Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
NB: Baadhi yetu tuliofurahishwa na sehemu ya kwanza ya ushambulizi wa kihoja na kiakili wa hotuba ya vitisho kwa wafanyakazi ya Rais Kikwete tumempa moyo Mhadhiri Bakari Mohammed wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na kupendekeza kwake kwamba japo sehemu ya kwanza ilikuwa imegusa kwa kiasi matatizo ya kifalsafa na kimantiki ya hotuba ya Kikwete Bw. Mohammed angeweza kwenda mbele zaidi. Nashukuru kwamba Bw. Bakari ameenda mbele zaidi katika sehemu hii ya pili ya majibu yake kwa hotuba ya Rais Kikwete. Kinachofurahisha zaidi ni uwezo uliokubuhu wa kuweza kuunganisha hoja zake na sehemu ya historia yetu. Kwa tulio mashabiki wa fikra za Nyerere tumefurahishwa na utetezi wa hoja zake kwa kutumia mojawapo ya hazina kubwa za kifikra yaani hoja za Mwalimu hasa kutoka kijitabu maarufu (ambacho Watanzania wengi nina uhakika hawajawahi kukisoma licha ya kukisikia, yaani "TUJISAHIHISHE". Sehemu hii ya pili ina lengo la kugusa dhamira ya Kikwete na kuamsha dhamira za wananchi kuelewa kuwa mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kuwa endelevu (the unsustainability of a corrupt political system). Soma kwa furaha!
HOTUBA YA RAIS KIKWETE (2)
UPEMBUZI WA KITAKWIMU NA KIASTROLOJIA
§ Takwimu za bajeti zabainisha alivyopotoshwa
§ Vitisho, jazba, na kebehi nini ishara yake?
§ Ilikuwaje Siku ya Jumatatu?
§ Ushauri elekezi
Watanzania, wa hali zote za maisha (masikini, matajiri, wakulima, wafanyakazi, wakwezi, wasomi na wanazuoni) bado tungali wanaitafakari hotuba ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa siku ya Jumatatu tarehe 3, Mei 2010. Pamoja na jitihada za mtu mmoja mmoja, vikundi vvya watu hata wazee wastaafu (kama Rais wa Awamu ya Pili Mzee Ruksa) wanaitafakari hotuba ile na hatma ya Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010 na miaka mitano ijayo! Kwa kuwa (1) takwimu, (2) vitisho, jazba, na kebehi, na (3) Siku ya Jumatatu vilitumika; kwa hivyo basi, makala haya yanajaribu kupembua: (1) vielelezo vya takwimu za bajeti ili kuona uhalali wa shilingi trilioni 6.85293; (2) ishara ya hamaki aliyoionesha Rais wa Nchi; na (3) Upembuzi wa Sayari ya Jumatatu.
Ukiisoma Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2009/2010 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Mheshimiwa Mustafa Haidi Mkullo (MB) aliyoisomwa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) tarehe 11 Juni, 2009 na inayopatikana kwenye www.mof.go.tz/mofdocs/budget na kwenye wavuti wa Bunge la JMT ina mengi ya kelezea juu ya mwelekeo wa gharama za mishahara ya watumishi wa Serikali. Pamoja na mambo mengine na kwa kurahisisha haja ya upembuzi tufanye udondozi, upekuzi na uchambuzi wa taarifa za takwimu juu ya malipo ya mishahara peke yake. Jedwali lifuatalo limenyofolewa (detached) kutoka kwenye Jedwali 2a na Jedwali 2b ya Hotuba ya Bajeti 2009/2010.
Download: