 had reached Bosnia and over 61,000 had been evacuated to other countries. Within Kosovo itself, an estimated 580,000 people had been rendered homeless.
  • It is estimated that by the end of May, 1.5 million people, i.e. 90% of the population of Kosovo, had been expelled from their homes. Some 225,000 Kosovar men were believed to be missing. At least 5000 Kosvars had been executed.
  • NATO forces have flown in many thousands of tons of food and equipment into the area. By the end of May 1999, over 4666 tons of food and water, 4325 tons of other goods, 2624 tons of tents and nearly 1600 tons of medical supplies had been transported to the area.
Source: http://www.nato.int/kosovo/history.htm

 
Ndugu zangu, hebu tujaribu kubadilika kidogo. Nadhani kuna tatizo kubwa sana nchini.
1. Kushindwa kuelewa maana
2. Kushindwa katika muktadha ulikosudiwa
3. Kuangalia mambo kwa kicho la dini. Gonjwa baya sana hili.


Mleta mada kaangalia mahojiano na kuona mambo mawili, ukristo na Uislam. Kakokotoa maneno yake na kuondoa mada halisi iliyojadiliwa. Huu ni ugonjwa mbaya sana wa kushindwa kufanya analysis ya mambo kama watu huru.
Niseme hizi dini zinazidi kupumbaza watu badala ya kuwajenga. Niwieni radhi mtakaokereka na mtazamo huo.

Siasa za mashariki ya kati haziangaliwi kwa jicho jepesi. Kwa maoni yangu, alichopinga Bushiri Ali ni kitendo cha Marekani kuwatumia Yazidu kuficha matatizo waliyosababisha siku za nyuma.

ISIS wanaelekea Baghdad, kuna shinikizo ndani ya Marekani kuwa Trillion 2 na askari 5,000 wamepotea kwa jambo lisiloonekana kuwa na manufaa. Walichokitaka Wamarekani ni udhibiti wa Iraq kwa sababu mbili, mafuta na kulinda mshirika wao aliyetishiwa na Saddam, Israel.

Walichokitaka ni kuhakikisha hakuna mbabe mashariki ya kati atakayetishia nchi rafiki kama Saudia na UAE.
Ndilo lengo la kumuondoa Saddam. Sasa ISIS wanaporudi na kutangaza utawala wao, kwa Marekani ni sawa na kuruka hoja majivu ukanyage Moto.

Lakini, kuna challenge pia. Kurudi kwao Iraq kutawalizimu wainge maeneo kama Syria Pia. Obama anataka nchi imalize vita eneo hilo, hivyo lazima atafute sababu za kurudi Iraq ili kulinda masilahi yaliyowapeleka kwa mara ya kwanza.

Njia rahisi ni kuwatumia Yazidu ambao sehemu kubwa ni Wakristo. Hawa wame survive genocide zaidi ya 72 wakati Marekani haikuwepo. Ni kwa kuwatumia, Marekani ikaingia na misaada halafu jana wakashusha kipigo kwa ISIS waliokuwa wanaelekea Baghdad. Ni kutafuta sababu tu za kuwaadhibu ISIS.

Marekani inaelewa kuwa kuacha ISIS itwae Iraq ni kuruhusu Syria ianguke na nchi za mashariki ya kati. Kutakuwa na kibarua kigumu sana cha ku-deal na ISIS ambao wamejinasibu wanataka dola moja mashariki ya kati.

Si kweli kuwa Marekani imekwenda kwasababu ya Wakristo. Laiti ingekuwa hivyo, tungewaona Darful na kwingineko.
Kuna interest zao ambazo usipiziangalia kwa jicho zuri, unaishia katika Uislama na Ukristo.

Hivyo Bushiri alikuwa anatoa analysis kwa maana ya kupinga ulaghai ni sukupinga wale watu ksaidiwa.
Sidhani kama Bushiri haelewi Bosnia Herzegovina nchi za magahribi zikiongozwa na Maekani zilifanya nini.

Hivyo, ningeomba watu wafungue akili zao na kuyaangalia mambo kwa mtazamo mpana, kuziangalia hoja kama zilivyo na si kwa jicho la ukirsto na Uisalam.Ugonjwa huu unaliumiza taifa sana.

Najiuliza angesema Bensona wa UDSM au John wa Mzumbe Unv, leo mleta mada angekuwa na hoja gani.

Nashangaa uzi unaendelea tu kukiwa na habari mstari mmoja bila kufikiria dhana halisi ya mzungumzaji.
Au habari hiyo ingesemwa na Prof Chembelecho tusiyejua ana dini gani, mleta mada angesema nini.

Unapomuangalia mzungumzaji kwa jina na si kwa wasifu au sifa zake, unajinyima nafasi ya kufikiri na kutojitendea haki.

Huu ugonjwa kuangalia majina ni mbaya sana, unapumbaza taifa unawaumbaza vijana.
Leo mtu akiteuliwa, hakuna anayeangalia sifa, jicho ni jina na imani yake.
Hatuwezi kujenga taifa tukiwa na kundi lisiloweza kuchambua mambo, lisilokubali au kupinga hoja kwa hoja.

Mada nzima haizungumziwi kwa kwa kuunga mkono au kupinga hoja, ni udini tu.
Elim yetu ina matatizo lakini hizi dini nazo zinasehemu yake katika kupumbaza watu
 

Katika siku zooote leo umeongea jambo la maana.

Heko.
 
Wewe ndiyo mdini mkubwa jibu swali la Bashiru kwa nini Marekani aendi sehemu zingine kama Gaza kuwasaidia watu wanaouliwa kwa ni hiyo Iraq na Libya?
 

Nguruvi3 shukran kwa darsa lako nadhani watu watajifunza kupitia hii post yako.
 
Last edited by a moderator:

phd=pengine hana degree
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…