Mhadhiri Chuo Kikuu auawa na majambazi

Mhadhiri Chuo Kikuu auawa na majambazi

mamanalia

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2009
Posts
666
Reaction score
146
Wadau najua mmeishaiona hii. Hivi haya mauaji ni ya kijambazi kweli au kuna kitu kinaendelea kwenye system huko. Maskini, Kavenuke!.

Mhadhiri Chuo Kikuu auawa na majambazi
Monday, 27 September 2010 09:40 newsroom .NA MOHAMMED ISSA

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Johns, Dodoma, Damas Kavenuke amefariki dunia baada ya kushambuliwa na majambazi usiku wa kuamkia juzi.Kavenuke alifariki katika Hospitali ya Mkoa wa Mara alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na majeraha makali aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwemo kichwani.

Akizungumza na Uhuru jana kwa njia ya simu, kaka wa marehemu David Kavenuke alisema, mhadhiri huyo alivamiwa na majambazi katika kijiji cha Lugala kilomita nane kutoka kijiji cha Bugushili.

Alisema mhadhiri huyo alikwenda wilayani Musoma kwa ajili ya kusaidia kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Oshadi Mang'ombe inayomilikiwa na Mbunge wa Musoma Vijijini. Nimrod Mkono. Kwa mujibu wa Kavenuke, mhadhiri huyo alikuwa akisaidia kufundisha katika shule hiyo baada ya kuwa kwenye mapumziko na siku ya tukio alikuwa anatoka katika michezo ya shule hiyo, akiwa na dereva wa shule hiyo ambaye alijeruhiwa.

Akizungumzia tukio hilo, alisema marehemu Kavenuke alikuwa katika gari la shule, na walipofika eneo la Lugala walikuta barabara imewekwa gogo kubwa na waliposimama walivamiwa na majambazi zaidi ya watano.

Alisema baada ya kuvamiwa na majambazi hao walikatwakatwa sehemu mbalimbali za miili yao na marehemu alipata majeraha makubwa sehemu za kichwa, ambapo walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kwa matibabu.

Kavinuke alisema kutokana na hali za majeruhi hao kuwa mbaya, Mkono alitoa ndege kwa ajili ya kuwasafirisha majeruhi kuja Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi, ambapo ilishindikana baada ya hali zao kuwa mbaya.

Alisema mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda mkoani Iringa kwa mazishi na kwamba marehemu atazikwa keshokutwa wilayani Mufindi. Marehemu ameacha mjane na watoto wawili na hali ya dereva wa gari hiyo inaendelea vizuri.
 
Je hao majambazi waliiba chochote kwenye hiyo gari?
Na ni wangapi walijeruhiwa vibaya?
Au alilengwa yeye tu?
Pengine tukijua na misimamo yake huko nyuma tuanaweza unganisha dots

RIP
 
Imeniumiza sana maana Kavenuke ni mwalimu wangu wa Chemistry Msalato miaka ya 2002/2003. Baada ya hapo alijiendeleza na alikua idara ya Maths pale UD. Nadhani hajaanza kufundisha St Johh siku nyingi.

Kwa nlivyomfahamu hakua na element za kisiasa, ni kijana mchapa kazi na mpenda michezo.
 
Kama kuna juhudi zinafanyika kujua chanzo halisi cha kifo cha Damas ni tunaomba zifanyike kwa usahihi na majibu yawekwe hadharani. Ninamfahamu kiasi Ndugu Damas akiwa tangu akiwa Malangali Sekondari. Japo binadamu tuna mapungufu, lakini sikuwahi kuwa na mashaka yoyote juu yake na mahusiano ya kijamii. Na zaidi kama alivyosema Hope 2 hapo juu, hakuwahi kuwa na elements za kisiasa.

