Mhadhiri Bakari Muhammed amng'ang'ania Kikwete - Sehemu ya 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhadhiri Bakari Muhammed amng'ang'ania Kikwete - Sehemu ya 2

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 9, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  NB: Baadhi yetu tuliofurahishwa na sehemu ya kwanza ya ushambulizi wa kihoja na kiakili wa hotuba ya vitisho kwa wafanyakazi ya Rais Kikwete tumempa moyo Mhadhiri Bakari Mohammed wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na kupendekeza kwake kwamba japo sehemu ya kwanza ilikuwa imegusa kwa kiasi matatizo ya kifalsafa na kimantiki ya hotuba ya Kikwete Bw. Mohammed angeweza kwenda mbele zaidi. Nashukuru kwamba Bw. Bakari ameenda mbele zaidi katika sehemu hii ya pili ya majibu yake kwa hotuba ya Rais Kikwete. Kinachofurahisha zaidi ni uwezo uliokubuhu wa kuweza kuunganisha hoja zake na sehemu ya historia yetu. Kwa tulio mashabiki wa fikra za Nyerere tumefurahishwa na utetezi wa hoja zake kwa kutumia mojawapo ya hazina kubwa za kifikra yaani hoja za Mwalimu hasa kutoka kijitabu maarufu (ambacho Watanzania wengi nina uhakika hawajawahi kukisoma licha ya kukisikia, yaani "TUJISAHIHISHE". Sehemu hii ya pili ina lengo la kugusa dhamira ya Kikwete na kuamsha dhamira za wananchi kuelewa kuwa mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kuwa endelevu (the unsustainability of a corrupt political system). Soma kwa furaha!

  HOTUBA YA RAIS KIKWETE (2)
  [FONT=&quot]UPEMBUZI WA KITAKWIMU NA KIASTROLOJIA[/FONT]

  § Takwimu za bajeti zabainisha “alivyopotoshwa”
  § Vitisho, jazba, na kebehi nini ishara yake?
  § Ilikuwaje “Siku ya Jumatatu”?
  § Ushauri “elekezi”

  Watanzania, wa hali zote za maisha (masikini, matajiri, wakulima, wafanyakazi, wakwezi, wasomi na wanazuoni) bado tungali wanaitafakari hotuba ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa siku ya Jumatatu tarehe 3, Mei 2010. Pamoja na jitihada za mtu mmoja mmoja, vikundi vvya watu hata wazee wastaafu (kama Rais wa Awamu ya Pili – Mzee Ruksa) wanaitafakari hotuba “ile” na hatma ya Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010 na miaka mitano ijayo! Kwa kuwa (1) takwimu, (2) vitisho, jazba, na kebehi, na (3) Siku ya Jumatatu vilitumika; kwa hivyo basi, makala haya yanajaribu kupembua: (1) vielelezo vya takwimu za bajeti ili kuona uhalali wa shilingi trilioni 6.85293; (2) ishara ya hamaki aliyoionesha Rais wa Nchi; na (3) Upembuzi wa Sayari ya Jumatatu.


  Ukiisoma Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2009/2010 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Mheshimiwa Mustafa Haidi Mkullo (MB) aliyoisomwa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) tarehe 11 Juni, 2009 na inayopatikana kwenye www.mof.go.tz/mofdocs/budget na kwenye wavuti wa Bunge la JMT ina mengi ya kelezea juu ya mwelekeo wa gharama za mishahara ya watumishi wa Serikali. Pamoja na mambo mengine na kwa kurahisisha haja ya upembuzi tufanye udondozi, upekuzi na uchambuzi wa taarifa za takwimu juu ya malipo ya mishahara peke yake. Jedwali lifuatalo limenyofolewa (detached) kutoka kwenye Jedwali 2a na Jedwali 2b ya Hotuba ya Bajeti 2009/2010.


  Download:
   

  Attached Files:

 2. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mhadhiri Bakari ni mchambuzi jasiri, makini na mahiri kabisa... ila kidogo sehemu hii ya pili imenishangaza baadhi ya sehemu hasa pale alipoingiza mamabo ya Sheikh Yahya...kidogo naanza kuwa na shaka na mwelekeo wake.."Mtabiri huyo anayetambulika nchini na Afrika ya Mashariki, Kusini na Kati na hata Falme za Kiarabu na Ulaya ameorodhesha mambo kumi na sita (16) yanayotawaliwa na "Sayari ya Jumatatu" na kati ya hayo mambo matano (5) makubwa yalitokea "Siku ya Jumatatu" ya tarehe 3 Mei, 2010"
   
 3. m

  mtemi Member

  #3
  May 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmeshaharibu sasa......na shekh yahaya tena..
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Labda JK atamuelewa vizuri!!
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  May 9, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Huyu Mhadhiri ajiandae kufukuzwa kazi kama wengine wa huko nyuma.Mizengwe iko mbele yake inakuja..Hii nchi bana sijui ikoje.
   