Raha ya Milele umpe ee bwana
Na mwanga wa milele umwangazie
Astarehe kwa Amani. Amina
 
So sad indeed.
RIP Damas!
"mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi sio nyingi. Naye huchanua kama maua na kisha hunyauka"
 
Halafu unamkuta Kikwete bila aibu anawautangazia umma kwamba CCM imedumisha amani!! Amani gani ili hali kila kona ni mauaji tu ya watu wasiokuwa na hatia? Natamani siku moja hao majambazi wavamie Ikulu. Pengine atatambua kwamba amani ya nchi hii ilishapotea siku nyingi. Sasa hivi tunaishi kwa kubahatisha tu.
 
RIP.

Ukamsalimie Jwani Mwaikusa.

It appears life expectancy ya wahadhiri wa vyuo vikuu ni ndogo.
 
RIP Damas Kavenuke
nimemfahamu toka akiwa malangali, akaenda kufundisha msalato, akafundisha UDSM na kabla mauti hayajamfika alikuwepo Dodoma St. Johns. alikuwa ni mchapakazi sana na mtu wa kujichanganya kwenye jamii na mpenda michezo.
mauaji ya namna hii lazima yathibitiwe na polisi

MUNGU ametoa na MUNGU ametwaa jina lake libarikiwe
 
Wadau najua mmeishaiona hii. Hivi haya mauaji ni ya kijambazi kweli au kuna kitu kinaendelea kwenye system huko. Maskini, Kavenuke!.

Mhadhiri Chuo Kikuu auawa na majambazi
Monday, 27 September 2010 09:40 newsroom .NA MOHAMMED ISSA

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Johns, Dodoma, Damas Kavenuke amefariki dunia baada ya kushambuliwa na majambazi usiku wa kuamkia juzi.Kavenuke alifariki katika Hospitali ya Mkoa wa Mara alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na majeraha makali aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwemo kichwani.

Akizungumza na Uhuru jana kwa njia ya simu, kaka wa marehemu David Kavenuke alisema, mhadhiri huyo alivamiwa na majambazi katika kijiji cha Lugala kilomita nane kutoka kijiji cha Bugushili.

Alisema mhadhiri huyo alikwenda wilayani Musoma kwa ajili ya kusaidia kufundisha katika Shule ya Sekondari ya Oshadi Mang'ombe inayomilikiwa na Mbunge wa Musoma Vijijini. Nimrod Mkono. Kwa mujibu wa Kavenuke, mhadhiri huyo alikuwa akisaidia kufundisha katika shule hiyo baada ya kuwa kwenye mapumziko na siku ya tukio alikuwa anatoka katika michezo ya shule hiyo, akiwa na dereva wa shule hiyo ambaye alijeruhiwa.

Akizungumzia tukio hilo, alisema marehemu Kavenuke alikuwa katika gari la shule, na walipofika eneo la Lugala walikuta barabara imewekwa gogo kubwa na waliposimama walivamiwa na majambazi zaidi ya watano.

Alisema baada ya kuvamiwa na majambazi hao walikatwakatwa sehemu mbalimbali za miili yao na marehemu alipata majeraha makubwa sehemu za kichwa, ambapo walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kwa matibabu.

Kavinuke alisema kutokana na hali za majeruhi hao kuwa mbaya, Mkono alitoa ndege kwa ajili ya kuwasafirisha majeruhi kuja Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi, ambapo ilishindikana baada ya hali zao kuwa mbaya.

Alisema mwili wa marehemu utasafirishwa leo kwenda mkoani Iringa kwa mazishi na kwamba marehemu atazikwa keshokutwa wilayani Mufindi. Marehemu ameacha mjane na watoto wawili na hali ya dereva wa gari hiyo inaendelea vizuri.

ndugu kwa HILI kama ni MARA MUSOMA NI JAMBO LA KAWAIDA WAO DAMU YA BINADAMU NI KAMA YA NGOMBE NA MBUZI KULE DODOMA...MUNGU AMPE RAHA YA MILELE NA MWANGA WA MILELE AMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI..
 
Back
Top Bottom