 6. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Huyu Mhadhiri ni mahiri pia katika matumizi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Sikujua kwamba Probability theory kwa Kiswahili ni Nadharia ya Yumkini. Interesting...
   
 7. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Bwana Mohamed Bakari umetusaidia sana kuichambua hotuba ya Mhe JK.

  Kweli tumetambua mapungufu mengi na bila shaka serikali na washauri wa Rais wanajiuliza n wapi walipopotoshwa na ni nani alikuwa na dhamira ya kuuficha ukweli huu.

  Kasoro ndogo niliyoiona katika makala yako ni unajimu! Hatuhitaji nyota kuona serikali hii isivyokuwa na lengo la kumkomboa mfanyakazi! Hatuhitaji ramri kuona serikali ya JK isivyokuwa na mpango endelevu! sasa kama huwezi lipa mshahara 315000 hata kama ungepewa miaka 8 unagombea urais wa nini? Mambo ya wanajimu tuwaachie wanajimu, ukweli unajulikana na uko wazi ni hesabu ya kujumlisha na kuota tu basi!
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Haya tena kumekucha.................Mkuu Bakari kwa mara nyingine shukurani sana
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Suala pale haliko kwenye unajimu....................suala zima liko kwenye zile baadhi ya hoja kuhusu jumatatu alizowakilisha...............the statements are valid!.....
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  May 9, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0

  Nimeupenda huu uchambuzi wa Bakari lakini maenigusa zaidi alivyoonesha msisitizo kwenye hiki kipengele pamoja na mapendekezo yake ya jinsi ya kuongeza pato la taifa..Kama alivyoainisha hapa chini.Nikubaliane na yeye pia katika ushauri aliompa Mhe Rais kwani bado hajachelewa fursa ya kujirekebisha anayo.


  Kwa kuwa, kwa mujibu wa Kiambatisho Na. 4b (Hotuba ya Waziri wa Fedha na Uchumi 2009/2010), mishahara ya Serikali ni asilimia 19 ya matumizi yote yaliyokadiriwa kufikia shilingi milioni 9,513,685 (sawa na trilioni 9.514 hivi) si kweli kusema kwamba KCC kikiwa shilingi 315,000.00 Serikali itashindwa kulipa! Serikali inao uwezo wa kulipa KCC na isiathirike kabisa! Unaotakiwa ni utashi wa kisiasa ili kuhakikisha kwamba:

  (1) Mfumo wa ukusanyaji kodi unakuwa makini na wenye ufanisi kwa kuondoa aina zote za ukwepaji na misamaha holela ya kodi;
  (2) Wigo wa kodi unapanuliwa kwenye sekta nyeti za madini na utalii ili kutega mapato mengi zaidi kwa gharama ndogo ya ukusanyaji wake;
  (3) Wafanyabiashara wakubwa na wa kati wenye biashara (wawekezaji) kwenye sekta zote wanabanwa vema na sheria katika kufidia uharibifu wa mazingira kwa kulipa "fidia" stahiki itakayobebeshwa kwenye kodi-ambatano;
  (4) Matumizi ya Serikali yanadhibitiwa kwa umakini mkubwa kwa kuondoa aina zote za matumizi yasiyo ya lazima na anasa za safari, warsha, makongamano na starehe nyingine zisizo kuwa na tija; na
  (5) Serikali ichukuwe hatua za makusudi katika kurasmisha walipa kodi wadogowadogo ili kuwajengea uwezo wa kulipa kodi na kuongeza uwezo wao wa kuzalisha mali na ziada.

  Sidhani kama Serikali makini inaweza kushindwa kuelekeza nguvu zake katika kuhakikisha inasimamia sekta muhimu ya fedha na uchumi ili kuongeza mapato na kupunguza utegemezi. Napenda kuikumbusha Serikali kwamba kama wafanyakazi watawezeshwa, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza tija na kuzifanya sekta za huduma na uzalishaji mali kutoa tija inayokusudiwa.
   
 11. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani unajimu si taaluma kama taaluma nyingine, kwanini watu wanapenda kupuuzia unajimu??? Unajimu na Uchawi ni vitu viwili tofauti..!
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Great philosopher! Upembuzi makini asante sana
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Watanzania wanabadilika ingawa viongozi wanafikiri bado mambo ni yale yale. Kuwaita wazee wa Dar ili kutaka kpata support ya kitu ambacho ni wazi hakiko sawa ni upotezaji wa muda. naona siku hizi resources zetu nyingi zinaelekezwa huko kwenye upotezaji wa muda kwenye mambo yasiyo na tija hata kidogo kwa Taifa. Namshukuru mchambuzi kwa kuonyesha ni jinsi gani watawala hawajui wanalofanya. Wanafikiria bado ni enzi zile za kulishana maneno na kutegemea watu watashiba wasihoji nini kinachoendelea.
  Kila kitu kina kikomo.
   
 14. M

  Mundu JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  May 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  uchambuzi wa muhadhiri wa chuo kikuu mzumbe Mohamed Maligwa...umeenda shule ,umetulia sana ni busara basi anayetaka kuupinga aje na waraka kama wake...maana hapa jf ni hoja kwa hoja ...hoja nzito kamwe haipingwi na hoja shallow .........

  ....ni wazi kuwa rais kikwete ameshagundua kuwa alikosea na kukurupuka....na hata tulio na uwezo wa kusoma uso wa mtu na kujuwa...tangu mwanzo tuliona ...hali aliyokuwa nayo na kupata wasi wasi mkubwa hata wa afya yake ....he looked unfocused than ever..to the extent of requring medical and psychological attention ...he was in total disray..and in poor state of mind.....nimerudia kuangalia ile video clip...and satisfy my self kuwa we are right ...kuhisi kuwa rais alipokuwa akitoa hotuba ile hakuwa kwenye hali nzuri ya afya na akili...[rudieni kuangalia]..nyuma ya rais kwa kawaida kunakuwa na..aide de camp mmmoja na wengine husimama kwa mbali...au kukaa...but that day nyuma yake viti vitatu walikaa wasaidizi mahsusi wa usalama ,ambapo daktari wake alikaa nyuma yake kabisa na ndiye aliyekuwa akimmiminia maji ya glucose mara kwa mara....pia walikuwepo nyuma yake washauri [secretaries] wawili...ambao mara zote they seated leaned toward his chair...and one of them was always noddin his head.....wakiwa pamoja na kapuya....idadi ya wasaidizi waliokuwa nyuma ya rais siku ile ilisababisha hadi wakuu wa vyombo vya usalama kukaa kwa mbali kidogo nyuma.....

  mpangilio wa maneno ya rais na kurudia rudia kauli bila utaratibu ni dhahiri kuwa hata kama wasaidizi walimuandikia detail nzuri basi alishindwa kufikisha hadhirani..kutokana na pressure aliyokuwa nayo na hasira juu...nachelea kuwatupia washauri wake lawama....nahisi inawezekana mara zote wanamshauri vema basi akichanganya na akili zake anaharibu ndio maana anashindwa kuwafukuza.......

  rais wetu ni wazi kuwa anao udhaifu mkubwa wa kutopenda kujisomea .....na kubaki kutegemea kuandaliwa kila kitu...ni hatari hii....ushahidi ni namna alivyoweza kusaini sheria kubwa kama ya uchaguzi bila hata kupitia madokezo.....ya washauri wake wa sheria na pia yeye mwenyewe kuisoma......urais ni kazi inayotaka sana kusoma ...kwani washauri wakijuwa kuwa husomi haata maofisini basi watakuchomekea mambo kwa faida yao......ni hatari...
  sasa tujiulize ni muda gani rais wetu anapata kusoma makabrasha mbalimbali anayowekewa mezani..........au anawaambia kina mbena na januari...".someni tu ....mkiona sawa niwekeeni mezani nisaini..!!"...ndio kwa kuwa mara zote yupo safarini....au matembezini au anapiga soga.....ni hatari sana hasa kama rais wa nchi anakutana na hotuba zake jukwaani kwa mara ya kwanza....na kwa kujianya naye "nyerere" akataka kuhutubia pasi kuonekana anasoma sana hotuba..ni dhahiri atapotosha kabisa hotuba aliyoondaliwa na washauri...basi na washauri wakijuwa waanaandaa hotuba hazifuatwi na mambo yanaongewa kinyume basi hata hotuba zinazofuata wataandaa bila umakini!! ndicho kinachooendelea ikulu!!

  viongozi wote waliotangulia kama nyerere ,mwinyi na mkapa walikuwa na muda wa kukaa ikulu na kusoma nyaraka zao si huyu!!...makosa mengine anatakiwa awe na uwezo wa kuyaona...kabla ya kusoma kwa watu....naomba lets keep washauri ..in these...washajuwa kuwa yeye kiazi!!

  Tazameni hata kikwete anavyotoa hotuba zake kwenye makongamano na marais wenzake utaona kuwa hoja zake zipo too shallow na hurudia hizo hizo kila forum...ni wazi general knowledge yake ni ndogo kuliko ya wenzake..yote he because hasomi ..vitabu wala majarida na machapisho mbali mbali ......ni lazima abadilike ....la sivyo viongozi wenzake watakuwa pia wanamshangaa......
   
 16. n

  nndondo JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Kwani alipata alama gani kwenye degree yake pale mlimani, PASS kama ya mwanawe Ridhwani? natumaini angalau wakati ule hakuhitajia jaji Juma kumtetea asifukuzwe shule japo hakupata alama za kuendelea na wote tunajua, muulizeni prof Shivji haya. Mkapa tunajua ana hons tena ya kiingereza na hobby yake ni kusoma. Yeye anaandika hotuba zake mwenyewe lakini bado anasoma kwa kuwa anajua na kuheshimu taratibu za 'public speaking'. Hata first class material wa Harvard Rais Obama anasoma kwanza hotuba zake kabla ya kuja kuzitoa. Pili jamani let us be fair hata hao waandishi wanatuacha hoi kwa hiyo huyu Galanos Boy wa juzi hata ukele haujamtoka ndio wakuandaa hotuba? aliwekwa abebwe na yule jamaa wa ukerewe sasa jamaa yuko wizara ya habari mtoto hana mbeleko. Ndio hayo, hivi mnaamini katika forum ya uchumi wa afrika kaleta mambo ya Zinduka na Malaria? si kituko hicho?
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu Phil............shukran kwa hilo hapo juu.....................natumaini ujumbe ameupata..............dereva wa gari letu....inabidi achukue hatua za ziada.......kuhusu kusoma.................
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .............hayo ndio matatizo ya kuleta mzaha kwenye issue serious Mkuu...............experience ni kitu muhimu sana..............Mkapa alimuacha JK Foreign akidhani jamaa ata-gain experience kuhusu kazi kumbe wapi...............we are doomed.............
   
 19. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tazameni hata kikwete anavyotoa hotuba zake kwenye makongamano na marais wenzake utaona kuwa hoja zake zipo too shallow na hurudia hizo hizo kila forum...ni wazi general knowledge yake ni ndogo kuliko ya wenzake..yote he because hasomi ..vitabu wala majarida na machapisho mbali mbali ......ni lazima abadilike ....la sivyo viongozi wenzake watakuwa pia wanamshangaa......[/QUOTE]

  Mkuu hii nimeona kwenye WEF hivi karibuni...jamaa alikuwa anarudia rudia tu mambo!Ila tatizo la kutopenda kusoma ni la sehemu kubwa sana ya watanzania.Wengine majumbani wana-shelf ya vitabu ila hawajawahi kusoma ni kama urembo.Jamani tusome...tujengee na watoto wetu tabia ya kupenda kusoma kwani inasaidia sana katika kukuza uwezo wa kufikiri,kujenga hoja na pia udadasi ambayo ni mambo ya msingi sana katika ku-excel hapa duniani.
   
 20. b

  bnhai JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Andiko langu litatofautiana kidogo na wengi. Kwanza nampa pongezi Bakari kwa kurekebisha hesabu zake za kwanza. Ila angekuwa muungwana kwa kukana hesabu zake katika toleo la kwanza. Angalau sasa tunaweza kujadili facts.
  Hizo figure zako ni stagnant? Kuna vitu vingi hujaviaacount. Naomba nikukumbushe baadhi ya mambo muhim ambayo umeyaacha. Mosi; Wafanyakazi hupanda vyeo. Mf wewe katika sekta uliopo unaweza kuwa mhadhiri kamili baadae. Sasa kila sekta watu hupanda vyeo. Pili umesahau kwamba serikali kwa sasa hivi inaajiri saana sekta ya kilimo, afya na elimu. Sijui hesabu za hao watu umeziaccount vipi. Tukiachana na hesabu hizo, in real world serikali ikilipa mshahara huo based on yr hesabu ninakuhakikishia ni lazima ifilisike. Kwahiyo ishu iwe ni ukweli kwa kusimamia taaluma na ni vyema pia ukaanisha na madhara kwa uchumi wetu kama mishahara hiyo italipwa. Pia hoja zako zinasahau kuainisha matumizi mengine muhim ya serikali km miundo mbinu nk.
   
Loading...